Waziri Jafo amuondoa kwenye nafasi yake Meneja wa TARURA jijini Arusha kwa kushindwa kuita Wananchi kushuhudia ufunguzi wa barabara

Duh, kazi hizi ngumu sana, ingefaa huyu mtendaji wa TARURA afanye mawasiliano ya kutosha nini na nini atahitaji waziri kabla ya kufika site. Nadhani hakukuwa na mawasiliano mazuri kabla
Haijalishi kuwepo au kuto kuwepo kwa mawasiliano mazuri, swali la msingi ni JE, NI JUKUMU LA MHANDISI KUITA WATU WAJE KWENYE UZINDUZI WA BARABARA? Je hili sio jukumu la DC, DAS, wenyeviti wa vijiji, watendaji kata et al?
 
Nyie manyumbu naona humu mnapayuka tu...hapo jukumu la huyo meneja na mkurugenzi ilikuwa ni washirikiane watangaze ratiba ya ujio wa waziri...hayo ya kujaza uwanja mngewaachia wananchi wenyewe kwani siku hizi wanajua wenyewe nini cha kufanya muda ukitaradadi.

Mkurugenzi au meneja katuhujumu.
 
Kwani hao wananchi hawaoni jamani hizo barabara? Sasa barabara utaifichaje? Halafu meneja kazi yake ni kuhakikisha kazi imefanyika kwa kiwango. Siyo kukusanya wananchi. Hii serikali ya sifa, hii...! Ngoja nikazane na biashara zangu tu.
Hiyo barabara nasubiri giza liingie nikaiibe naipeleka namtumbo halafu nasema ACT ndio wametengeneza, nahisi jafo anaogopa uwizi wangu maana ni wa kiwango cha lami
 
Nyie manyumbu naona humu mnapayuka tu...hapo jukumu la huyo meneja na mkurugenzi ilikuwa ni washirikiane watangaze ratiba ya ujio wa waziri...hayo ya kujaza uwanja mngewaachia wananchi wenyewe kwani siku hizi wanajua wenyewe nini cha kufanya muda ukitaradadi.

Mkurugenzi au meneja katuhujumu.
Namini nakuja kuwahujumu kwa kuiiba hiyo road.
 
Watu wengi tulimheshimu Jafo lakini kwa hili la jana, mh amejipaka matope yanayonuka.
Kuna harufu ya visasi kwenye maamuzi yake hayo.
Mungu amhurumie Jafo
Nashangaaga wanaomsifia Jafo yani katika mawaziri vimeo jamaa yupooo...!! Ana misifaa sanaa. Alafu huyu engineer hakutakiwa hata Kuomba msamahaaa maana hana kosaaa.. Kuita watu waje kwenye mkutano huo ni jukumu la wateuliwa wa kisiasaa...wakurugenzi na wengineoo sio msomi kama huyu aanze kufanya upuuzi huo.
 
Kosa la injinia ni kutokuita watu waone uzinduzi live,yaani barabara imezinduliwa kimyakimya bila live,na Mr jo amekosa haki yake ya kusifiwa.
 
uipeleke wapi...tunakuloga ukojoe mkojo wa kijani mpaka uiludishe hiyo road yetu.
Naiiba kabla wanachi hawajajua kama imejengwa na serikali maana kwa mujibu wa jafo anajua wananchi wanafahamu hiyo road imejengwa na chama cha hashim rungwe
 
Waziri wa TAMISEMI, Selemani Jafo amemuondoa kwenye nafasi yake Meneja wa TARURA Jijini Arusha, Podia Mwankenja kwa kushindwa kukusanya Wananchi kushuhudia barabara zilizokamilika alizokuwa akizitembelea.

Waziri Jafo amesema, “Mnataka Serikali ionekane haijafanya kitu wakati Wananchi ndio barabara yao? Kama ni barabara ya Wananchi mbona Wananchi hawapo hapa? Au unataka Serikali ionekane haijafanya kitu katika maeneo yao?”

Waziri Jafo amemuhoji Meneja huyo ambaye pia ndio Mratibu wa barabara za Jijini humo “Kwanini hii tunazindua barabara hii Wananchi hawapo? Unataka Rais aonekane hajafanya kitu? Rais ameweka fedha hapa. Mmeficha halafu kesho na kesho kutwa mseme Rais hajafanya kitu?”

Aidha, Meneja huyo alipoanza kujitetea na kusema kuwa alidhani Mtendaji (Mkurugenzi) amefanyia kazi suala hilo, Waziri Jafo alimwambia “Wewe si barabara zako? Unafanya sabotage ili Rais aonekane hajafanya kitu halafu kesho Wananchi waseme hakuna lolote Rais amefanya?”

Waziri Jafo amemalizia “Ninyi ndio wataalamu mnaofanga Serikali ionekane haijafanya jambo wakati sisi hapa Arusha tumewekeza fedha nyingi. Mji wa Arusha tumetandaza Barabara ila wewe unaficha hata Wananchi hapa jirani wasijue tumeweka barabara”

Kigoma ina nini jamani? Buhigwe, Kakonko dah, kumbe hata kwenye ndoto ya kuendelezwa hatumo? Machikini weee
 
Katika hili waziri Jafo amechemsha. Hizi ni kazi za mihemko. Mbona hakumwajibisha Mkurugenzi na mkuu wa wilaya?
Engineer wa barabara anaanzia wapi kukusanya watu wakati ni kazi za watendaji.
Labda Jafo Alitalia Engineer amkusanyie vibarua wake.
Katika hili waziri umechemsha, nyie ndo type za kina Gambo na kina Makonda mnaotaka muonekane kwenye midia.
Sabotage ingeonekana kama anafanya kazi chini ya viwango. Acheni kumdhalilisha aliye wachagua maana hapo umekuwa busara na hekima katika kufanya uliyoyafanya. Mtu mwenye matatizo ya akili na uelewa atakaye kusifia kwa ulichokifanya ila kumbuka" lila Mpanda ngazi hushuka".

Back
Top Bottom