Waziri Jafo apiga marufuku Wakala wa Majengo Tanzania kupewa kazi Halmashauri ya Buchosha

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
3,393
2,000
Wakala wa Majengo Tanzania ( TBA) wametakiwa kurejesha Shilingi million 300 walizolipwa kwa ajili ya ujenzi wa majengo ya Serikali katika Halmashauri ya Buchosa mkoani Mwanza, huku Halmashauri hiyo ikipigwa marufuku kuwapa kazi TBA.

Akizungumza wakati wa ziara yake wilayani humo juzi, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, (TAMISEMI), Seleman Jafo alimtaka Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo kuwaandikia barua ya kuwataka warejeshe fedha hizo ili zitumike kwenye majukumu mengine.

" Nilitamani ujenzi huu uwe umeisha lakini siyo sababu yenu ni sababu ya mtu mliyempa kazi msiwape tena kazi za huku ndani unapowalipa wanaenda kufanya kazi sehemu nyingine maeneo ya mjini wanafanya kazi sana ili kusifiwa na viongozi lakini huku ndani hawafanyi vizuri kabisa Mkurugenzi waandikie barua tena zile fedha zirudi zifanye mambo mengine" alieleza Jafo.

Akizungumzia suala la ukusanyaji wa mapato katika halmashauri hiyo alisema hawafanyi vizuri hivyo waongeze juhudi katika kukusanya kwani mpaka sasa wanaokusanya kwa asilimia 29, ukusanyaji wa mapato ndio kipimo cha Wakurugenzi kwa watakaoshindwa hawatakuwa na sifa.

" Ofisa mipango ,idara ya fedha imani yangu mtafanya vizuri katika hili na ofisi ya Mkurugenzi ninachowaomba mdumishe mahusiano pia wakuu wa idara fanyeni kazi vizuri na watu wa chini na mfanye kwa mahusiano mazuri na mpendane ili mfanye kazi na kuacha maigizo nataka watu wafanyakazi kwa amani msiwaonee watu" alisema Jafo.

Pia Waziri alisifia ujenzi wa hospital na jengo la Halmashauri nakusema kuwa wanafanya vizuri na kuwa halmashauri inayokuja kwa kasi na kuzitaka halmashauri zote nchini kuiga mfano wake.

Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo hilo Erick Shigongo alisema matatizo yanayomkosesha usingizi ni ubovu wa barabara, huduma za afya na miundombinu ya madarasa hivyo aliiomba Waziri Jafo kuliangalia hilo

" Nafarijika umetusifia uliposema mmejitahidi roho yangu imefarijika, shida kubwa ni barabara siku ikiondolewa tutalala simu nyingi nazozipokea kwa wananchi wangu ni hiyo ombi langu kwa watumishi tuchape kazi kwa nguvu ili kuonyesha Buchosa tunania ya kuleta maendeleo na kuipeleka Buchosa mbele" alieleza Shigongo.
 

chikutentema

JF-Expert Member
Dec 10, 2012
7,297
2,000
Wanaionea tu hii taasisi.

Wameipa kazi ambazo sio zake na wala hawakujiandaa nazo. Construction sio kazi ya mchezo, wamefanya lini hizo kazi? Wana uwezo wa kuzifanya? Wamepewa uwezo wa kuzifanya?
Wanachofanya ni kupewa hela mradi A wanahamishia mradi B, na huko mradi B wanafanya chini ya certificate wanayokuwa wamelipwa na kisha wanahamishia mradi C.

Narudia tena, TBA ni janga
 

MtamaMchungu

JF-Expert Member
Apr 10, 2011
5,670
2,000
Wanachofanya ni kupewa hela mradi A wanahamishia mradi B, na huko mradi B wanafanya chini ya certificate wanayokuwa wamelipwa na kisha wanahamishia mradi C.

Narudia tena, TBA ni janga
Kwani kazi walizopewa ni nini? Hela wanapewa za kutosha kufanya miradi?

Hii TBA kabla ya Magufuli nadhani ni Watanzania wachache sana walikuwa wanaijua, nini kimebadilika?

Tuwe critical kidogo
 

chikutentema

JF-Expert Member
Dec 10, 2012
7,297
2,000
Kwani kazi walizopewa ni nini? Hela wanapewa za kutosha kufanya miradi?

Hii TBA kabla ya Magufuli nadhani ni Watanzania wachache sana walikuwa wanaijua, nini kimebadilika?

Tuwe critical kidogo
Critical for what sense?! Unaipimaje TBA kwamba haikuwa na uwezo wa kufanya kazi hivyo isilaumiwe?

Unaelewa maana ya TBA na objective ya kuanzishwa kwake na kazi zake?

