Waziri Jaffo (TAMISEMI) aagiza kila Mkuu wa Mkoa kujenga viwanda vipya 100

Serikali ya Maagizo ya ajabu!

How do you expect an RC to supervise au Kujenga viwanda hivi Jafo amekuwa so desperate mpaka aagize wakuu wa Mikoa kujenga viwanda and even set a KPI what a shame!

Serikali imeshindwa kujenga vyoo na ofisi za waalimu Dar Es Salaam na kumwachia Bashite awe ombaomba kwa watu wamchangie! And this brand new Minister aliyechukua nafasi ya Simbachawene kuagiza wasimamie Ujenzi wa viwanda tena na idadi kasema 100 kwani ni madarasa ya shule?

Some things are hard to swallow imagine Simiyu hakuna maji then how do you dream of building a kiwanda bila maji na umeme wa uhakika? Kujenga kiwanda inabidi ufanye upembuzi yakinifu about resources and corresponding markets you don’t simply jenga bila ya kuwa na uhakika wa raw materials, usafiri , distribution chain and right technology plus the right size manpower!

Kwa maagizo haya it’s zero output hata kama ni cherehani ni lazima ujuue nyuzi pamoja na majora ya vitambaa unapata wapi and the demand must be firmed! Maajabu ya CCM ni makubwa!!!
 
Kikubwa ni ajira, bidhaa /Huduma, na kipato vipatikane mbona bodaboda anajenga nyumba na kuhudumia familia yake vizuri?
Kwa hiyo hata kuendesha bodaboda ni kiwanda...aisee....au kuna tafsiri mbalimbali za neno kiwanda???Bac sawa lkn manake hata Mwijage alisema vyerehani vinne ni kiwanda....
Kwa hali hii....inapaswa serikali itoe semina inaposema kiwanda inamaanisha nn..aiseee
 
Duh mbona lengo kubwa sana? Mimi nadhani walao wangesema kila Mkoa kuwa na viwanda 15 hadi 25 tena viwe productive na bidhaa zinazozalishwa ktk kila Mkoa serikali isaidie kuwatafutia masoko. Halafu bidhaa hizo kufanyiwa promotion ndani na nje ya nchi ili viweze kujimudu kwa muda mrefu. Halafu mwaka unaokuja lengo jipya tena viwanda 15 hadi 25 tena. Huku tunavifanyia tathimini hivi vya mwaka uliopita halafu tunajenga vipya. Mdogo mdogo tunafika tu.
Tusikimbilie kwenye ukubwa au wingi wa data.
Viwanda 100 kwa mkoa ni vidogo sana.

Kwa mfano Singida kuna alizeti mpaka inaoza, viwanda havizidi kumi
Huu ni wakati wa kufanya kazi serikalini kwa kutumia KPI's, key performance indicators! Kama huku perform unakwenda na maji.

Mbona Makonda anahangaika na kazi inaonekana?
 
Kwa hiyo hata kuendesha bodaboda ni kiwanda...aisee....au kuna tafsiri mbalimbali za neno kiwanda???Bac sawa lkn manake hata Mwijage alisema vyerehani vinne ni kiwanda....
Kwa hali hii....inapaswa serikali itoe semina inaposema kiwanda inamaanisha nn..aiseee
Sijasema bodaboda ni kiwanda bali ni sehemu ya vyanzo vya ajira kama viwanda, sababu lengo la kujenga viwanda ni kutengeneza ajira na kipato kwa wananchi.

Viwanda vingi China vilianzia nyumbani China taifa lililopiga hatua kiviwanda zaidi ya 40% ya viwanda huko vinaendeshwa nyumbani viwanda vidogovidogo.
 
Huyu waziri kachafukwa! Viwanda 100kwa kila mkoa tena ndani ya mwaka! Hebu mwenye ueledi na kauli hii atudadavuilie.
Hivi amewaza juu ya upatikanaji wa mitaji? Anaujua urasimu wa mabenki yetu na riba zake? Amewaza juu ya masoko ya bidhaa zitakazozalishwa? Na ubora wa bidhaa hizo nayo ni changamoto. Hebu akae chini aitafakari na kuifanyia ukarabati hoja yake isiyotekelezeka!
 
Viwanda 100 kwa mkoa ni vidogo sana.
Kwa mfano singida kuna alizeti mpaka inaoza,viwanda havizidi kumi
Huu ni wakati wa kufanya kazi serikalini kwa kutumia KPI's,key performance indicators!kama huku perform unakwenda na maji.
Mbona Makonda anahangaika na kazi inaonekana?
Nimekuelewa hoja yako sasa inamaanisha kuna baadhi ya Wakuu wa Mikoa hawatoi kipaumbele cha kutosha kwenye ujenzi wa viwanda. Sasa hawa wanaihujumu serikali ni lazima watoke. Lakini je kuwatoa ndio solution? Maana ujenzi wa viwanda unahusisha ushirikiano kati ya serikali na sekta binafsi.
 
ni miaka miwili sasa kila mkoa ulipaswa uwe na mpango wa kueleweka wa kujenga viwanda
Hivi viwanda hivyo ni vya serikali au watu binafsi? Kama anategemea watu binafsi wavijenge atasubiri sana kuroka na sera ya mwenyekiti kutaka matajiri wachache waliokuwepo waishi maisha ya kishetani jambo ambalo limefanikiwa sana.

Na asisahau pia kuwa hata wakija wageni kuvijenga watakimbia mapema kutokana na mlolongo wa kodi. Sioni litakalofanyika zaidi ya kuzungumza na kuagiza visivyotekelezeka!
Awape mitaji na mikopo kutoka BoT.
 
Lo viwanda hivyo ni vingi mno,na umeme utatokea wapi wa kutosheleza viwanda vipya 2600?
Ipo mikoa haina barabara ya uhakika,kwa ufupi miundo mbinu.
Tengeneza 5 year financial plan kwanza ya viwanda.
 
Mawaziri mshindwe wakuu wa mikoa wataweza kweli?..
Punguza lwambe bhana hao sio mtaji wa viwanda kaz yao kuu ni kuzurura na polisi kukamata upinzani.
 
Hahahahahah mtafute comedian Mwijage atasema serikali haijengi viwanda inaweka sera ili iweje binafsi ijenge viwanda........sasa viwanda 100 ni sawa binafsi au serikali?? Wameanzia mguu wa kulia!! Tungeanzi kilimo cha kisasa na procesisng machines zake.......kuweka thamani mazao yatakayolimwa kwakilimo kisasa!!!!!!! Viwanda mchezo....... !! Labda kama machine kukamua juice na kutengeneza koni ni viwanda hapo sawaaaa
 
Kujenga vyoo tu vya shule tunashindwa, sembuse viwanda 100.
Sijui tafsiri ya Viwanda kwa huyo waziri ni vioksi vya kuuza mihogo na chapati?
Mkuu wa mkoa akasimamie kujenga viwanda 100 kwa mwaka mmoja. How?
Ni uwendawazimu huo.
 
  • Thanks
Reactions: SDG
Back
Top Bottom