Waziri Gwajima: Askofu Gwajima ni shemeji yangu, alidai atamfufua Chifupa pia alikutwa na Mrembo akasema mkono wa Baunsa

Kwa nini ninyi msikubali kushitakiwa na kulipa ikiwa mtu atapata madhara? Hiyo ni njia rahisi ya kuthibitisha usalama wa chanjo. Yaani badala ya nyie kuthibitisha usalama, mnageuza kibao kwamba tunaochanjwa ndio tuthibitishe KUWA SI SALAMA! Dunia iko kichwa chini miguu juu. Tunaye Mungu mbinguni wa kututetea.
 
Hapa tena AIBU TU

Umesoma andiko au umekuja kubishana bila kusoma?

Ngoja wenzako waliosoma wapite kwenye comments zako wakudharau btw sikujibu tena

Labda urudi kwenye uzi uje na hoja za.msingi
Andiko lipi?

Huo upuuzi ulioandika, au?

Btw, unahoji ikiwa nimesoma hivi sasa ina maana hukuona hapo mwanzo? Au baada ya kukuonesha clip ya Tapeli Gwajima akijifanya kufufua mtu ndo unahoji ikiwa nimesoma?

Btw, hoja zipi?! Nimekuuliza maswali kadhaa kuhusiana na hicho unachoita hoja... je umeyajibu?
 
Humu umedhihirisha upeo wako mdogo bado unafanya mashambulizi binafs unaacha Hoja we utakuwa binto wa kambo wa Gwajigirl
Very stupid!! Unaona mashambulizi binafsi huku ukishindwa kuona kwamba ni wewe ndo umeanza personal attack?! Badala ya kujibu nilichokuwa nimekuliiza, ukarudia tena na tena kusema eti niruidishe simu? Sio personal attack hiyo?

Iwe bado nasoma au sisomi, inahusiana nini na kile ambacho nilikuwa nimekuuliza?

Kama mimi ni Bint wa kambo wa Gwajima, bila shaka wewe utakuwa yule mliyejirekodi huku akikutafuna; kwahiyo upo hapa kumpigania hawala pornstar mwenzako!!!

Btw, kama mimi nina upeo mdogo, vipi kuhusu yule anayemuamini tapeli anayejifanya kufufua watu? Huyo nae atakuwa na upeo mdogo au mpumbavu kabisa?
 
Waziri wa Afya, Dkt Gwajima leo ameelezea suala askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Askofu Josephat Gwajima kupinga chanjo ya Covid-19 na kudai pamoja na ushemeji walionao haungani na itikadi zake.

Pia ameshangaa wanaomuamini akitolea mfano wa Askofu kudai atamfufua Amina Chifupa kitu ambacho hajatimiza mpaka sasa. Pia amemshangaa kuchukua ubunge ilhali alishasema ni cheo kidogo kwake.

Mwisho Dkt Gwajima amemshangaa askofu Gwajima kukutwa na mrembo na kudai ni mkono wa baunsa.

Waziri Gwajima amesema Askofu amejigeuza msemaji wa sekta ya afya na kulitaka Jeshi la Polisi na Takukuru wamuite atoe maelezo ya chanjo feki alizosema pia atoe ushahidi wa yeye waziri Gwajima na Rais kupewa pesa.
================

Waziri Gwajima: Tumepata walimu waliosomea kwenye mitandao wakajipa vyuo vikuu kama ndugu yangu anayeitwa askofu Gwajima. Yule ni shemeji yangu lakini mitazamo, sera, imani na itikadi tofauti.

Mimi sifungamani na mtu kwasababu eti shemeji yangu. Mimi waziri wa afya, nimeapa kwa viapo vya Amiri Jeshi mkuu na Majeshi yote, wewe ni mume wangu, shemeji yangu, mjomba wangu, ni dada yangu unaleta za kuleta, ninakuambia hiyo hapana na nanyanyua sheria zikushughulikie.

Habari ya kutuambia sisi zile chanjo zimewekwa vitu havieleweki, eti mule ndani zina sumaku. Sasa leteni hizo sumaku muweke hapa, mimi nimeshachanja hapa, muje muweke. Shilingi muweke, balbu muweke maana mimi nimetangaza milioni mbili kwa mtu ambae atachanjwa balbu iwake, nimekaa nazo mpaka nimeshakula laki tano, imebaki milioni moja na nusu.

