#COVID19 Waziri Gwajima, takwimu za Covid-19 mnaandaa au mnapika?

brazaj

JF-Expert Member
Jul 26, 2016
27,822
35,817
Amesikika waziri Gwajima akisema wanaandaa takwimu za hali ya ugonjwa wa Corona nchini.

Watu wanapoendelea kufa huku takwimu zikiendelea kuandaliwa bila mwisho, ina maana gani?

Inachukua muda gani kujua idadi ya wagonjwa waliolazwa mkoa kwa mkoa, vifo au waliopona?

Hapa tuna mwenzetu mwingine kwenye yale majina makubwa, katutangulia:

Padre Haule wa St Peters afariki dunia

Yaonesha mwendo ni ule ule mmoja mmoja kivyake vyake hadi yatakapotukuta huku tukilipa kodi na tozo zilizo boreshwa.

Mko kama vile mnachohitaji kwetu ni pesa tu pasipo na kuwajibika.
 
Mzee leo nimepokea taarifa za msiba, kuna jamaa wa karibu amekutwa na changamoto za mfumo wa upumuaji kwa siku nne, akashindwa kumaliza hii wiki, wamethibitisha ni UVIKO-19, nimeenda kutoa pole na kuondoka, msiba wenyewe ni familia tu ndio wapo wamejitahidi kuzuia watu kukaa msibani, unafika kutoa pole na kugeuza!

Sijui na huyo atahesabiwa na Dorothy au la.
 
Mzee leo nimepokea taarifa za msiba, kuna jamaa wa karibu amekutwa na changamoto za mfumo wa upumuaji kwa siku nne, akashindwa kumaliza hii wiki, wamethibitisha ni UVIKO-19, nimeenda kutoa pole na kuondoka, msiba wenyewe ni familia tu ndio wapo wamejitahidi kuzuia watu kukaa msibani, unafika kutoa pole na kugeuza !

Sijui na huyo atahesabiwa na Dorothy au la.

Pole sana mkuu.

"Watu wanakufa sana na asiyeliona hilo atakuwa tu hajaguswa." Hayo si maneno yangu bali yake SSH.

#COVID19 - Chanjo isiwe Siasa, Vigezo na Masharti vizingatiwe

Kumeingizwa siasa katika ugonjwa huu ya kiwango cha SGR.

Wala haipo tofauti sasa na hata ilivyokuwa awamu ya 5 kwenye zama za nyungu.
 
Awamu hii inafanya zaidi maigizo ilikuwa na "optics" nzuri, kwamba tunatoa chanjo, tuna miongozo ya kujilinda na covid lakini hakuna dhamira ya kweli ya kupambana na huu ugonjwa. Mabasi yanajaa kama kawaida, matamasha yanaendelea ni kama tu awamu ya tano.

Dortothy, na Mwenzake Mollel hawana moral authority ya kuongoza haya mapambano. Hakuna haja ya lockdown wala kutishana, ni suala la kuelezana ukweli wa hali halisi ili kila mtu ajilinde. Wengi wanaanza kujilinda na kuchukua tahadhari baada ya makubwa kuwakuta.
 
Unajilinda vipi binafsi kwenye janga hili ambalo kina jpm, Maalim, waziri mramba nk pamoja na mabunduki kuwalinda halikuwanusuru?

Mikusanyiko kama ya mbio za mwenge, makanisani, misikitini, misibani, magulioni, masokoni, nk miye na wewe tunaishurutisha vipi kuwa salama?

Serikali inajua uchumi wa watu umetetreka mno na janga hili? Vipi kodi na tozo zaidi zinazotuhusu sisi tu lakini si wao?

Vipi sisi kujigharimia matibabu tunapokumbwa na UVIKO?

Mboma tumetelekezewa janga?
 
Amesikika waziri Gwajima akisema wanaandaa takwimu za hali ya ugonjwa wa Corona nchini.

Watu wanapoendelea kufa huku takwimu zikiendelea kuandaliwa bila mwisho, ina maana gani?

Inachukua muda gani kujua idadi ya wagonjwa waliolazwa mkoa kwa mkoa, vifo au waliopona?

Hapa tuna mwenzetu mwingine kwenye yale majina makubwa, katutangulia:

Padre Haule wa St Peters afariki dunia

Yaonesha mwendo ni ule ule mmoja mmoja kivyake vyake hadi yatakapotukuta huku tukilipa kodi na tozo zilizo boreshwa.

Mko kama vile mnachohitaji kwetu ni pesa tu pasipo na kuwajibika.
Acha wafe shida ipo wapi.kwani takwimu itazuia watu kufa
 
acha wafe shida ipo wapi.kwani takwimu itazuia watu kufa

Acha wafe -- kauli fikirishi kutoka kwa binadamu mwenye akili timamu.

Ni ujinga uliopitiliza kuwasemea hivyo watu wasio kuhusu.

Inahitaji busara ya kawaida mno kuonyesha kuwa takwimu zikitolewa zitasaidia kupunguza vifo.
 
Nchi ilitulia hii na corona,mkaichokonoa mpaka imerudi ,acha mfe tu
 
Kuna muda tulisema corona haituathiri sana kwa sababu population yetu asilimia kubwa wengi ni vijana ila sasa nasikia tunasema watu wanakufa sana, sasa sijaelewa hao wanaokufa sana ni katika wale wachache ambao ni wazee au sasa hivi wanakufa hadi vijana?
 
IMG_20210820_111307_441.jpg
 
Back
Top Bottom