#COVID19 Waziri Gwajima: Kanda ya Ziwa, Kilimanjaro kumeathirika zaidi na Corona

Kwa mujibu wa Dkt. Gwajima, huku kumeathirika zaidi:

“Maeneo ya kanda ya ziwa pamoja na Kilimanjaro yameathirika kwa kiasi kikubwa na ugonjwa huo, na ilihitajika mitungi ya ziada kutokana na eneo la kanda ya ziwa kuathirika zaidi na ugonjwa huo,” alisema Gwajima."

Mwenye masikio na asikie:

“Nataka hapo wananchi watuelewe, tuvae barakoa, tunawe mikono na maji tiririka pia tujiepushe na misongamano isiyo ya lazima. Katika wakati huu hakuna ulazima wa mtu kwenda katika miziki au kupanda katika gari lililojaza watu,” amesisitiza Dk Gwajima."

--------
My take:

Tahadhari zaidi maeneo hayo ikiwamo kupunguza safari zinazoweza kuepukika, kutoka au kwenda maeneo hayo ni jambo la busara zaidi.
Huyu waziri hana Akili sawa sawa.
Taarifa yake imekaa kisiasa badala ya kuakisi uhalisia.

Waziri anapaswa kuja na taarifa yenye takwimu kuhusu wagonjwa na vifo vinavyohusiana na Corona nchi nzima ili tujijue tuko kwenye hali gani.
 
Subiri baada ya siku chache utasikia idadi imepanda zaidi. Mara tutasikia lockdown. Unacheza na new world order:(:(:(:(
 
Tuendako wapi mama, 'no way out' unamaanisha nini, hata mwendazake aliwahi kusema 'never' kwa hiyo haya maneno yanabaki kuwa misemo tu....
Chanjo haitakwepeka wakati wenzetu wakidhibiti huku kwetu ndo itakuwa kuhangaika sasa
 
Chanjo haitakwepeka wakati wenzetu wakidhibiti huku kwetu ndo itakuwa kuhangaika sasa
Haitakwepeka kivipi mama, unamaanisha itatolewa kwa mtutu wa bunduki.......labda utakuwa ni utawala wa mnyama uliotabiriwa kwenye maandiko ya dini, hakuna kula, hakuna kuuza, hakuna kununua hadi uwe na alama ya mnyama......
 
Unajua nini Mkuu, huna haja ya kushupaza shingo, ndita, kuumiza vidole na kuchafua nafsi yako bure kuabuse watu wasiotaka.

Vita ya kupambana na mtu asiye na uelewa si sawa na vita ya kupambana na mtu mwenye uelewa ila hataki tu.

Hapa unapambana na watu wanaelewa fika kuna korona, korona inaua na kuna chanjo ya kuzuia korona ila hawataki chanjo.

Ni kupoteza muda tu kumshawishi mtu ambaye hataki tu!

As long as huhitaji mashabiki wala ufuasi wowote kupata au kutopata chanjo, chanjo ikija kachanje kimyakimya uinjoi security kimyakimya na wasiotaka wasichanje kimyakimya then wafe kwa kishindo kama inavyoendelea.

In short kila mtu ashinde mechi zake.
Duh sawa maana sijashikia mtu fimbo achanje Mimi
 
Haitakwepeka kivipi mama, unamaanisha itatolewa kwa mtutu wa bunduki.......labda utakuwa ni utawala wa mnyama uliotabiriwa kwenye maandiko ya dini, hakuna kula, hakuna kuuza, hakuna kununua hadi uwe na alama ya mnyama......
Itafika tu mahali itakuwa lazima bila hivo huwezi kuwa na access na huduma muhimu za kijamii no need of mtutu wa bunduki siunaona Kuna nchi mpaka uonyeshe kuwa umepatiwa chanjo loh, I think yaliyoandikwa Sasa yanaanza kutimia
 
Itafika tu mahali itakuwa lazima bila hivo huwezi kuwa na access na huduma muhimu za kijamii no need of mtutu wa bunduki siunaona Kuna nchi mpaka uonyeshe kuwa umepatiwa chanjo loh, I think yaliyoandikwa Sasa yanaanza kutimia
Ni kumtegemea Mungu tu, maana ishara nyingi zipo wazi....
 