Mtu ameanzisha kanisa lake, ndo kanisa mibara ya waziri wa afya, yeye ndio msemaji mkuu wa sekta ya afya, anatetea watanzania kuliko mama Samia Suluhu alieapa kwa majeshi yote na sheria zote, yeye ndio mtetezi wa watanzania.

Lakini watanzania sijui huwa mnasahau vipi haya mambo, huyu sio ndio alisema atamfufua Amina Chifupa! Yuko wapi sasa? Huyu si ndio aliewaambia hataki ubunge cheo kidogo akauchukua!

Lakini si huyu aliekutwa na yule mrembo, akasema mkono wa baunsa! Lakini huyu si yeye yule aliekuwa CCM akaenda CHADEMA sasa hivi anasema yuko tayari kurudi, arudi tena CHADEMA!

Hoja zake za kisayansi zimeshajibiwa na wanasayansi wote labda kama hamfatilii, yuko yeye pamoja na wenzake.

Sasa mimi kwa dhamana niliyonayo kama waziri wa afya nimechoka kuvurugiwa wizara, naelekeza Majeshi yote ya Polisi na Takukuru waende wakatumie sheria zao wamuite awaeleze maana kwamba amesema pesa pesa pesa.

Mimi waziri wa Afya na Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania tumepigwa pesa pesa pesa, chanjo ziingie. Sasa yeye si anajua, alikuwa shahidi, alikuwa anatuchungulia, atutajie na alietupa na tulipokelea wapi na yeye alikuwa yuko wapi chini ya sheria ya Takukuru na leo nitasaini tamko langu, La sivyo tutaendelea kuchezeana sana hii nchi.

Amesema chanjo ni feki, chanjo feko zinathibitishwa kisayansi, akatuletee ile batch number ambayo ni feki ni batch ipi na ziko wapi? Kachomwa nani? Tufanye hivi vitu kisheria!

Hatuwezi tukawa na Serikali ambayo mtu anajinyanyua tu anampita na Rais, mara anaitwa Rashid, mara anaitwa Gwajima, mimi sielewi yeye yuko wapi alafu anavuruga vuruga, tunaacha mambo, tunasumbuana kama vile nchi hii haina sheria.

Kwahiyo tunahitaji Gwajima Askofu popote ulipo, nasimama kama waziri wa Afya wa nchi hii, ukatutafutie na kututhibitishia hiyo chanjo ambayo ni fake tuipeleke kwa mkemia mkuu, kama wa Dar es Salaam humuamini twende Nairobi, twende Naijeria, twende kokote tukathibitishe kwamba hizi ni fake.

Na wale waliochanjwa feki ututajie, ututajie twende tukawachukue, tuwapeleke maabara tuchukue damu zao, tuangalie kama anti bodies waliotakiwa kuzalishwa na johnson and johnson wamezalishwa ama hawajazalishwa.

PIA, Soma

=▷ Dkt. Mollel: Askofu Gwajima ataitwa athibitishe kauli zake, akishindwa tutamshughulikia

=▷ Serikali yaagiza Askofu Gwajima kukamatwa ili athibitishe kauli anazozitoa dhidi ya Serikali na viongozi kuhusu chanjo ya UVIKO-19

=▷ IGP Sirro: Hatuna barua ya kumkamata Askofu Gwajima, utaratibu ufuatwe

View attachment 1895773
Wacha dhambi ya uchafuzi wa 28|10|2020 iwatafune.
 
Hiki kimeumana:

1. Kumfufua AC
2. Mkono wa baunsa 😂😂!
3. Ubunge cheo kidogo 😂!

Hivi hamkumbuki wajameni? Na huku nako je?

IMG_20210725_012351_122.jpg

Nani wanakumbuka nini?

Kimeumana!
 
Kwani na sisi tukimuuliza dokta Gwajima si ni yeye alisema tujifukize na kupiga nyungu mpaka akatengeneza video yeye na mumewe kutuhamasisha Watanzania?

Imekuwaje sasa amebadili gear angani? Au kwasababu bwana yule amesha resti in pisi?
Vita yeyote ina short and long strategy!
Wachawi nao wana mbinu hizo hizo za kujaribu zari!
Sioni alipo kosea huyu mama!
 
RC tu anaweza kutoa amri kwa RPC amkamate raia wa mkoa wake, na RC yuko chini sana ya Waziri, yaani mfano Waziri wa TAMISEMI ndio boss wa RCs, RAS, DCs, DAS etc nchi nzima.

