#COVID19 Waziri Jaffo aongoza Maombi ya waislamu kufukuza CORONA

jembejembe

JF-Expert Member
Jun 9, 2016
664
1,000
Waziri wa nchi ofisi ya Makamu wa rais muungano na mazingira, Suleiman Jaffo ameongoza maombi ya kumwombea rais Samia Suluhu pamoja na Taifa kuepuka ugonjwa hatari wa Corona na kuzitaka taasisi zingine za dini hapa nchini kusimamia amani ya nchi .

Akiongea wakati wa maombi hayo yaliyofanyika makao makuu ya taasisi ya dini ya kiislamu ya Twariqa mjini Moshi, Mkoani Kilimanjaro waziri Jaffo amesema ipo haja kwa taasisi zote za dini hapa nchini kuliombea taifa kuepuka mifarakano inayoweza kuhatarisha amani ya nchi.

Alisema uamuzi uliofanywa na taasisi ya Twariqa kuliombea taifa ni Jambo jema linalopaswa kuigw na taasisi zingine za dini chini ili kuepuka ugonjwa hatari wa Corona ambao umelikumba taifa na dunia kwa ujumla.

Akitolea mfano nguvu ya maombi ilivyokimbiza ugonjwa wa Corona hapa nchini ,pamoja na kimbunga hatari cha Jobo kilichotishia amani ya nchi ni kielelezo kwamba ipo haja kwa viongozi wa dini kuzidisha nguvu ya maombi ili taifa liendelee kubaki salama.

Awali katibu wa taasisi hiyo ya Twariqa Yahaya Mkindi alisema lengo la kuwakutanisha waislamu na waziri Jaffo katika makao makuu ya taasisi hiyo ni kuliombea Taifa kuepuka ugonjwa hatari wa korona sanjari na kumwombea rais Samia Suluhu Hasan aweze kuliongoza Taifa vema akiwa na hofu ya mungu Kama mwanamke wa kwanza Tanzania kuwa rais wa kike.

"Tumekutana hapa kwa ajili ya kuombea janga la gonjwa wa covd 19 likae mbali na Tanzania pamoja na kumwombea rais Samia Suluhu Kama mwanamke wa kwanza kuliongoza Taifa la Tanznaia"alisema

Aidha katika hatua nyingine katibu mkuu Mkindi alisema taasisi hiyo ipo katika hatua ya mchakato wa ujenzi wa kituo Cha afya Cha mama na Mtoto kitakachosaidia akina mama kujifungua na kuepusha Vifo visivyo vya lazima.

Kwa upande wake msemaji mkuu wa Twariqa sheikh Haruna Hussein aliwataka waislam kuendelea kuwa wamoja na kuepuka mifarakano isiyo na tija inayotokana na kugombea madaraka kwa waislamu wasiotaka mabadiliko kuendelea kung'ang'ania madarakani.

Alisema maombi hayo yaliyowakutanisha pia viongozi wa wakuu wilaya ya Moshi mjini na meya wa Juma Shaibu Hussein alisema Amani ni tunu ya nchi hivyo kila kiongozi anapaswa kudumisha Amani na kuielezwa Amani kwa jamii yote inayomzunguka.

Ends...

IMG_20210522_151101_626.jpg
 
ivunya

JF-Expert Member
Sep 18, 2015
1,909
2,000
Haya mambo ya Maombi Rais alitakiwa yeye atao tamka kuomba watu wafanye Maombi ya Taifa badala Yake Rais anaunda Tume .
Yupo pekee yake Ikulu anavaa Barakoa

Akiwa Na mgeni wapo 2 Ikulu kwenye mazungumzo mgeni kavaa barakoa na yeye anavaa barakoa. Akivaaa mmoja Barakoa inatosha
Sijajua wataalamu wa AFYA wanamahauri vipi
 
Bulesi

Platinum Member
May 14, 2008
10,300
2,000
Huyu si ndio alianzisha NYUNGU day? Hawa wazaramo taabu sana!! Ukiwa na wake watatu chances za kuambukizwa corona ni kubwa kuliko ukiwa na mke mmoja; hasa hawa wazaramo na wakwere wanaoshinda kucheza ngoma!
 
peno hasegawa

JF-Expert Member
Feb 24, 2016
3,923
2,000
Waziri wa nchi ofisi ya Makamu wa rais muungano na mazingira, Suleiman Jaffo ameongoza maombi ya kumwombea rais Samia Suluhu pamoja na Taifa kuepuka ugonjwa hatari wa Corona na kuzitaka taasisi zingine za dini hapa nchini kusimamia amani ya nchi .

