#COVID19 Waziri Gwajima: Tanzania maambukizi yafikia watu 47 toka 14 kwa siku

Jabali la Siasa

JF-Expert Member
Jul 10, 2020
2,476
2,105
WAZIRI DK DOROTHY GWAJIMA AZINDUA MPANGO WA JAMII HARAKISHI NA SHIRIKISHI WA CHANJO YA COVID -19 AWAMU YA PILI

===
Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima amezindua Kampeni Harakishi na Shirikishi kwa Jamii awamu ya pili na kusema, changamoto za uwepo wa UVIKO 19 ni changamoto kwa maendeleo ya dunia nzima ikiwemo na Tanzania.

Dkt. Gwajima, ameyasema hayo leo Desemba 22, 2021, mkoani Arusha, ambapo Hafla hiyo imefanyika na kuhudhuriwa na Viongozi wa Serikali, Dini pamoja na Jamii sambamba na Wananchi wa Arusha na Mikoa ya Jirani.

Akizindua Mpango huo, Dkt. Gwajima, amesema, katika kipindi cha kuanzia Mwezi Disemba, 2021 nchi yetu pia imeshuhudia kuendelea kuongezeka kwa maambukizi mapya ya UVIKO-19 kutoka maambukizi 14 kwa siku hadi 47 miongoni mwa wasafiri kwa takwimu za vipimo vya maabara kuu ya taifa.

"Mafanikio ya mapambano haya yanategemea zaidi jinsi gani Wakuu wa Mikoa na vyombo vyenu mmeendelea kujipanga kila siku, kwa kuboresha mikakati ya kuwafikia wananchi hadi ngazi ya mitaa, vijiji na vitongoji ili waelimike wajikinge na wapate huduma ya chanjo. Alisema Dkt. Gwajima.

Kampeni ya kaya kwa kaya ya kuwashirikisha viongozi wa mitaa, vijiji na vitongoji inadhamira ya kuona mikoa mingine inafanya na kupata mafanikio makubwa zaidi kama Mwanza, Kagera na Ruvuma ilivyofanikiwa.

Dkt. Gwajima ametumia fursa hiyo, kuwaomba, Viongozi wa Mikoa na Halmashauri wanakua bega kwa bega ili kufikia azma yakuchanja watu wapatao 4000 hadi 5000 kwa Mkoa na watu 80,000 hadi 100,000 kwa nchi nzima kila siku.

Akitoa taarifa wakati wa hafla hiyo, Katibu Mkuu Wizara ya Afya Prof. Abel Makubi alisema, kwa sasa wameanza kufanya utafiti wa chanjo na wataendelea kutoa taarifa wapi tumefikia kwenye Chanjo hiyo, aidha "kwa sasa nchi ina mitambo ya kufua hewa ya Oksijeni kwenye hospitali zetu, hii itasaidia kuokoa maisha kwa wahitaji wa hewa kama watoto njiti na wagonjwa wengine mahututi" Prof.Makubi.

Akiongea kwa niaba ya Wakuu wa Mikoa, Mwenyekiti wa Wakuu wa Mikoa, nchini ambaye pia ni Mkuu wa Arusha, John Mongella, alisema, wamejipanga kutekeleza maelekezo ya Serikali.

"Mhe Waziri, sisi ni Wasaidizi wa Mhe. Rais, hii ajenda ameibeba mwenyewe Rais, kwa kuanza kuchanja, na sisi wengine baada yakuona amechanja, Wakuu wa Mikoa wote tukachanja, hii ni kuonesha kuunga mkono mapambano haya" alisema Mongela.

Naye Prof. Riziki Shemdoe, Katibu Mkuu Tamisemi, akizungumza kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Ummy Mwalimu, alisema, Mpango Harakishi na Shirikishi ni Mpango unaosimamiwa na Wizara zote ndio maana katika Kampeni hiyo wanashirikiana pamoja hasa ikizingatiwa kuwa Wizara hiyo ndio iliyo karibu zaidi na Wananchi.

