Waziri Jafo: Asiyekuwa na kitambulisho au hana kundi asiruhusiwe kufanya biashara

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,877
6,326
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jafo amewapa wiki mbili Viongozi wa Sekretarieti za Mikoa, na Mamlaka za Serikali za Mitaa kuhakikisha kuwa ndani ya wiki mbili kuanzia sasa wawe wamesimika mfumo wa kutambua orodha ya majengo na mabango yaliyopo katika maeneo yao ili kurahisisha ukusanyaji wa kodi na ushuru.

Akizungumza wakati wa kikao kilicho wakutanisha, Makatibu Tawala wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa nchini leo jijini Dodoma, Mhe. Jafo amesema, changamoto kubwa ambayo inasababisha zoezi la ukusanyaji kodi za majengo ni kutokuwepo kwa orodha kamili ya majengo katika mamlaka husika.

Hivyo, amesema suluhu ya kudumu itakayosaidia kuyabaini kwa wepesi na kurahisisha ukusanyaji wa kodi za majengo na ushuru wa mabango ni kuwepo kwa mfumo utakaosaidia kuyabaini majengo yote na mabango na kuhifadhi kumbukumbu hizo katika Kompyuta.

“Tunataka kuanzia tarehe 05 hadi 28 Februari, 2021, iwe ni kazi ya kubainisha majengo yote yanayopaswa na ambayo yanakidhi kulipiwa kodi,” amesema Waziri Jafo na kuongeza kuwa nyumba za matope zimeondolewa katika utaratibu huu.

“Kila Mtendaji wa Mtaa, Mwenyekiti wa Kijiji anatakiwa kuwa na takwimu za majengo yote yanayopaswa kulipiwa kodi, Mkurugenzi hakikisha kuwa Mtendaji wako wa Kijiji au Mtaa anakupatia takwimu ndani ya Wiki mbili kuanzia leo,” alisisitiza Mhe. Jafo.

Waziri Jafo amesema, Wakurugenzi wa Halmashauri watatakiwa kuwasilisha kanzi data hizo ngazi ya Wilaya kwa ajili ya uhakiki kwa Mkuu wa Wilaya, kabla ya kuwasilisha ngazi ya Mkoa kwa Katibu Tawala wa Mkoa na ifikapo tarehe 04 Machi, 2021 zoezi hilo liwe limekamilika na taarifa ya majumuisho iwe imetumwa kwa Katibu Mkuu TAMISEMI.

Waziri amesisitiza kuwa, taarifa hizo zitatakiwa kuanisha nyumba, mmiliki na mawasiliano yake kwa wepesi wa rejea, ambapo mara baada ya hapo, itafanyika kampeni maalum ya kuanza kukusanya kodi ya majengo nchi nzima, itakayoanza tarehe 22 Machi hadi tarehe 05 Aprili, 2021.

“Tunataka huko mbeleni hizi Mamlaka za Serikali za Mitaa ziweze kufanya baadhi ya shughuli za Maendeleo zenyewe, hivyo katika zoezi hili tutaweka mfumo maalum utakaoweza kuona mambo kadhaa yanayo endelea nchi nzima kwenye kazi hii, hatutaki watu washindane bali tunataka kila Halmashauri iwe ya kwanza,” amesema Mhe. Jafo.

Kuhusu vitambaulisho vya wajasiriamali, Waziri Jafo, amesema tayari vitambulisho million 1.6 vimechapishwa na mamlaka ya Mapato Tanzania na kusambazwa katika Mikoa.

“Huu ndio mwanzo na maelekezo ya Serikali, ambayo yatakuwa katika makundi matatu, Wafanya Biashara wakubwa wanaolipa kodi TRA, Wafanyabishara wa kati wenye Leseni za Halmashauri na kundi la tatu ni wenye Vitambulisho vya Mjasiriamali, kila mmoja wetu lazima awe sehemu ya kundi moja wapo” amesema Waziri Jafo

Amesema kuwa asiyekuwa na kitambulisho au hana kundi lolote kati ya hayo, asiruhusiwe kufanya biashara.

Kwa upande wake Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Fedha, Aldolf Ndunguru amesema pamoja na kwamba zoezi la kukusanya kodi hizo limehamishiwa Mamlaka za Serikali za Mitaa bado anaamini ushirikishwaji madhubuti wa viongozi katika maeneo mbali mbali utawezesha kukabiliana na mianya ya upotevu wa mapato ya Serikali.