Akiongea wakati wa maombi hayo yaliyofanyika makao makuu ya taasisi ya dini ya kiislamu ya Twariqa mjini Moshi, Mkoani Kilimanjaro waziri Jaffo amesema ipo haja kwa taasisi zote za dini hapa nchini kuliombea taifa kuepuka mifarakano inayoweza kuhatarisha amani ya nchi.

Alisema uamuzi uliofanywa na taasisi ya Twariqa kuliombea taifa ni Jambo jema linalopaswa kuigw na taasisi zingine za dini chini ili kuepuka ugonjwa hatari wa Corona ambao umelikumba taifa na dunia kwa ujumla.

Akitolea mfano nguvu ya maombi ilivyokimbiza ugonjwa wa Corona hapa nchini ,pamoja na kimbunga hatari cha Jobo kilichotishia amani ya nchi ni kielelezo kwamba ipo haja kwa viongozi wa dini kuzidisha nguvu ya maombi ili taifa liendelee kubaki salama.

Awali katibu wa taasisi hiyo ya Twariqa Yahaya Mkindi alisema lengo la kuwakutanisha waislamu na waziri Jaffo katika makao makuu ya taasisi hiyo ni kuliombea Taifa kuepuka ugonjwa hatari wa korona sanjari na kumwombea rais Samia Suluhu Hasan aweze kuliongoza Taifa vema akiwa na hofu ya mungu Kama mwanamke wa kwanza Tanzania kuwa rais wa kike.

"Tumekutana hapa kwa ajili ya kuombea janga la gonjwa wa covd 19 likae mbali na Tanzania pamoja na kumwombea rais Samia Suluhu Kama mwanamke wa kwanza kuliongoza Taifa la Tanznaia"alisema

Aidha katika hatua nyingine katibu mkuu Mkindi alisema taasisi hiyo ipo katika hatua ya mchakato wa ujenzi wa kituo Cha afya Cha mama na Mtoto kitakachosaidia akina mama kujifungua na kuepusha Vifo visivyo vya lazima.

Kwa upande wake msemaji mkuu wa Twariqa sheikh Haruna Hussein aliwataka waislam kuendelea kuwa wamoja na kuepuka mifarakano isiyo na tija inayotokana na kugombea madaraka kwa waislamu wasiotaka mabadiliko kuendelea kung'ang'ania madarakani.

Alisema maombi hayo yaliyowakutanisha pia viongozi wa wakuu wilaya ya Moshi mjini na meya wa Juma Shaibu Hussein alisema Amani ni tunu ya nchi hivyo kila kiongozi anapaswa kudumisha Amani na kuielezwa Amani kwa jamii yote inayomzunguka.

Ends...

View attachment 1795019
"Chato wanakulaani Mh. Jaffo"
 
Snowden E

JF-Expert Member
Apr 27, 2018
540
1,000
Huyu si ndio alianzisha NYUNGU day? Hawa wazaramo taabu sana!! Ukiwa na wake watatu chances za kuambukizwa corona ni kubwa kuliko ukiwa na mke mmoja; hasa Hawa wazaramo na wakwere wanaoshinda kucheza ngoma!
Wivu tu...wazaramo wamekukosea nini...
Umekatazwa kuoa wake watatu.
 
Sir_Mimi

JF-Expert Member
Jun 21, 2013
7,141
2,000
Yale yale siasa,huyu si ndiye kiongozi wa kwanza wa serikali kuonekana hadharani amevaa barakoa tena kwenye msiba wa bosi wake aliyekuwa anapiga nae mapambio ya hakuna Corona?
 
mmh

JF-Expert Member
Nov 9, 2010
2,863
2,000
Jafo kaongea kama mkuu wa nchi kongole.
Jinsi Mungu alivyoumba dunia yake huwezi kupata vacuum za kiuongozi, kukiwa na vacuum tu automatically atatokea kiongozi kufill gape hilo.
Asante Jafo Mungu aendelee kukutumia
 
Mr.Junior

JF-Expert Member
Sep 8, 2013
10,463
2,000
Haya mambo ya Maombi Rais alitakiwa yeye atao tamka kuomba watu wafanye Maombi ya Taifa badala Yake Rais anaunda Tume .
Yupo pekee yake Ikulu anavaa Barakoa,
Akiwa Na mgeni wapo 2 Ikulu kwenye mazungumzo mgeni kavaa barakoa na yeye anavaa barakoa. Akivaaa mmoja Barakoa inatosha
Sijajua wataalamu wa AFYA wanamahauri vipi
Bro unajua ulichoandika?
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom