Waziri Gwajima, Wizara yako ifanye kampeni ya Afya ya Akili ili Watanzania wawe na uelewa na kuwalinda wazazi wetu

jMali

JF-Expert Member
Nov 9, 2010
8,392
4,942
Dkt. Gwajima D Wasalaam,

Ni tatizo la kawaida kwa watu wazima kupoteza uwezo wa kiakili au kupoteza kumbukumbu kadiri umri unavyokwenda. Hata hivyo kwa baadhi ya Watanzania hili suala halijulikani sana. Kuna wenzetu huko wanakotoka labda hakuna wazee au labda wazee wao tatizo hili hawana, kwa hiyo hawana ufahamu hata kidogo juu ya hili suala la wazee kuwa senile.

Matokeo ya ujinga huu ni kudhalilisha wazee ambao wamefikwa na masaibu haya kwa kuwaita wachawi na pengine hata kuwaua huko Kanda ya Ziwa, kwa sababu tu sometimes hawaeleweki n.k.

Nimesikitika kuona video moja mtandaoni ambayo inamuonyesha mama mtu mzima anatembea usiku akiwa uchi wa mnyama huko maeneo ya Chamazi. Watu waliomzunguka wamevaa reflectors nadhani either ni Bodaboda au walinzi Shirikishi wanamchukua video zaidi na wengine hata kumshika maungo nyeti wakidai eti alikuwa “anawanga!”

Lakini kila kukicha kuna kesi nyingi tu za watu wenye matatizo ya akili umri kama huyo bibi kupotea, lakini hakuna mtu anaunganisha dots kuwa huenda hawa vichaa mitaani ni senile elders.

Tafadhali hii video haiwezi kuishia hivi hivi tu, naomba uchukue hatua, wanaozungumza sidhani kama wanashindikana kupatikana maana wako kiofisa zaidi na reflectors zao huko Chamazi. Hatua zichukuliwe kwa hao vijana wadhalilishaji. Hakuna kisingizio cha kumshika makalio mtu yoyote awe “mwanga” au la!

Pia hebu tufanye jambo kwa hizi imani uchwala. Tumekuwa jamii ya hovyo inayoamini ukikutana na mtu usiku yuko uchi basi amedondoka kwenye ungo! What nonsense! Wizara yako ifanye kampeni ya haya mambo ya afya ya akili ili Watanzania wawe na uelewa wa kuwalinda wazazi wetu hawa. Sio bibi wa watu katoka kujisaidia kapotelea mtaani anakwenda kukumbana na hawa vijana wa hovyo.

Obviously siwezi kuituma hiyo video hapa kwa kuhofia kumdhalilisha zaidi huyo bibi. Kama mpaka naandika thread hii huyo kesi ya huyo bibi haijulikani kabisa, basi tutafanya mawasiliano nikutumie. Otherwise nitashukuru nikijua kesi ya huyu Bibi wa Chamazi imeshughulikiwaje.

Nikutakie utumishi mwema.
 
Inasikitisha sana. Karne ya 21 tungali jamii yenye kuamini u wanga, majini, uchawi, +nyungu, nk.

Ulaya na Marekani ziliondoka huku yapata miaka 500 iliyopita.
 
Back
Top Bottom