Waziri Jafo abadili gia angani, afuta maamuzi yote ya wasimamizi wa uchaguzi kuwaengua wagombea. Wagombea wote ruksa kushiriki uchaguzi

idawa

JF-Expert Member
Jan 20, 2012
25,284
38,305
Waziri wa Nchi ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe. Selemani Jafo ametangaza kuwaruhusu wagombea wote waliochukuwa fomu na kuzirejesha kwa ajili ya kugombea nafasi mbalimbali katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaotarajiwa kufanyika nchini Tanzania Novemba 24, 2019 wanaruhusiwa kushiriki uchaguzi huo na amefuta maamuzi yote yaliyofanywa na wasimamizi wa uchaguzi Nchini kote ya kuwaengua wagombea wa vyama mbalimbali. Waziri Jafo ametoa uamuzi huu jijini Dodoma alipokuwa akizungumza na wanahabari leo.

Chanzo: Ukurasa wa OR-Tamisemi Facebook


Hata hivyo Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa nchini Tanzania (Tamisemi), Selemani Jafo ametangaza wenyeviti wa vijiji 6,248, wa mitaa 1169 na vitongoji 37,505 wanaotokana na CCM wamepita bila kupingwa baada ya kutojitokeza kwa wagombea kutoka vyama vya upinzani.


“Kwa upande wa vitongoji Chama cha Mapinduzi kimepita bila kupingwa katika vitongoji 37,505 kati ya vitongoji 64,384 sawa na asilimia 58,”

Amesema katika wajumbe wa kundi la wanawake jumla ya wajumbe 64,085 wamepita bila kupingwa na wajumbe kundi la mchanganyiko jumla ya wajumbe 75,560 wamepita bila kupingwa.


2210108_IMG-20191111-WA0006.jpg



-----


Jafo awaruhusu wagombea wote nchini waliochukua fomu na kuzirejesha kushiriki uchaguzi wa Serikali za Mitaa.
1573459642722.png

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jafo wagombea wote waliochukua na kurejesha fomu za kuwania nafasi mbalimbali za uongozi katika uchaguzi wa serikali za mitaa bila kujali kama walienguliwa isipokuwa kwa wale wasio raia wa Tanzania, hawakujiandikisha au wamejiandikisha mara mbili.

Ameyasema hayo leo wakati akiongea na waandishi wa Habari ofisini kwake Jijini Dodoma kuhusiana na mapingamizi na rufaa mbalimbali zilizotolewa wakati wa urejeshaji wa fomu katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa.

Mhe. Jafo amesema kuwa hatua hiyo imetokana na kanuni za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa ambapo Waziri mwenye dhamana ya uchaguzi ana nafasi ya kutoa mwongozo wa jambo lolote kuhusu uchaguzi huo.

“ Kwa mujibu wa kanuni za uchaguzi wa Serikali za Mitaa mwaka 2019 Tangazo la Serikali Na. 371, Kanuni ya 49, Tangazao Na. 372 la mwaka 2019 Kanuni ya 51, Tangaza la Serikali Na. 373 la mwaka 2019 la mwaka 2019 Kanuni ya 52 na Tangazo la Serikali Na. 374 la mwaka 2019 kanuni ya 52 ninaotoa mwongozo kwamba wagombea wote ambao waliteuliwa na kudhaminiwa na vyama vyao na kufanikiwa kurejesha fomu zao za uteuzi kwa wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi katika kipindi kilichokuwa kimepangwa cha kuchukua na kurejesha fomu wanapewa sifa ya kupigiwa kura na wananchi.”

Amezitaja sababu ambazo hazitamruhusu mtu kugombea nafasi ya uongozi kuwa ni wale ambao watabainika kuwa wamejidhamini wenyewe, kutodhaminiwa na chama chake cha siasa, wagombea wawili wa chama kimoja kurejesha fomu katika nafasi moja na kama atakuwa amejitoa kwa mujibu wa Kanuni za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa

“Nadhani ni habari njema kwa wale waliokuwa na madukuduku, mapingamizi sasa mambo yote yale tumeyaondoa ili mradi wamerejesha fomu zao lakini hawana pingamizi za uraia na mambo mengine niliyoyaeleza basi naelekeza wasimamizi na wasimamizi wasaidizi wawajumuishe kwa kuwa wamepewa sifa” amesema Mhe, Jafo.