Akitoa Salaam za Kamati ya Bunge, Mwenyekiti, Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Masuala ya Ukimwi Mhe. Fatma Tofiq, amesema wanaihakikishia Serikali, kuwa bega kwa bega katika kusukuma ajenda ya Chanjo. Naye Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma za Jamii Mhe. Dkt. Stanslaus Nyongo amempongeza Wizara ya Afya kwa namna ilivyoweza kutekeleza Maekezo ya Serikali pamoja na yale ya Bunge

^Mhe. Waziri kwaniaba ya Kamati ya Bunge, niwapongeze sana kwa jinsi mnavyotekeleza Maelekezo ya Bunge, lakini pia ya Serikali, niahidi kwaniaba ya Kamati kuendelea kukupa Ushirikiano wakati wote na kuwashauri inavyopaswa" Alisema Mhe. Nyongo.

Katika Hafla.hiyo, Waziri wa Afya, Dkt. Dorothy Gwajima aliitaja Mikoa vinara kwa Chanjo yaani iliyofanya vizuri katika Chanjo mpaka sasa kuwa ni Ruvuma, Mwanza, Dodoma, Kagera na Mara. huku akiitaka Mikoa mingine kuongeza bidii

IMG-20211222-WA0084.jpg

IMG-20211222-WA0082.jpg

IMG-20211222-WA0085.jpg

IMG-20211222-WA0079.jpg

IMG-20211222-WA0080.jpg
 
Huyu mama yupo kumbe..toka lini Nyongo nae ni Daktari?....Tanzania elimu inachezewa sana...very embarrassing .....
 
View attachment 2053776

View attachment 2053779

View attachment 2053780

View attachment 2053781

View attachment 2053783
Promoting Covid-19 Financial AID.
Je kuna rapid test locations ngapi?!
Gawaneni tu hamna shida.
 
Zile tetesi kwamba chanjo ya JJ inasababisha kuganda kwa damu kwenye ubongo, serikali imetolea ufafanuzi? Ikumbukwe wananchi wengi walipatiwa hizo chanjo.
Dunia nzima wamechanja mkuu hii chanjo, Chanjo ni salama ukiacha hiyo magnitude ndogo,
 
Wadau na Wakuu heshima yenu,
Naomba Kuuliza maswali ya Mtu nisielewa Kuhusu Afya na Kirusi,
Naomba Msinicheke...
Nahitaji Elimu wandugu.

Naomba Kuuliza kwa wataalam:
Hivi Kama Mtu hajachanjwa Mpaka sasa,
1. Je akiugua Corona sasa hivi atakuwa ameugua corona ipi? Ile ya Kwanza, Ya Pili au ya Tatu au hii Omicroni?

2. Je ina Maana Zile Corona na Mwanzo Hazipo? Kama Zipo Zina Nguvu ya Kuwashambulia watu wasiochanjwa?
Kama Hazina Nguvu sasa Wasiochanjwa wamepata Kinga ya Mwili?

3.Hii Omicron na Yenyewe Kuna watu wamepata Mafua na Homa za Hapa na Pale na Wanaendelea Ku recover na Hawajachanjwa sasa Baadae Wakihitajika Kuchanjwa? Wanachanjwa kwa ajili ya wimbi lipi?
Kuanzia La Kwanza? Au hili la Sasa hivi?
Naomba Majibu wataalam
 
#Naanza kumuelewa Dk Gwajima sasa, Mama chapa kazi, Hafi mtu hapa, Tukachanje

Wadau na Wakuu heshima yenu,
Naomba Kuuliza maswali ya Mtu nisielewa Kuhusu Afya na Kirusi,
Naomba Msinicheke...
Nahitaji Elimu wandugu.

Naomba Kuuliza kwa wataalam:
Hivi Kama Mtu hajachanjwa Mpaka sasa,
1. Je akiugua Corona sasa hivi atakuwa ameugua corona ipi? Ile ya Kwanza, Ya Pili ya Tatu au hii Omicroni?

2. Je ina Maana Zile Corona na Mwanzo Hazipo? Kama Zipo Zina Nguvu ya Kuwashambulia watu wasiochanjwa?
Kama Hazina Nguvu sasa Wasiochanjwa wamepata Kinga ya Mwili?

3.Hii Omicron na Yenyewe Kuna watu wamepata Mafua na Homa za Hapa na Pale na Wanaendelea Ku recover na Hawajachanjwa sasa Baadae Wakihitajika Kuchanjwa? Wanachanjwa kwa ajili ya wimbi lipi?
Kuanzia La Kwanza? Au hili la Sasa hivi?
Naomba Majibu wataalam
 
6 Reactions
Reply
Back
Top Bottom