seedfarm
JF-Expert Member
- Feb 9, 2020
- 260
- 2,654
Members,
Siri aliyoitoa Selemani Jafo huko Arusha inafikirisha sana na kutoa picha halisi ya Chama cha Mapinduzi.
Mosi, kumbe watu wanakusanywa na kulazimishwa wajitokeze waonekane wengi wakati wa uzinduzi wa miradi na kampeni za CCM.
Hili jambo la kukusanya watu wasiojielewa kama mifugo ili waje kupiga makofi uzinduzi wa barabara ya lami halina afya hata kidogo kwa mustakabali wa taifa.
Leo hii watu wengi wanafahamu ni kazi ya serikali kuweka lami na kujenga miundombinu, hili sio ombi ni lazima kwa kuwa wanatuumiza kwenye kodi.
Jambo baya zaidi unalazimisha watumishi wenye taaluma zao wakakusanye watu ili waje kukushangilia wewe na barabara ya lami
Pili, watendaji wenye taaluma zao mfano engineers, waganga wakuu wa hospital za wilaya na afya na wengine wanalazimishwa kujiingiza kwenye siasa kwa nguvu ili kusifu na kupiga makofi. Nini kosa la yule mtendaji wa serikali?
Je, yule mtendaji anayelazimishwa kukusanya watu Arusha na Selemani Jafo alipewa pesa za mafuta na vipaza sauti ili ashawishi wananchi kuja kushangilia barabara ya lami.
Kwa hili Jafo kubali umekosea na omba msamaha watu watakusamehe, kubali umeteleza.
Yule mtumishi anayesimamia barabara Arusha hukutaka kumsikiliza uliona hoja zake zina mashiko. Ulikuwa na hasira na frustration zako na mihemko isiyokuwa na maana kama Waziri.
Selemani Jafo ukiwa na hasira jaribu kunywa maji mengi na kutulia kwanza. Ulevi wa madaraka ulioonyesha kwa mtumishi Arusha mwenye taaluma yake kumlazimisha akaswage watu kama mifugo halikubariki kabisa.
Propaganda fanyeni nyie wanasiasa. CCM Arusha ilikuwa wapi kukusanya hao watu waje kukushangilia wewe na barabara ya lami.
Je, Arusha hakuna katibu wa chama cha mapinduzi au Mwenyekiti wa CCM Arusha.
Umetumia madaraka yako vibaya sana. Watu walikuamini lakini sasa wanapata picha yako halisi kuwa wewe ni katili, mpenda sifa na usiyetaka kusikiliza hoja za watumishi wa umma.
Yule mtumishi aliyesimamia barabara Arusha kama engineer ulipasa kumsifu na kumpa hongera yake. Kitendo cha kumlazimisha engineer akatafute watu waje kukupigia makofi wewe na barabara ya lami ni aibu kubwa. Hata bosi wako hawezi kukubaliana na ulichokifanya Arusha kumuondoa mtumishi wa uma kisa hajatafuta watu wa kukupigia makofi wewe na kupigia makofi barabara ya lami.