Mhe. Jafo amesema hakuna kuweka mpira kwapani, hakuna kukimbia hapa mpaka kieleweke, kama mtu alirejesha fomu na hana makandokando niliyoyabainisha wote wamepewa sifa na watajumuisha kwenye wangombea wa uchaguzi.

Kuhusu Vyama vilivyojitoa Mhe. Jafo amesema kwa mujibu wa kanuni za uchaguzi zinatambua kujitoa kwa mgombea na si Chama kujitoa hivyo mpaka sasa wagombea ambao walijaza fomu na kuzirejesha zikiwa zimedhaminiwa na vyama vya siasa wagombea hao wanatambulika kushiriki uchaguzi huo.

“Kama kuna chama kinataka kutoshiriki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa havikatazwi kuendelea kugoma kwani huwenda hiyo ndiyo aina ya demokrasia yao.”amefafanua Mhe. Jafo

Ameendelea kusema kuwa utaratibu wa uchukuaji na urejeshaji fomu, jumla ya wananchi 555,036 kutoka vyama vyenye usajili wa kudumu walifanikiwa kuchukua fomu za kugombea na kati ya hao wananchi 539,993 sawa na wasilimia 97.3 walifanikiwa kurejesha fomu zao.

Mhe. Jafo amesema wananchi walichukua fomu kutoka Chama cha Mapinduzi walikuwa ni 412,872 ikiwa ni asilimia 74 ya watu wote waliochukua fomu wakati Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) walikuwa ni 105,937 ambayo ni sawa na asilimia 19.

Amesema Chama cha Wananchi (CUF) walikuwa ni 24,592 ambao ni sawa na asilimia 4, ACT- Wazalendo walikuwa ni 8,526 ambao ni sawa na aslimia 1.5, NCCR-Mageuzi walikuwa ni 2,244 ambao ni asilimi 0.4 huku vyama vingine vyenye usajili wa kudumu walikuwa chini ya asilimi 0.1 kwa kila chama.

Hata hivyo Mhe. Jafo amesema mapingamizi na rufaa mbalimbali zipatazo 15,380 ziliwasilishwa katika kamati za rufaa kote nchini na kuwa baada ya uamuzi kutolewa rufaa 4,921 ambazo ni sawa na asilimi 32 ya rufaa zote zilitishwa.
“Baada ya maamuzi ya kamati, asilimia 32 ya rufaa hizo zilipitishwa lakini asilimi 68 ya rufaa zilikosa sifa kwa sababu mbalimbali kulingana na kanuni za uchaguzi.”amesema Mhe. Jafo

Mhe Jafo amefafanua kuwa katika machakto wa kuchukua na kurudisha fomu CCM iliweza kupita bila kupingwa katika maeneo mbalimbali kwa kuwa hapakuwa na mgombea yeyote kutoka vyama vingine vya siasa.

“Hii inamaana katika nafasi zilizoombwa katika baadhi ya maeneo, aliyechukua fomu na kurudisha fomu ni mgombea kutoka Chama cha Mapinduzi pekee na hakukuwa na mgombea yeyote kutoka vyama vingine vya siasa,” amesema Mhe. Jafo.

Akifafanua zaidi, Mhe Jafo amesema kwa upande wa nafasi ya wenyeviti wa vijiji CCM imepitwa bila kupingwa katika vijiji 6,248 kati ya vijiji 12,319 vilivyopo nchini ambayo ni sawa na asilimia 51.

