Binafsi sipendi namna suala la chanjo ya Corona linavyotaka kugeuka kuwa masuala binafsi na mipasho. Lakini mwisho wake unaweza usiwe mzuri kama hautodhibitiwa.
Kwanza ieleweke tu kuwa hakuna nchi yoyote duniani iliyofanikiwa sana kushawishi wananchi wake 100% wakubali chanjo. Hata nchi za magharibi bado zinapambana kuwashawishi raia wao maana huko kuna hadi maandamano kupinga chanjo. Na badala yake serikali zao zimekuwa zikitumia njia za ushawishi ambapo US tumesikia mpaka ahadi za kupewa Fedha. Na hapa kwetu chanjo ni hiari lakini pia bado watu wengi wana wasiwasi maana yake ni kuwa tutegemee mawazo tofauti. Kumbuka siku zote jambo likikubaliwa na wapinzani wa utawala mara nyingi huwa tinategemea kuwa wafuasi wao watalisapoti kwa wingi lakini Corona imeunganisha viongozi wa CCM na wapinzani ila imewatenga na wafuasi. Yani hata baadhi ya wataalamu wa Afya wamesita kuchanja.
Hivyo tuendelee kutumia ushawishi wetu kama Mama Samia badala ya kutaka kulazimisha na kuwaziba midomo wenye mashaka. Tuwape majibu sahihi, kama huwezi kujibu kistaarabu wape nafasi wengine wajibu badala yako.
Back to the Point.
Mh. Waziri usitegemee kulumbana kwa maneno na Askofu Gwajima alafu utegemee kumshinda. Ni ngumu sana. Utajikuta baadaye unalalamika anakunyanyasa kijinsia na kuwashirikisha kina TAMWA na TAWLA wakusaidie (wakuhurumie).
Kumbuka kuna watu wanakufahamu tangu unazaliwa, unasoma, boyfriends wako before ndoa etc. Hao wataanza kumpa Askofu mafaili yako naye ataanza kuyafunua kama ile issue ya Bashite. Akianza hachoki.
Utajifanya kujitutumua kumjibu na kujikuta unaropoka kama ambavyo umeanza kufanya sasa hivi na hatimaye utapoteza heshima yako mbele ya aliyekuteua hapo utakuwa umekwisha.
Achana na Askofu Gwajima zingatia weledi wa Taaluma na Nafasi yako. Punguza uongeaji kama mtu unprofessional.
Yataletwa mafaili yako ya kweli na uongo ambayo yatakufedhehesha maana naona kundi kubwa la watu nyuma ya Askofu Gwajima kinyume na wewe.
Acha kumjibu atakaa kimya.
Makonda alijaribu kupambana naye akajikuta anapata msongo wa mawazo mara analia kwenye gari, mara anaombewa huku analia kanisani. Yale yote sasahivi hayapo sababu aliyeyasababisha aliamua kutulia.
Sasa wewe ukiwasha kiberiti yeye anakuja na dumu la petroli hapo ndiyo sipataki kabisa.
Asante