#COVID19 Waziri Gwajima amteua Steve Nyerere kuwa Balozi wa Uviko-19

Msanii maarufu nchini na Mwenyekiti wa Jukwaa la Mama Ongea na Mwanao, Steven Mengele 'Steve Nyerere' ameteuliwa kuwa Balozi wa harakati za kupambana na ugonjwa unaosababishwa na virusi vya corona (Uviko-19).

Steve ameteuliwa leo Alhamisi Agosti 12 na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Dorothy Gwajima, jijini Dar es Salaam.

Pamoja na Steve, wengine walioteuliwa ni Mwanaharakati wa Kutetea Haki za Wanawake nchini, Joyce Kiria na Mbunge wa Viti Maalumu, Neema.

Tangu janga la Uviko 19 liibuke tena nchini mwaka huu, Steve ameonyesha kupambana na janga hilo huku akihamasisha Watanzania kupata chanjo ili kujikinga dhidi ya ugonjwa huo hatari duniani.
bila shaka atalipwa na wahisani waliotupatia hizi kinga na sio fedha zetu za ndani
 
CTV yeye ukatibu walipishana

Yeye ni uenyekiti tu

Mdogowake askofu gwajima mkewe waziri walikutana wapi kwenye matibabu mmoja kutibiwa au semina
 
Msanii maarufu nchini na Mwenyekiti wa Jukwaa la Mama Ongea na Mwanao, Steven Mengele 'Steve Nyerere' ameteuliwa kuwa Balozi wa harakati za kupambana na ugonjwa unaosababishwa na virusi vya corona (Uviko-19).

Steve ameteuliwa leo Alhamisi Agosti 12 na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Dorothy Gwajima, jijini Dar es Salaam.

Pamoja na Steve, wengine walioteuliwa ni Mwanaharakati wa Kutetea Haki za Wanawake nchini, Joyce Kiria na Mbunge wa Viti Maalumu, Neema.

Tangu janga la Uviko 19 liibuke tena nchini mwaka huu, Steve ameonyesha kupambana na janga hilo huku akihamasisha Watanzania kupata chanjo ili kujikinga dhidi ya ugonjwa huo hatari duniani.
Mbona sijaona mwenye baracoa hata mmoja? corona na wasani Wapi na Wapi, Gwajima kakosa Madoctor wa kuelimisha watu Kweli?kuishi kwingi ni kuona mengi
 
Tanzania kwa sasa ina viongozi wa kuungaunga hapa ndo nakumbuka Mwl Nyerere kwamba alikuwa timamu kwelikweli kichwani.
 
Back
Top Bottom