Akitoa salamu za Mamlaka ya Mapato nchini, Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato nchini TRA, Dkt Edwin Mhede, ametaka kuwepo ushirikiano na Wakuu wa Wilaya kwani maeneo hasa ya upande wa forodha bado hali siyo nzuri kama matarajio na malengo yao yalivyo, hivyo akaomba msaada wa karibu kutoka kwa viongozi hao ambao ni wenyeviti wa Kamati za ulinzi za Wilaya.
 
Sijui kama anajua kuwa makusanyo ya kodi yanakuja na sheria yake kila. Je, kodi za majengo zimepitishwa lini na bunge liwa zirejeshwe halmashauri? Asikurupuke wakati serikali imeingia gharama kununua mifumo hiyo.
 
Vitambulisho vya mjasiriamali sawa, ila viwe kama daraja la kumkuza mfanyabiashara na sio mtu anahamishia "supermarket" kando kando ya barabara kwa kodi ya 20,000 kwa mwaka!!! Sasa wenye supermarket na efd machines watapata wapi wateja ili Kodi zilipike!? Jamani Waziri
 
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jafo amewapa wiki mbili Viongozi wa Sekretarieti za Mikoa, na Mamlaka za Serikali za Mitaa kuhakikisha kuwa ndani ya wiki mbili kuanzia sasa wawe wamesimika mfumo wa kutambua orodha ya majengo na mabango yaliyopo katika maeneo yao ili kurahisisha ukusanyaji wa kodi na ushuru.

Akizungumza wakati wa kikao kilicho wakutanisha, Makatibu Tawala wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa nchini leo jijini Dodoma, Mhe. Jafo amesema, changamoto kubwa ambayo inasababisha zoezi la ukusanyaji kodi za majengo ni kutokuwepo kwa orodha kamili ya majengo katika mamlaka husika.

Hivyo, amesema suluhu ya kudumu itakayosaidia kuyabaini kwa wepesi na kurahisisha ukusanyaji wa kodi za majengo na ushuru wa mabango ni kuwepo kwa mfumo utakaosaidia kuyabaini majengo yote na mabango na kuhifadhi kumbukumbu hizo katika Kompyuta.

“Tunataka kuanzia tarehe 05 hadi 28 Februari, 2021, iwe ni kazi ya kubainisha majengo yote yanayopaswa na ambayo yanakidhi kulipiwa kodi,” amesema Waziri Jafo na kuongeza kuwa nyumba za matope zimeondolewa katika utaratibu huu.

“Kila Mtendaji wa Mtaa, Mwenyekiti wa Kijiji anatakiwa kuwa na takwimu za majengo yote yanayopaswa kulipiwa kodi, Mkurugenzi hakikisha kuwa Mtendaji wako wa Kijiji au Mtaa anakupatia takwimu ndani ya Wiki mbili kuanzia leo,” alisisitiza Mhe. Jafo.

Waziri Jafo amesema, Wakurugenzi wa Halmashauri watatakiwa kuwasilisha kanzi data hizo ngazi ya Wilaya kwa ajili ya uhakiki kwa Mkuu wa Wilaya, kabla ya kuwasilisha ngazi ya Mkoa kwa Katibu Tawala wa Mkoa na ifikapo tarehe 04 Machi, 2021 zoezi hilo liwe limekamilika na taarifa ya majumuisho iwe imetumwa kwa Katibu Mkuu TAMISEMI.

Waziri amesisitiza kuwa, taarifa hizo zitatakiwa kuanisha nyumba, mmiliki na mawasiliano yake kwa wepesi wa rejea, ambapo mara baada ya hapo, itafanyika kampeni maalum ya kuanza kukusanya kodi ya majengo nchi nzima, itakayoanza tarehe 22 Machi hadi tarehe 05 Aprili, 2021.

“Tunataka huko mbeleni hizi Mamlaka za Serikali za Mitaa ziweze kufanya baadhi ya shughuli za Maendeleo zenyewe, hivyo katika zoezi hili tutaweka mfumo maalum utakaoweza kuona mambo kadhaa yanayo endelea nchi nzima kwenye kazi hii, hatutaki watu washindane bali tunataka kila Halmashauri iwe ya kwanza,” amesema Mhe. Jafo.

Kuhusu vitambaulisho vya wajasiriamali, Waziri Jafo, amesema tayari vitambulisho million 1.6 vimechapishwa na mamlaka ya Mapato Tanzania na kusambazwa katika Mikoa.

