Waziri Jaffo: Mwezi April 2020 nitamkabidhi Rais Magufuli orodha ya Wakurugenzi wavivu

Waziri wa nchi Tamisemi, Seleman Jafo amesema ana majina ya wakurugenzi wasiokwenda na kasi ya utendaji kazi wa Serikali ya Tanzania, atayakabidhi kwa Rais John Magufuli Aprili, 2020.

Jafo ameeleza hayo leo Jumatano Januari 22, 2020 mjini Dodoma wakati akikabidhi mashine 7227 za kukusanyia mapato kwa halmashauri zote. Mashine hizo imetolewa na balozi wa Norway nchini Tanzania, Elisabeth Jacobsen.

Waziri huyo amesema ameshindwa kuzivumilia baadhi ya halmashauri kwa kuwa zinatekeleza majukumu yake kinyume na miongozo ya Serikali, ikiwa ni pamoja na kutokusanya fedha ipasavyo.

"Wiki ijayo nitatoa taarifa ya makusanyo yote kwa halmashauri, lakini taarifa yangu ya mwezi Aprili nitaorodhesha majina na kumkabidhi mwenye mamlaka, nitatoa mapendekezo ikibidi wakurugenzi waachiwe maana hawatufai," amesema Jafo.

Amebainisha kuwa kuna halmashauri zinadaiwa madeni makubwa, zikiwemo posho za madiwani, “kuna halmashauri inadaiwa Sh758 bilioni ambazo ni malimbikizo ya posho za wabunge, mkurugenzi wake anapaswa kujitathimi.”

Sent using Jamii Forums mobile app
Hahahaha..Waziri kakasirika simply because posho za wabunge hazijalipwa!!??... nilidhani kaguswa na madeni ya local suppliers including contractors.. anyways, yote kheri.
 
Hahaha dona kantri trunashindwa kununua mashine......
Serikaly za Mitaa ni shida sana. Fikiria Mkuu wa Mkoa, Wilaya, Mkurugenzi, Maafisa Elimu na Walimu Wakuu wana taarifa ya watoto wanaotegemewa kumaliza darasa la saba (Elimu ya Msingi) na kuingia Kidato cha Kwanza( Elimu ya Sekondari) lakini hadi mwaka wa masomo unafika shule hazina madawati, mashimo ya vyoo wala vyumba vya madarasa! Inasikitisha sana. Hivi ni nini kinawazuia kuweka utaratibu wa kujenga miundombinu hiyo kwa wakati wkati wakijua na idadi ya wanafunzi watakojiunga na elimu ya sekondari hata kwa makisio (estimates)? Alafu Kiongozi ngazi ya Mkoa anafikia hatua hata ya kuweka ndani walimu kwa wanafunzi kushindwa kufaulu. Kweli kwa mtindo huu elimu itakuwa yenye kiwango?!
 
Waziri wa nchi Tamisemi, Seleman Jafo amesema ana majina ya wakurugenzi wasiokwenda na kasi ya utendaji kazi wa Serikali ya Tanzania, atayakabidhi kwa Rais John Magufuli Aprili, 2020.

Jafo ameeleza hayo leo Jumatano Januari 22, 2020 mjini Dodoma wakati akikabidhi mashine 7227 za kukusanyia mapato kwa halmashauri zote.

Mashine hizo imetolewa na balozi wa Norway nchini Tanzania, Elisabeth Jacobsen.

Waziri huyo amesema ameshindwa kuzivumilia baadhi ya halmashauri kwa kuwa zinatekeleza majukumu yake kinyume na miongozo ya Serikali, ikiwa ni pamoja na kutokusanya fedha ipasavyo.

"Wiki ijayo nitatoa taarifa ya makusanyo yote kwa halmashauri, lakini taarifa yangu ya mwezi Aprili nitaorodhesha majina na kumkabidhi mwenye mamlaka, nitatoa mapendekezo ikibidi wakurugenzi waachiwe maana hawatufai," amesema Jafo.

Amebainisha kuwa kuna halmashauri zinadaiwa madeni makubwa, zikiwemo posho za madiwani, “kuna halmashauri inadaiwa Sh758 bilioni ambazo ni malimbikizo ya posho za wabunge, mkurugenzi wake anapaswa kujitathimi.
Jaffo naye mvivu. Wakurugenzi ni saizi take na ana mamlaka ya kuwawajibisha. Kusubiri mpaka ampelekee Rais ni uzembe.
 
Katika orodha hiyo mkurugenzi wa Moshi manispaa Kule mkoani Kilimanjaro,akikosekana ,nitashangaa sana.
 
Back
Top Bottom