Waziri Jafo akerwa na uchafu soko la Sabasaba Jijini Dodoma

KAGAMEE

JF-Expert Member
Dec 20, 2013
3,869
4,495
Habari wakuu!Kuna taarifa jana nmeisoma kwenye social media inaeleza kwamba Mheshimiwa Jafo kaagiza soko la sabasaba jijini Dodoma libomolewe na kujengwa upya Mara moja.Hii taarifa ina ukweli wowote?

=====

JAFO akerwa na uchafu soko la Sabasaba Jijini Dodoma
thumb_2313_800x420_0_0_auto.jpeg
January 25th, 2020
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jafo amekerwa na hali ya uchafu katika Soko la Sabasaba Jijini Dodoma, amuagiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma kuhakikisha wanafanyia ukarabati soko hilo katika mwaka wa Fedha 2020/2021

Mhe Jafo amekerwa na hali hiyo alipotembelea Soko la sabasaba lililoko katika Halmashauri ya Jiji la Dodoma na kukuta hali ya uchafu uliokithiri katika eneo hilo huku mifereji ya maji ya mvua ikiwa imejaa uchafu jambo ambalo linahatarisha afya za wafanyabishara wa eneo hilo.

“Jiji la Dodoma halina mashaka katika ukusanyaji wa mapato, na najua mnafanya mambo makubwa na mazuri lakini kwa hili hapana sijaridhishwa kabisa na hali ya soko, hili ni jambo pana la wananchi ni vyema likafanyiwa kazi kwa haraka” amesema Mhe. Jafo

Ameendelea kusema kuwa wafanyabishara hawa ni wapiga kura wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. John Pombe Magufuli, hivyo wanatakiwa kufanya biashara katika mazingira mazuri na si katika mazingira haya, wanatakiwa wafanye bishara katika mazingira masafi na mazuri.
jafo.jpg

Mhe. Jafo anafafanua kuwa Jiji la Dodoma linaongoza kwa ukusanyaji wa mapato ambapo limeweza kukusanya zaidi ya shilingi bilioni 70 kwa mwaka, inasikitisha kuona wanashindwa kukarabati soko hilo, hivyo amemuagiza Mkurugenzi wa Jiji hilo kuhakikisha soko linajengwa.

“Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma sijafurahishwa na hali ya uchafu unaoendelea katika soko hili, uchafu huu unahatarisha afya za wafanyabishara na wananchi kwa ujumla, nakuagiza kuhakikisha Soko hili linafanyiwa ukarabati” Amesisitiza Mhe Jafo

Aidha, Mhe. Jafo ameutaka uongozi wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma kuhakikisha wanasimamia usafi na kuhakikisha mitaro inasafishwa ili kulinda afya na usalama wa wafanyabishara na wananchi kwa ujumla.
 
Back
Top Bottom