Waziri huyu kwa matamko sasa amezidi, Uongo una faida gani?

MAHANJU

JF-Expert Member
Aug 26, 2014
5,244
7,966
Niwaulize tu jamani, hivi si ndio waziri huyu huyu alitamka kua waliomaliza darasa la saba tu wataanza kudahiliwa chuo kikuu?

Mbona sasa amegeuka anataka form 6 tu? Alisema kwa ulimi wake kua watu wa aina hiyo watakua na utaratibu maalum utakaowawezesha kwenda chuo kikuu lakini amesahau maneno yake? Hii ni shida.

Ifike mahali tuwe na hofu ya Mungu, tusijifanye kuwa miungu watu.
 
Niliwaambia sheria mpya ya habari ianze na mawaziri Wa Magufuli waongo ...

Wanatoa habari za uzushi na kuja kuzikana ......

Wanatoa habari za uchochezi na kuzikana....

Eti professor labda pro uchwara laana ya kusaliti watanzania na kabadilika wakati mliaidi kuwa viongozi wa wanyonge itawatafuna milele.......
 
Niwaulize tu jamani,hivi si ndio waziri huyu huyu alitamka kua waliomaliza darasa la saba tu wataanza kudahiliwa chuo kikuu?
Mbona sasa amegeuka anataka form 6 tu? Alisema kwa ulimi wake kua watu wa aina hiyo watakua na utaratibu maalum utakaowawezesha kwenda chuo kikuu lakini amesahau maneno yake? Hii ni shida.

Ifike mahali tuwe na hofu ya Mungu, tusijifanye kua miungu watu.

Hivi kweli alikuwa yeye
 
Lissu aliwahi kusema kuwa endeleeni kukaa kimya haki ya wenzenu ikikanyagwa kwa sababu mnamini haiwahusu, na siku haki yako ikikanyagwa ndiyo utajua kuwa pia yaliyomkuta mwezako yanakuhusu na wewe.

Leo kwa pamoja wote namba zinawahusu ingawa mlichekelea bunge kutokurushwa live, mlichekelea sheria katili ya mitandao,
mlichikelea kijitabu cha Nape cha kubana haki ya kutoa na kupata habari,
Mlichekelea maalim Seif kubentwa ushindi October 2015,
mlichekelea marehemu Kabwe akisulubiwa na Makonda jukwaani,
mlichekelea Pogba akipiga marufuku shuhuli za kisiasa hadi 2020;

Leo wewe yamekukuta ya kutodahiliwa degree hadi ufaulu A-level, je la leo alikuhusu uendelee kuchekelea?
 
Waislam tulivyomfanyia maadamano huyu Ndalichako alipokuwa NECTA mlitusema sana, sasa mnayaona?

Kulikoni? Au ndiyo mkuki kwa nguruwe kwa binaadam mchungu!
 
Back
Top Bottom