Mama angu mzazi amefariki kwa gonjwa hili huwa nawashangaa wanao puuza ni hatari zaidi ya hatari anae puuza hajaguswa
Pole sana mkuu. Mimi pia binafsi sijafiwa na ndugu wa karibu lakini nimeona waliofariki na ninaona wanaougua ndio nami nashangaa wanaosema Covid-19 haipo.
 
Huyu waziri hana Akili sawa sawa.
Taarifa yake imekaa kisiasa badala ya kuakisi uhalisia.

Waziri anapaswa kuja na taarifa yenye takwimu kuhusu wagonjwa na vifo vinavyohusiana na Corona nchi nzima ili tujijue tuko kwenye hali gani.

Kuna chawa wa mwendazake wanamshinikiza takwimu zisiwepo.

Wengine hata humu JF wapo wangalipo wanapumua.
 
Lumumba FC naona mashambulizi yao yamelekezwa kwenye hii proganda ili watu wavute mkwanja. Siamini upepo ulivyogeuka ghafla hivi waunga mkono chanjo na wenye kudai kuwa hali ni mbaya ni wengi hivi hali miezi ya nyuma tulikuwa nyuma ya nyungu, maombi, na kupinga barakoa, mabeberu kutokutupenda, chanjo si salama, na mambo yalienda vizuri tu.

Ipo ila si kwa kiwango kinachohibiriwa

Labda kama watega kunguru chambo maharage makavu.

Hakuna Lumumba FC anayeunga mkono vita dhidi ya Corona. Mgawanyo kamili uko hivi:

IMG_20210711_205649_038.jpg


Hatudanganyiki!
 
We matako kwani tanzania na ulaya wapi walikufa zaidi wakati wa magufuli !? Nyinyi ndiyo wale mkiulizwa kilo moja ya pamba na kilo moja ya chuma ipi nzito mnajibu " ya chuma" wazungu walivaa barakoa na madaktari bado walikufa kuliko sisi ,sasa ukiulizwa tufate njia ya mzungu lakini tufe kama wao au tusifuate tusife wewe ungechagua nini?kwa upuuzi uko nao najua ungechagua kufa kama wazungu

Kwani huku kuna aliyekufa wakati Corona haijawahi kuwapo.
 
Niko Mwanza mweiz wa tatu sasa.Hiyo 'taharuki" hata sijaiona na maisha yanendelea kama kawaida tu.
Sijui perpetrators wa haya wanafanya kwa faida ya nani kwakweli
Si ndo nasema sasa, huu upuuzi hatuuoni maisha ni kama kawa? Wanatimiza mashart eeh? Kazi ipo
 
Wewe yawezekana hupo sawasawa. Sifahamu huko Kilimanjaro. Lakini huku Knda ya Ziwa, hali siyo nzuri. Wanaoumwa ni wengi sana ukilinganisha na idadi ndogo waliolazwa. Lakini vifo vinavyotokana na corona vipo.

Kuna rafiki yangu amepoteza ndugu zake wawili Sengerema na mmoja Mwanza.
Mi sikatai kiviiiile ila nawaza corona gani hii kama inapulizwa? Tangu mwezi wa tatu ilienda likizo miezi mitatu, sasa hivi eti imerudi.anyway tusubiri tukio jingine.pole kwa kufiwa ila sidhani kama ni corona
 
Kauli za kukizana za Wanasayansi zimeletelezea Misimamo tofauti ya Wanasiasa, Viongozi na Jamii yote kwa ujumla wake. Mkanganyiko upo kwenye Tiba , je tahadhari pekee yake inajitosheleza au chonjo ni jawabu? Je nchi iingie kwenye lockdown au maisha yaendelee? Kunapokuwa na taharuki na sintofahamu kama hii kila mtu atakuwa na lake kichwani na ndipo kunatakiwa kiongozi wa kutoa neno la matumaini. Corona ipo na haina Tiba. Chanjo siyo tiba bali ni Kinga . Ni changamoto ya maisha
 
Mi sikatai kiviiiile ila nawaza corona gani hii kama inapulizwa? Tangu mwezi wa tatu ilienda likizo miezi mitatu, sasa hivi eti imerudi.anyway tusubiri tukio jingine.pole kwa kufiwa ila sidhani kama ni corona

Kama hujui maana ya mawimbi, jivinjari ufukweni kujifunza yanavyokuja moja baada ya jingine.
 
15 Reactions
Reply
Back
Top Bottom