Ameendelea kusema kuwa kwa upande wa wenyeviti wa mitaa, CCM imepita bila kupingwa katika mitaa 1,169 kati ya mitaa 4,263 iliyopo nchini ambayo ni sawa na asilimi 27 na kwa upande wa vitongoji CCM imepita bila kupingwa kwenye vitongoji 37,505 kati ya vitongozji 64,384 sawa na asilimia 58.

Mhe Jafo amesema kwa upande wa wajumbe wa kundi la wanawake jumla ya wajumbe 64,085 wamepita bila kupingwa na wajumbe kundi la mchanganyiko jumla ya wajumbe 75,560 wamepita bila kupingwa.

Aidha, Mhe.Jafo amevitaka vyama vya siasa vinavyoshiriki uchaguzi huo kuhakikisha wanawasilisha ratiba za kampeni kwa wasimamizi wa uchaguzi
 
Siasa za ulaghai zimefika mwisho Wananchi hatudanganyiki tena

Mimi nilijua huu ni mchezo wa upinzani kuepuka aibu ya kushindwa

Wamenusa harufu ya uchapakazi wa Magufuli anavyokubalika kwa Wananchi wakaona njia ya kuepuka aibu ni kujitoa kwenye Uchaguzi

Ila kwa kuwa Serkali inamkono mrefu ikawa imenasa huo mtego

Wengine walikosea kujaza fomu makusudi ili wasipitishwe

Ningeomba serkali iwarudishe wote hata wale wasio jua kusoma na kuandika
 
Eti anasema kama jina lilikatwa alafu ukaenda kushtaki eti jibu likitoka kuwa umeshinda basi jina lako litakuwa kwenye form ya wagombea..
Sasa najiuliza mtu ameshakatwa alafu chama chake kishajivua alafu jina mkaliweke kwenye form ya wagombea ina maana huyo mgombea atakuwa binafsi au??
 
Sidhani kama ana hekima ya kuweza kutoa kauli yoyote ile ya kulisaidia Taifa. Hawa wamelaanika. Aliyelaanika hasikii wala hasikilizi.

Hawa siyo watu wa kubadilika ili waendane na matakwa ya umma bali wanataka umma utekeleze tu wanayoyataka wao hata kama ya upuuzi.
 
Namuona jafo hapa UTV wagombea wa chadema walikuwa 19% ya wabombea wote

CUF likuwa na wagombea 4% ya wagombea wote

VYAMA vilivyobakia walikuwa 1.005 ikiwemo na ACT

CCM ilikuwa na wahombea 79& ya wagombea wote

Form zilizokataliwa zilikuwa asilia 28.66% ya form zote


State agent
 
Sidhani kama ana hekima ya kuweza kutoa kauli yoyote ile ya kulisaidia Taifa. Hawa wamelaanika. Aliyelaanika hasikii wala hasikilizi.

Hawa siyo watu wa kubadilika ili waendane na matakwa ya umma bali wanataka umma utekeleze tu wanayoyataka wao hata kama ya upuuzi.
Aje atangaze ushindi wa kishindo kwa chama chetu pendwa Ccm maana jamaa wameweka mpira kwapani.. Yaani gharama zote hizi serikali inaingia kwa kutumia ubabe kuliko busara. Endeleeni maana nyie ndio wenye dola ila mjue siku hazigandi. Mtakuja kujibu huu uhujumu uchumi mnao ufanya kwa kubeba Ccm mbelekoni.. Kama mnaamini mmetekeleza vyema ilani yenu kinacho wafanya muogope uchaguzi ni kitu gani???
 
1/wagombea wa chadema na act bado wanarejesha form licha ya viogozi wake kusema wamejitoa na tumewapokea na tutawapa fursa ya kugombea

2/Tumewapa fursa ya rufaa na wengi wameshida na tumewapa ridhaa ya kugombea

3/hakuna kuweka mpira kwapani,hakuna kuruka ukuta lazima wagombee

4/walichukua form na kulejesha wote watashiriki hiyo tarehe 24/10

State agent
 
11 Reactions
Reply
Back
Top Bottom