Kuwekeza kunawezakuwa na tija lakini ni vizuri wakajifunze kwa Mkoa wa Dar es Salaam ambao ulikuwa na vitega uchumi chini ya DDC. Vile vile kuna Chama cha Ushirika cha Mkoa Kilimanjaro, kilikuwa na KNCU Hotel lakini miradi hiyo haiingizi fedha tena kama ilivyokuwa imetarajiwa.Tatizo kubwa la Halmashauri nyingi ni baraza la madiwani kukosa watu wabunifu wa vyanzo vya mapato ndani. Je ! wakuu wa idara na Vitengo mbalimbali ambao ni wataalamu washauri wanatekeleza jukumu lao katika Baraza la madiwani; na wanatimiza wajibu kama wataalamu kuwasaidia wakurugenzi katika utekelezezaji wa shughuli mbalimbali katika kila idara na vitengo kwa mafanikio ya halmashauri ? Vema halmashauri nyingine kujifunza kwa jiji la dodoma