Waziri Jafo amuondoa kwenye nafasi yake Meneja wa TARURA jijini Arusha kwa kushindwa kuita Wananchi kushuhudia ufunguzi wa barabara

Influenza

JF-Expert Member
Jul 1, 2018
1,445
3,402

Waziri wa TAMISEMI, Selemani Jafo amemuondoa kwenye nafasi yake Meneja wa TARURA Jijini Arusha, Podia Mwankenja kwa kushindwa kukusanya Wananchi kushuhudia barabara zilizokamilika alizokuwa akizitembelea.

Waziri Jafo amesema, “Mnataka Serikali ionekane haijafanya kitu wakati Wananchi ndio barabara yao? Kama ni barabara ya Wananchi mbona Wananchi hawapo hapa? Au unataka Serikali ionekane haijafanya kitu katika maeneo yao?”

Waziri Jafo amemuhoji Meneja huyo ambaye pia ndio Mratibu wa barabara za Jijini humo “Kwanini hii tunazindua barabara hii Wananchi hawapo? Unataka Rais aonekane hajafanya kitu? Rais ameweka fedha hapa. Mmeficha halafu kesho na kesho kutwa mseme Rais hajafanya kitu?”

Aidha, Meneja huyo alipoanza kujitetea na kusema kuwa alidhani Mtendaji (Mkurugenzi) amefanyia kazi suala hilo, Waziri Jafo alimwambia “Wewe si barabara zako? Unafanya sabotage ili Rais aonekane hajafanya kitu halafu kesho Wananchi waseme hakuna lolote Rais amefanya?”

Waziri Jafo amemalizia “Ninyi ndio wataalamu mnaofanga Serikali ionekane haijafanya jambo wakati sisi hapa Arusha tumewekeza fedha nyingi. Mji wa Arusha tumetandaza Barabara ila wewe unaficha hata Wananchi hapa jirani wasijue tumeweka barabara”

photo_2020-07-09_16-05-21.jpg
 
Mimi nadhani ni Sawa tu,

Maana yake halisi ni Sawa na Baba kujenga nyumba ya pili Halafu asiimbie familia yake kuwa amejenga nyumba nyingine mahali, Halafu akaweka wapangaji wasijue hata familia yake
 
Back
Top Bottom