“Huu ndio mwanzo na maelekezo ya Serikali, ambayo yatakuwa katika makundi matatu, Wafanya Biashara wakubwa wanaolipa kodi TRA, Wafanyabishara wa kati wenye Leseni za Halmashauri na kundi la tatu ni wenye Vitambulisho vya Mjasiriamali, kila mmoja wetu lazima awe sehemu ya kundi moja wapo” amesema Waziri Jafo

Amesema kuwa asiyekuwa na kitambulisho au hana kundi lolote kati ya hayo, asiruhusiwe kufanya biashara.

Kwa upande wake Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Fedha, Aldolf Ndunguru amesema pamoja na kwamba zoezi la kukusanya kodi hizo limehamishiwa Mamlaka za Serikali za Mitaa bado anaamini ushirikishwaji madhubuti wa viongozi katika maeneo mbali mbali utawezesha kukabiliana na mianya ya upotevu wa mapato ya Serikali.

Akitoa salamu za Mamlaka ya Mapato nchini, Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato nchini TRA, Dkt Edwin Mhede, ametaka kuwepo ushirikiano na Wakuu wa Wilaya kwani maeneo hasa ya upande wa forodha bado hali siyo nzuri kama matarajio na malengo yao yalivyo, hivyo akaomba msaada wa karibu kutoka kwa viongozi hao ambao ni wenyeviti wa Kamati za ulinzi za Wilaya
Hizi kodi zote zinaua tabaka la kati middle class ambalo ni muhimu katika kukuza uchumu wanchi, naona kila waziri anakuja kuongea anavyotaka bila kufuata sera na sharia husika, machinga wamesababisha maduka mengi kufunga, na kodi nyingi zinapotea kwa ajiri ya shillingi 20,000 ya kitamburisho.
 
Sijui kama anajua kuwa makusanyo ya kodi yanakuja na sheria yake kila. Je, kodi za majengo zimepitishwa lini na bunge liwa zirejeshwe halmashauri? Asikurupuke wakati serikali imeingia gharama kununua mifumo hiyo.
Mkuu izi Kodi halmashauri wanakusanya tu baada hapo zinapelekwa TRA kwa kutumia control number Kama ilivyo kwenye vitambulisho vya majasirimali mdogo
 
Unajua hawa mawaziri kuna wakati wanapenda kuwachanganya watu na kuwatesa bila sababu za msingi.

Sasa waziri wa Tamisemi Selemani Jafo anaposema wafanyabiashara wanaoruhusiwa ni wale wakubwa, wa Kati na wenye Kitambulisho cha Mjasiriamali amewapanga kwa kutumia vigezo gani?

Ina maana wafanyabiashara wadogo wenye leseni halali yeye hawatambui?

Halafu utakuta 2025 Jafo anachukua fomu ya kugombea urais, yaani CCM bhana!!
Ngoja niishie hapo.

Maendeleo hayana vyama.
 
Hakuna mateso yasiyo na mwisho, hiki ni kipindi cha Watanzania kuteseka, lakini Mungu hatawaacha watu wake wateseke kwa muda mrefu.
 
Uwezi ukawa na wabunge kama Ja people(Sanga) , Tale , msukuma etc ukatoka na mawazo ya kututoa hapa tulipo mpka tufikie nchi tajiri?

Alafu kwasasa Mataga mlipaswa kupeleka hoja zenu kwenye ofisi tu, maana ujinga wa bungeni unatosha na nyinyi mfiche ujinga, kwasababu mpaka sasa tuaona viongozi na Mataga akili hakuna
 
Serikali haiwezi kuendesha nchi kwa kutumia kodi pekee.
Pesa zinawekwa kwenye miradi mingi mikubwa isiyoingizia nchi chochote na isiyo lazima.
Kama hiyo mibudget mikubwa ingewekwa kwenye miradi ambayo itatatua aina fulani ya changamoto humuhumu Tanzania ambapo watanzania wengi wa hali ya chini watafaidika na hivyo serikali itafaidika pia simultaneously tena pakubwa sana.
Then hapo wangeweka budget kwenye mambo yasiyo na ulazima ambayo wananchi wachache ndio wanafaidika.

Yaani seriously hawajui jinsi ya kuweka vitega uchumi zaidi ya kukamua kodi what the hell?

Tanzania kuna changamoto nyingi zinawakabili wananchi wa chini ambao ni wengi Tanzania kama serikali ingeziona na kuzitatua basi ingefaidika pakubwa pamoja na wananchi wote considering pesa ya kutatua hizo changamoto zipo.

Kama wangekuwa na uono wa kuona changamoto hizo in positive way basi wangepunguza kukamua na kubana kodi.

Even uchumi ungekuwa pakubwa well ndo hivyo.
 
