Waziri Gwajima: "Nawaagiza Polisi na TAKUKURU" - Hii kauli kutamkwa na waziri ni sahihi?

Waziri ni mtu mkubwa sana sema Magufuli aliwafanya wadharaulike kwa kutaka kila kiki iwe yake.

Wakati tunakua Mawaziri kama Mungai, Makweta, Ngasongwa, Njelu Kasaka, Pius Ng'wandu, Steven Wasira n.k walikuwa wakiongea nchi na magazeti yote ni front page na watu wanatii. Tena walikuwa hawatumbuliwi ovyo ovyo.

Leo hii Waziri anabishiwa hadi na Makonda au Sabaya.

Aliyekuwa mkuu wa wilaya ya Kilolo/Asia alimchana Majaliwa kuwa hujaniteua wewe, jamaa akawa mpole.
 
Waziri yupo ndani ya executive ambapo kazi ya executive Ku in force law..........so wazir ana power hiyoooo
 
Waziri hana mamlaka ya kutoa amri ya kukamata (detain/arrest). Huwa wanalazimisha haswa huko vijijini wakitembelea.
Mkuu wa Wilaya na Mkoa wanayo mamlaka hayo.
Mkuu, samahani ukipata muda wako unisaidie kidogo kwanini iwe kwa hawa wakuu wa wilaya na mikoa na isiwe kwa waziri? Natamani kuelewa zaidi.
 
Mbona DC anamuarisha IGP? Au mmeshasahau huu mjadala?
Hao DC na rc ni wenyeviti wa kamati za ulinzi na usalama wa sehemu zao. Waziri huyo Hana mamlaka ya kuamrisha jeshi isipokua waziri husika.
 
Back
Top Bottom