Waziri Jaffo (TAMISEMI) aagiza kila Mkuu wa Mkoa kujenga viwanda vipya 100

Hivi punde

JF-Expert Member
Apr 1, 2017
2,554
8,552
Kila mkuu wa mkoa nchini ameagizwa kujenga viwanda vipya 100 katika kipindi cha mwaka mmoja kinachoanzia Desemba 2017.

Akizungumza na wakuu wa mikoa wapya walioapishwa juzi Ikulu jijini Dar es Salaam, waziri wa nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Selemani Jafo aliwataka kuitekeleza ipasavyo sera ya ujenzi wa viwanda.

Jafo alisema lengo la Serikali ni kuhakikisha kuwa ifikapo Desemba 2018 kila mkoa uwe umejenga viwanda vidogo na vya kati visivyopungua 100.

Alisema mikoa 26 ya Tanzania Bara inatakiwa kuwa na viwanda vipya vidogo na vya kati visivyopungua 2,600 ifikapo Desemba 2018. Alisema Serikali imekusudia kufikia nchi ya uchumi wa kati kupitia ujenzi wa viwanda huku akiwataka wakuu hao kuibua viwanda vidogo na vya kati kwa kuhamasisha ushiriki wa viongozi ndani ya mikoa na wananchi katika maeneo yao ya utawala.

Jafo aliongeza kuwa, katika kusimamia utekelezaji wa agizo hilo ofisi yake itaweka utaratibu maalumu wa kupima utendaji kazi wa kila kiongozi wa mkoa kwa kuangalia ushiriki wake wa kuwajengea hamasa viongozi wa chini wakiwamo wakuu wa wilaya na wananchi.

Alisema katika kufanikisha dhana ya ujenzi wa uchumi wa viwanda, Serikali inaendelea kuweka mkazo na kipaumbele katika upatikanaji wa malighafi za kilimo na kuwataka wakuu wa mikoa kuhakikisha kuwa maofisa ugani wanatekeleza vyema majukumu yao ya kazi.

Pia, aliwataka wakuu hao wa mikoa kusimamia makusanyo ya fedha za ndani katika halmashauri na kutumia vyema asilimia tano zinazotengwa kuwawezesha wananchi kupata mikopo ili washiriki katika ujenzi wa uchumi wa viwanda.

Mkuu wa Mkoa wa Mara, Adam Malima alisema ili kufanikisha dhana ya uchumi wa viwanda, Serikali haina budi kuwapa msukumo na ushirikiano wa karibu wanasayansi utakaowezesha kuibua viwanda vingi zaidi pamoja na kuhakikisha upatikanaji wa malighafi za kilimo nchini.

Mbali na Malima, wakuu wengine wa mikoa waliohudhuria mkutano huo ni Robert Luhumbi (Geita), Joachim Wangabo (Rukwa), Galesius Byakanwa (Mtwara) na Christine Mndeme (Ruvuma).

Soma pia:

1) Jafo: Utekelezaji viwanda 100 kila mkoa umefika nusu ya lengo kitaifa

2) Ushauri wangu kuhusu ujenzi wa Viwanda 100 kila mkoa na kila mwaka
 
Duh mbona lengo kubwa sana? Mimi nadhani walao wangesema kila Mkoa kuwa na viwanda 15 hadi 25 tena viwe productive na bidhaa zinazozalishwa ktk kila Mkoa serikali isaidie kuwatafutia masoko. Halafu bidhaa hizo kufanyiwa promotion ndani na nje ya nchi ili viweze kujimudu kwa muda mrefu. Halafu mwaka unaokuja lengo jipya tena viwanda 15 hadi 25 tena. Huku tunavifanyia tathimini hivi vya mwaka uliopita halafu tunajenga vipya. Mdogo mdogo tunafika tu.
Tusikimbilie kwenye ukubwa au wingi wa data.
 
mimi nilijua tuu Jaffo ni mzuri katika ufuatiliaji lakini sio mzuri katika kutunga sera,mipango na mikakati,Simbachawene alikuwa mzuri sana katika hili la kutunga sera mipango na mikakati ni vile tuu kakumbwa ajali ya kisiasa.
 
Awape tu nauli na pesa za malazi wakianza kuwasaka hao 100.
Jamani fursa hiyooooo lazima hakutakuwa na usumbufu wa kufungua kiwanda wakiwa na malengo kama haya.
 
Duh mbona lengo kubwa sana? Mimi nadhani walao wangesema kila Mkoa kuwa na viwanda 15 hadi 25 tena viwe productive na bidhaa zinazozalishwa ktk kila Mkoa serikali isaidie kuwatafutia masoko. Halafu bidhaa hizo kufanyiwa promotion ndani na nje ya nchi ili viweze kujimudu kwa muda mrefu. Halafu mwaka unaokuja lengo jipya tena viwanda 15 hadi 25 tena. Huku tunavifanyia tathimini hivi vya mwaka uliopita halafu tunajenga vipya. Mdogo mdogo tunafika tu.
ni miaka miwili sasa kila mkoa ulipaswa uwe na mpango wa kueleweka wa kujenga viwanda
 
Back
Top Bottom