Hivo vitambulisho vya mjasiriamali ukivitafuta huko sehemu husika majibu yao always ni kuwa vimeisha 😂😂😂
Hawa jamaa wa kijani walipokua wanasema tutaisoma namba, kwa akili zao walifikiri wanachama wao hawatahusika na kuisoma namba.
Leo sukari
Siment
Mafuta ya kupikia nao wanahusika.
 
Eeh hiki kipigo ni cha nyuzi 360' hamna mtu ambaye hakitamifikia 😁 hata uwe kada mtiifu!!!
 
Serikali ya wanyonge hii. Hakuna nchi kuna raia wapumbavu kama tanzania.Kodi kila sehemu na bado maendeleo ya kawaida.

Kuna baadhi ya bidhaa kodi inalipwa mala nne hadi tano
Acha tuendelee kusifu na kuabudu,huku wengine wakila kuku kwa mrija
 
Serikali haiwezi kuendesha nchi kwa kutumia kodi pekee.
Pesa zinawekwa kwenye miradi mingi mikubwa isiyoingizia nchi chochote na isiyo lazima.
Kama hiyo mibudget mikubwa ingewekwa kwenye miradi ambayo itatatua aina fulani ya changamoto humuhumu Tanzania ambapo watanzania wengi wa hali ya chini watafaidika na hivyo serikali itafaidika pia simultaneously tena pakubwa sana.
Then hapo wangeweka budget kwenye mambo yasiyo na ulazima ambayo wananchi wachache ndio wanafaidika.

Yaani seriously hawajui jinsi ya kuweka vitega uchumi zaidi ya kukamua kodi what the hell?

Tanzania kuna changamoto nyingi zinawakabili wananchi wa chini ambao ni wengi Tanzania kama serikali ingeziona na kuzitatua basi ingefaidika pakubwa pamoja na wananchi wote considering pesa ya kutatua hizo changamoto zipo.

Kama wangekuwa na uono wa kuona changamoto hizo in positive way basi wangepunguza kukamua na kubana kodi.

Even uchumi ungekuwa pakubwa well ndo hivyo.
Watu wenye akili hiyo hawako ccm,na walio nje ya CCM wakisema wanawaundia zengwe mpaka kesi za uhujumu
 
Sijui kama anajua kuwa makusanyo ya kodi yanakuja na sheria yake kila. Je, kodi za majengo zimepitishwa lini na bunge liwa zirejeshwe halmashauri? Asikurupuke wakati serikali imeingia gharama kununua mifumo hiyo.
Aaah hakuna cha bunge wala sheria wao ni mwendo wa matamko tuu..
 
Mkuu izi Kodi halmashauri wanakusanya tu baada hapo zinapelekwa TRA kwa kutumia control number Kama ilivyo kwenye vitambulisho vya majasirimali mdogo
Sijui kama utanielewa.. TRA tayari wana mfumo kwenye kodi za majengo. Mfumo ambao hata ukikwa Kagera na nyumba yako iko kigamboni unaweza lipia tu kodi yako. Mfumo ule haukushuka tu kutoka mbinguni ni serikali imeingia gharama kubwa kuununua na mwishoni mwa mwaka jana umefanyiwa maboresho makubwa. Afu mtu na kadegree kake kakuungaunga anaamua tu leo kodi hii ihamishiwe LGA tena. Lkn mbaya zaidi hizi kodi huwa zinapitishwa BUNGENI ambako zinaongozwa na Act mbalimbali kama Finance Act, TAA nk. Lazima tutumie weledi wetu katika kuamua mambo kama taifa. Watanzania sasa tuweke vigezo muhimu vya kuongoza hizi wizara ikiwa ni pamoja na uzoefu wa kutosha kazini, elimu nzuri sambamba na kukubali kutumia wataalam husika. Ameongea kuwa kuna makundi matatu ya wafanyabiashara kwamba kuna wale wa vitambulisho, wale wapatao leseni kutoka halmashauri na wale wafanyabiashara wakubwa wanaotambulika na TRA. Ni kichekesho kikubwa sana kuwa waziri huyu hajui ABC ya mambo ya kodi na hadi leo hajui kuwa MFANYABIASHARA AMBAYE ANAPATA LESENI YA BIASHARA KUTOKA HALMASHAURI ANATAKIWA KWANZA KUKADIRIWA KODI TRA ndipo apate Tax clearance kisha apeleke huko halmashauri kupata hiyo leseni. Hii nchi kama una akili timamu huwezi kuishi.
 
Back
Top Bottom