Waziri Gwajima: Mwalimu Gabriel aliwafanyia ukatili wa kingono takriban wanafunzi wote wa darasa la awali Shule ya Global International

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,794
141,691
Waziri wa Jinsia na watoto Dkt. Gwajima amesema uchunguzi wa shule ya Global international umeonesha wanafunzi takriban wote wa darasa la awali, wanafunzi wengine mpaka wa darasa la tatu aliokuwa anawafundisha walifanyiwa unyanyasaji wa kingono.

Ripoti hiyo imekuja baada ya watoto(wanafunzi) kuhojiwa na kudai kuwa Mwalimu huyo alihusika kuwafanyia vitendo hivyo ambapo alikuwa akiingia darasani anaziba dirisha na kufanya matendo hayo.

Pia Waziri Gwajima ametoa onyo kali kwa Shule hiyo baada ya kudaiwa kuwatisha wazazi kutoa ushirikiano kwa mamlaka kwa madai kuwa shule hiyo ni ya wakubwa Serikalini.

Muhusika ni Mwalimu Gabriel ambaye ameshakamatwa na Kesi iko mahakamani

Chanzo: ITV habari

Pia soma
 
Nahisi hii international ina watoto wa kishua waliolelewa kizungu kwa hiyo mitoto ya kike inavyaa vikaptula na vimini inakaa mbele ya teacher aliyebarehe juzi, sasa unategemea nini
 
Nahisi hii international ina watoto wa kishua waliolelewa kizungu kwa hiyo mitoto ya kike inavyaa vikaptula na vimini inakaa mbele ya teacher aliyebarehe juzi, sasa unategemea nini
Hapana si kweli mkuu. Hii shule mbona ni zile english medium za hali ya chini naweza kusema...? Naifahamu hii shule wala haina huo 'ushua'.
Halafu mkuu, hivi kumbe vitoto vya nursery vikivaa vimini huwa unapandisha stimu za kuwaingilia?
Hakuna namna yoyote ya kujustify huu ushenzi alioufanya jamaa.
 
Kuna binadamu wana roho mbaya sana, pamoja na sheria zilizopo lakini huyu ilipaswa watuachie wananchi wenye hasira kali tumalizane naye. Haya mambo ya mahakamani anaweza kuchomoka tu kama Sabaya.
Mkuu uwe unachangia mada sensitive kama hizi kwa kutumia akili ya ziada....kwa kuwa kesi iko mahakamani tusubiri hukumu....sometimes kesi kama hizi hutengenezwa. So usipende kujichukulia sheria.
Leo unamwamini mh.gwajima aliyemislead wananchi kipind cha covid19. Huyo waziri hamna kitu hapo
 
Kuna binadamu wana roho mbaya sana, pamoja na sheria zilizopo lakini huyu ilipaswa watuachie wananchi wenye hasira kali tumalizane naye. Haya mambo ya mahakamani anaweza kuchomoka tu kama Sabaya.
Hii ndiyo comment yangu Bora ya mwaka huu....
Pamoja Saanaa mkuu
 
Dah!! Kuna shida mahali hii si kawaida...Kama Taifa kuna haja ya kutafuta Tiba mbadala ya hili tatizo.
 
Nakazia tu: wazazi mnaopeleka watoto tuition za vichochoroni kwa mwalimu/walimu fulani fulani jiridhisheni na tabia za hao watu. Wengi wao si watu wazuri.
 
Nahisi hii international ina watoto wa kishua waliolelewa kizungu kwa hiyo mitoto ya kike inavyaa vikaptula na vimini inakaa mbele ya teacher aliyebarehe juzi, sasa unategemea nini
Wanafunzi wa awali wanamtamanishaje mtu hadi kufikia kutaka kungonoka nao?

Usiwe na mawazo ya kuchukulia poa hizi tabia za kishaitwani
 
Kuna binadamu wana roho mbaya sana, pamoja na sheria zilizopo lakini huyu ilipaswa watuachie wananchi wenye hasira kali tumalizane naye. Haya mambo ya mahakamani anaweza kuchomoka tu kama Sabaya.
Takbiir
 
Huyo hakutakiwa kuwa na kesi mahakamani ni kitanzi moja kwa moja kaharibu saikolojia ya watoto na future yao
 
Kuna binadamu wana roho mbaya sana, pamoja na sheria zilizopo lakini huyu ilipaswa watuachie wananchi wenye hasira kali tumalizane naye. Haya mambo ya mahakamani anaweza kuchomoka tu kama Sabaya.
Miongoni mwa faida za kumpata Muhalifua akiwa hai ni pamoja na kuweza kujua chanzo cha tatizo, na hiyi ni kwa ajili ya kutafuta suluhisho kwa siku za usoni sambamba kupata rekodi sahihi za visababishi...ambapo sasa kuanzia hapo mnaweza kuwashauri Wazazi na Shule namna ya kuchukua tahadhari n.k.

Na kwa kuwa uhalifu ulishatendeka hata kumuua hakutarekebisha madhara aliyokwishafanya.
 
Nahisi hii international ina watoto wa kishua waliolelewa kizungu kwa hiyo mitoto ya kike inavyaa vikaptula na vimini inakaa mbele ya teacher aliyebarehe juzi, sasa unategemea nini
Usiahalalishe ujinga Mkuu.

Kwa hiyo Mwanao mdogo au wa ndugu yako au jirani yako asiyejua hata kujisitiri anayekutegemea wewe Mzazi/Mkubwa umsaidie utamdhulumu kwa kisingizio tu kaacha maungo yake wazi?.

Mbona huko kwenye Mabaa na Klabu wapo wanaovaa uchi si ukashinde huko wakusaidie tamaa zako.
 
Back
Top Bottom