Una
 

Nsema

Senior Member
Feb 24, 2016
199
500
Serikali ya Tanzania inanichosha sehemu mmoja tu. Inataka kutoa Akira ml.8 halafu makampuni binafsi hayapewi tender. Tenda wanapewa TBA,SUMA jkt na mawakala mengine ya SERIKALI.

Badala ktoa kipaumbele kwa Kampuni binafsi ili zisaidie kutoa ajira na kulipa Kodi Serikalini.
Kampuni za ujenzi hazipati Miradi at the same time zilipe Kodi.
Kwa Hali hii wasomi watasugua Sana benchi kwani hata sekta binafsi nako hamna kitu.
 

Marytina

JF-Expert Member
Jan 20, 2011
7,177
2,000
Mfano ukichukua walinzi wa Suma jkt wakafanya uzembe mfano kutokuingia kazini na ukaibiwa Nani atalipa hiyo hasara? Serikali kweli itakulipa ?
 

MtamaMchungu

JF-Expert Member
Apr 10, 2011
5,670
2,000
Critical for what sense?! Unaipimaje TBA kwamba haikuwa na uwezo wa kufanya kazi hivyo isilaumiwe?

Unaelewa maana ya TBA na objective ya kuanzishwa kwake na kazi zake?

Una
Objectives za kuanzishwa zipo kwenye makaratasi, haziwi achieved by wishful thinking. TBA ili iweze kufanya hizo kazi wanahitaji utaalamu na mtaji, hivyo vitu wanavyo?

Ni kuwaonea tu. Ni kama walivyoamua kupeleka magari yao yote TEMESA. Baada ya muda mfupi TEMESA wakazidiwa, serikali ikarudi tena Toyota. Taasisi zinajengwa tena sio kwa uwekezaji sio ukali.
 

KUTATABHETAKULE

JF-Expert Member
Apr 2, 2012
2,673
2,000
Nilianza kuisikia TBA wakati wa mauzo ya zilizokuwa nyumba za Serikali. Utaratibu uliotumika ni uhamishaji wa miliki ya nyumba hizo toka HAZINA na kuzipeleka kuwa chini ya TBA ambao waliziuza nyumba hizo kwa watumiaji waliokuwa wakiishi humo. Hivyo moja ya kazi za mwanzo kabisa za TBA ni hiyo. Pia walipewa jukumu la kujenga nyumba mpya kwa wafanyakazi wa Serikali kama inavyonekana kwa mradi wa nyumba 300 pale Dodoma. Katika kujenga siyo kwamba wao ndio waifanye kazi hiyo, bali kwa kutumia wakandarasi. Kwa bahati mbaya sana mambo yanakwenda yanabadilika na wakajikuta na wao wanafanya kazi ya kujenga majengo badala ya kuwa wasimamizi wa miradi ya majengo hayo. Haposa, kama wasemavyo ndugu zetu wa Kenya, ndiyo matatizo yakaanza. Miradi haiishi, pesa zinaisha na matokeo yake ni majengo ambayo hayakidhi vigezo vinavyotakiwa. Mifano ipo mingi kuhusu ufanisi mbovu wa hawa jamaa, na huo huko Buchosa ni tone dogo tu la madudu hayo. Je wataendelea kuvumiliwa hadi lini?
Kwani kazi walizopewa ni nini? Hela wanapewa za kutosha kufanya miradi?

Hii TBA kabla ya Magufuli nadhani ni Watanzania wachache sana walikuwa wanaijua, nini kimebadilika?

Tuwe critical kidogo
 

MtamaMchungu

JF-Expert Member
Apr 10, 2011
5,670
2,000
wa bahati mbaya sana mambo yanakwenda yanabadilika na wakajikuta na wao wanafanya kazi ya kujenga majengo badala ya kuwa wasimamizi wa miradi ya majengo hayo
That is my point... wamepewa kazi ambayo basically hawana uzoefu au uwezo nayo. Wataendelea kulaumiwa tu, lakini Serikali kuu na wanasiasa ndio tatizo kubwa, hawataki kuonekana wabaya, ionekane shida ni wengine
 

Bombabomba

JF-Expert Member
Dec 23, 2017
1,228
2,000
Kwa kuwa ni watumishi wa Serikali wahamishiwe tu Halmashauri kuongeza wataalam wa Ujenzi kwenye force account
 

Valuhwanoswela

JF-Expert Member
Jun 27, 2019
1,073
2,000
TBA ni janga la taifa hili
Hao ndo walijenga zile Hostel mashughuri za Magufuli pale UDsm ambazo nyufa zilizojitokeza paka aliweza kupita mpaka yule mwanafunzi aliyepiga picha nyufa alitupwa lupango labda hadi leo. Taasisi nyingi za Serikali ni kwa ajili ya ajira za wateule!
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom