Waziri Jafo aamuru hadharani mwanamke aongezewe mshahara, awashangaa kwa kumlipa mrembo Tsh. 240,000

Azarel

JF-Expert Member
Aug 25, 2016
26,099
34,045
Habarini Wadau.

Waziri wa TAMISEMI amemwagiza Mkurugenzi wa Dodoma, Godwin Kunambi kumuongezea mshahara Mwanamke mmoja dereva wa Gari la Taka kutokana na Uzuri na Urembo wake huku akimsifia urembo wake.

Ninachojiuliza ni kuwa, hivi hawa huwa si wanalipwa kulingana na scale za serikali?

Na je utaratibu wa kumpandisha Mtumishi mshahara upo kienyeji hivyo?

Mshahara si ni siri ya Mtumishi?





Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huyo atakuwa mtumishi wa ajira ya Mkataba/Kibarua kwa kiwango hicho cha mshahara, hivyo endapo Waziri mwenye dhamana ametoa pendekezo kwa Mkurugenzi wa Jiji bidada atapata baada ya CMT kuidhinisha ombi la Mkurugenzi.
Point ya Jaffo siyo urembo, bali ni mshangao jinsi Wadada walivyo wabaguzi wa kazi yule yeye ameonyesha kutojali na akaenda kujichanganya Chuo cha Mitambo na sasa yuko Dampo anasukuma Dumper, Folk nk hivyo anapewa hiyo nyongeza ili iwe motisha kwake na salamu kwa WANAWAKE WENGINE WOOOOTE watambue kazi yoyote halali hakuna ya Mwanaume wala mwanamke zote ni Kazi tu.
 
Mi nadhani hakuamuru nyongeza ya mshara kwa huyo dada kutokaba na "urembo" wake. Mzee Sele anaonekana kuwa amestaajabishwa kuona mwanamke akifanya kazi ambayo ni "purely" za wanaume kutokana na ugumu wake.

Kwa hiyo alichofanya ni kutoa changamoto kwa wanawake wengine kama yeye wanaotumia urembo wao kuendesha maisha kwa "kudanga". Cha kuzingatiwa katika kauli ya Mzee Sele ni pale aliposema "kuna wanaume wanashindwa kuendesha mitambo ya manual hata taxi lakini dada huyu anasukuma mtambo mkubwa unaofanya kazi kwa ajili ya umma".

Labda tunachoweza kumlaumu Jaffo ni kuwa "specific" kwa mwanamke huyu wakati kuna akina dada wengi wanafanya kazi kama hizo au zaidi. Wapo wanawake wanaendesha "heavy articulated trucks" na mabasi ya abiria yanayosafiri umbali mrefu (nje ya nchi) ambao wanastaili "promotion" kama hii.
 
Sure. Taaluma za watu ziheshimiwe. Hiyo hela ni ndogo sana kwa kazi anayofanya na mazingira anayofanyia kazi (dampo).
Mshahara upo kwa mujibu wa Sheria na makubaliano ya pande mbili, bidada kaukubali mshahara yuko happy, wewe na House girl wako nani anafanyakazi nyingi na ngumu kwa mwezi. Je, mshahara wako na ule wa House Girl/Boy vinalingana??? Kitu kinalipwa per SKILLS mkuu siyo kwa kuangalia Uvundo, mafunza au uzito.
 
Back
Top Bottom