Waziri Gwajima: "Nawaagiza Polisi na TAKUKURU" - Hii kauli kutamkwa na waziri ni sahihi?

Hao DC na rc ni wenyeviti wa kamati za ulinzi na usalama wa sehemu zao. Waziri huyo Hana mamlaka ya kuamrisha jeshi isipokua waziri husika.
Ndio nasikia Leo, hii umeitoa wapi? Au umeongea tu?
 
Rais ndie mkuu wa nchi na mawaziri waandamizi ndio wasaidizi wake kwa kupitia baraza la Mawaziri. Tusitarajie matamko yote yatoke kwa Rais. Hata mkuu wa Wilaya anamweka mtu ndani itakuwa Waziri? Tutulie Serikali ichape kazi kila kitu kipo kwenye mstari. Kama barua inahitajika atapewe. Waziri yupo juu ya IGP ndio maana anampigia salute period. Hata makonda alimtuma kazi IGP leo mnahoji WAZIRI?
 
Ni vile tu hizi nchi zetu hazifuati ethics, Dr. Gwajima hata na Dr. Mollel walitakiwa kujiuzuru baada tu ya ile tume iliundwa na rais kuja na mapendekezo yale ya njia za kujikinga na corona, kamati ilikuja na mtazamo tofauti kabisa na yale waliotwambia wao mapema mwaka hu, kile kinacho hubiriwa na kina askofu GWajima ndicho hicho hicho wao walicho twambia tena through media kubwa kama TBC, Wasafi nk halafu huyo huyo leo tena hadi anatishia watu wanahubiri alichotwambia yeye mwenyewe miezi michache iliopita? Hivi vingapi wanavikana hawa?
 
Mkuu, samahani ukipata muda wako unisaidie kidogo kwanini iwe kwa hawa wakuu wa wilaya na mikoa na isiwe kwa waziri? Natamani kuelewa zaidi.
DC na RC ni wenyeviti wa kamati za ulinzi na usalama!

DC na RC ni wawakilishi wa Rais.

Waziri ni msaidizi wa Rais.
 
Mkuu, samahani ukipata muda wako unisaidie kidogo kwanini iwe kwa hawa wakuu wa wilaya na mikoa na isiwe kwa waziri? Natamani kuelewa zaidi.
Hao ni wenyeviti wa kamati za usalama kwenye maeneo yao ya utawala; DC kwenye mambo ya usalama OCD ana report kwake na RPC kuhusu mambo ya usalama wa mkoa anaripoti kwa RC but waziri?????
 
Leo hii ndio mnajua madhara ya vitu mlivyoshindwa kukemea utawala wa jiwe?

Mmesahau Makonda aliyekua anajibishana na kuwadhalilisha viongozi wenzie??

Kwa kauli zile za Makonda na miungu watu wengine wa awamu ya kidhalimu mlishindwa kukemea orders za ovyo leo ndio mmeona umuhimu?
 
Tu
Waziri ni mtu mkubwa sana sema Magufuli aliwafanya wadharaulike kwa kutaka kila kiki iwe yake.

Wakati tunakua Mawaziri kama Mungai, Makweta, Ngasongwa, Njelu Kasaka, Pius Ng'wandu, Steven Wasira n.k walikuwa wakiongea nchi na magazeti yote ni front page na watu wanatii. Tena walikuwa hawatumbuliwi ovyo ovyo.

Leo hii Waziri anabishiwa hadi na Makonda au Sabaya.

Aliyekuwa mkuu wa wilaya ya Kilolo/Asia alimchana Majaliwa kuwa hujaniteua wewe, jamaa akawa mpole.
Tuambie ni sheria ipi inampa ruhusa ya kuliamrisha jeshi la polisi
 
Kwa wale wajuzi wa itifaki na mambo ya chain of command naomba mnielimishe katika hili.

Mungu ni mwema wakati wote!
Waziri wa Afya hakupaswa kutoa kauli kama hii, sio kazi yake hata kama walikuwa na mpango wa kumkamata na kumhoji.
Ni ulevi wa madaraka katika nafasi na kupenda "kiki" vinawaponza wengi wa wateule.
 
Back
Top Bottom