So Waziri kama Gwajima ana mamlaka ya kusema naomba vyombo vya dola vimkamate fulani, na suala la barua linafuata na sbb za kumkamata zinawekwa wazi.

So Waziri kusema fulani akamatwe, ana mamlaka hayo, na ndio maana Waziri wa mambo ya ndani anaweza waamrisha IGP na kumwambia fulani mkamateni. Sasa Waziri Gwajima, ana mamlaka kama Waziri wa Mambo ya ndani, na anaweza sema aliyosema, sbb kama kuna mtu anatumia kanisa lake fake kuleta sintofahamu kwa nchi kuichafua Wizara ya Afya, Waziri ana mamlaka ya kusema akamatwe na barua na sbb za kukamatwa zinapelekwa polisi.
Waziri hana hayo mamlaka. Yeye kama waziri, endapo ana taarifa za mtu yeyote aliyetenda jinai anatoa taarifa polisi tu. Polisi watafanya uchunguzi na kuona ni lipi linafaa kutokana na sheria za nchi.

Tusijivike koti la udikteta la enzi za awamu ya utawala wa kidikteta za Jiwe. Ule ulikuwa uvunjivu wa sheria wa wazi. Utawala ule ulilaanika kwa matendo yaliyojaa uvunjivu wa sheria wa wazi kabisa.
 
Umesoma andiko au kama kawaida umekurupuka?? wamesema madhara ni muda gani??

Haya rudi kasome tena halafu uje uniambie umechoma lini
Sijachanja Johnson vaccine.

Pia long term effects za vaccine hakuna anayeweza kuzipredict leo unless hizo effects ni part ya vaccine toka mwanzo na wanaoweza kujua hilo ni watengenezaji wenyewe.

Kuna Watanzania wengi tu nje ya nchi kwa zaidi ya miezi 3 sasa. Kama kungekuwa na matatizo hakuna ambaye angekaa kimya. So far watu ninaowajua waliochanjwa wote wako salama. Ila pia nawafahamu Watanzania waliokufa kwa huu ugonjwa na hawakuwa wamechanjwa.
 
Wacheza sinema wawili wanapoparurana halafu wooote chama cha mbogamboga kazi ipo kwakweli, nadhani tuachane nao by the way ni mambo yao ya kifamilia yanawasumbua ama sivyo ndugu zangu, Nireteeni Gwajimaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa
 
Sijachanja Johnson vaccine.

Pia long term effects za vaccine hakuna anayeweza kuzipredict leo unless hizo effects ni part ya vaccine toka mwanzo na wanaoweza kujua hilo ni watengenezaji wenyewe.

Kuna Watanzania wengi tu nje ya nchi kwa zaidi ya miezi 3 sasa. Kama kungekuwa na matatizo hakuna ambaye angekaa kimya. So far watu ninaowajua waliochanjwa wote wako salama. Ila pia nawafahamu Watanzania waliokufa kwa huu ugonjwa na hawakuwa wamechanjwa.
Basi tulia hapa bongo ipo J.J ambayo tayari ishaanza kulalamikiwa
 
Hoja kubwa alizoibua Waziri ni:
1. Gwajima kuwatuhumu kuwa wamehongwa ambalo ni kosa kubwa sana.
2. Gwajima kusema kuwa chanjo zina vitu ndani yake ambavyo vitawadhuru watanzania huko mbeleni. Hii ina maana kuwa waliohusika na uagizwaji wa chanjo wana nia ya kuwadhuru watanzania.

Waziri kutumia mifano ya uongo wa Gwajima ni kuonyesha kuwa ni pathological liar ambae hastahili kuaminiwa.

Ukweli ni kuwa dola ilitakiwa iwe imemhoji Gwajima zamani kuhusu tuhma hizi. Hivi mpinzani angesema kuwa viongozi wakuu wa serikali wamehongwa ili wakubali chanjo, Ai Jii Pii angengoja barua?

Amandla...
Well said Fund.

Ni kweli kabisa mifano aliyoitumia Doroth kucounter upotoshaji wa shemejie ililenga kuonyesha kuwa Askofu Rashid ni muongo na hapaswi kuaminiwa. Jamaa akadanganya vitu vingi sana ila inaelekea watu hawaoni ...... imagine mpaka alifikia kufake kifo chake halafu akajifufua!!

Vilevile watu lazima wamuelewe Doroth, pamoja na makosa huko nyuma zigo lote kaachiwa yeye kulibeba .... that's not easy!!
 
Back
Top Bottom