Waziri gani alimdhulumu Rais mstaafu Mwinyi vifaa vyake vya ujenzi?

Alimrudishia kwa sababu alishampa somo la kuhadithia milele na hatarudia tena kusumbua watu majumbani kwao wamtunzie mabati kwenye front yard ya Waziri.

Nitarudia mpaka uelewe: Mwenye chake muungwana.

Mtu akikunyanyasa na mali yake, na nyumba yake, hata akufukuze kama mbwa ni yeye ndio muungwana kwa sababu ana kwake, hasumbui mtu. Wewe unaesumbua watu wakutunze au wakuhifadhie mabati majumbani mwao, wewe ndio sio muungwana.

Mwinyi alijua ni yeye amekosa uungwana ndo maana pamoja na yote hayo bado akamwita awe Waziri kwenye serikali yake.
Hujui uungwana na sheria za mtu kutoka katika nyumba ni mwezi moja mpaka mitatu, sasa yeye kajiuzulu hata wiki haijapita , kwa Sababu kateuliwa waziri na kuwa allocated Nyumba akitaka PAPO kwa PAPO, ndio Muungwana akamwachia , roho mbaya ikamsuta , jamaa alivyokuwa Raisi na Bado akamchagua Raisi. Na aliporudisha akaleta kuliko alivyochukua kutokana na bange ya makete
 
Yeye kawadhulumu WaZanzibari mpaka leo likitajwa jina lake wazanzibari wanasema .......kwa sababu alifanya jinai isiyoelezeka. hata hii leo mwanawe ni Raisi wa zanzibar bado Ali Hasan Mwinyi hawezi kutembea au kujitokeza mbele ya hadhara ya WaZanzibar,inahitaji mwanae amuombee msamaha kwa WaZanzibari.
 
Hujui uungwana na sheria za mtu kutoka katika nyumba ni mwezi moja mpaka mitatu, sasa yeye kajiuzulu hata wiki haijapita , kwa Sababu kateuliwa waziri na kuwa allocated Nyumba akitaka PAPO kwa PAPO, ndio Muungwana akamwachia , roho mbaya ikamsuta , jamaa alivyokuwa Raisi na Bado akamchagua Raisi. Na aliporudisha akaleta kuliko alivyochukua kutokana na bange ya makete
Kama alimdhulumu kwa nini alimpa Uwaziri mtu mdhulumati asiye na integrity ?
 
Katika kitabu cha kuelezea maisha yake mstaafu Mwinyi anasema alipojiuzulu uwaziri wa mambo ya ndani Waziri aliyechukua nafasi yake alimtaka ahamishe haraka mizigo yake ili yeye ahamie kwenye nyumba ya serikali aliyokuwa anakaa mzee Mwinyi.

Mzee Mwinyi alishindwa kuhamisha vifaa vyake vya ujenzi wa nyumba yake ya mikocheni kwa mwalimu, yule waziri akamdhulumu.

Pamoja na ubazazi na udhulmati wa waziri huyo lakini mzee Mwinyi alipochaguliwa kuwa Rais wa JMT alimchukua waziri huyo kwenye baraza lake la mawaziri.

Waziri huyo ni nani?

Wahenga Pascal Mayalla, Mohamed Saidi na Mrangi nikumbusheni!

Kazi Iendelee.
Katika kitabu chake "Maisha ya Mzee Rukhsa" ameiongelea habari hiyo na amemtaja Waziri huyo kuwa ni Marehemu Jackson Makweta
 
Kwa hisani kubwa kabisa ya Jamiiforums tarehe 23 Julai 2019
Bofya chanzo : Jinsi Natepe alivyomhenyesha Rais Ali Hassan Mwinyi

Alipojiuzulu uwaziri wa mambo ya ndani ya nchi mwaka 83? kama sijakosea nafasi yake aliteuliwa mzee mmoja kutoka Zanzibar anaitwa mzee Abdallah Said Natepe kushika uwaziri wa mambo ya ndani ya nchi.

Meja Jenerali Abdallah Said Natepe alipoingia tu ofisini alimtaka waziri aliemtangulia kutoka katika nyumba ya waziri ili yeye aweze kukaa hapo kama waziri.

Ilikuwa shida kidogo maana waziri aliyeondoka bado alikuwa anatafuta makazi lakini alitakiwa haraka kutoka na Meja Jenerali Natepe.

Ikampasa mzee Ali Hassan Mwinyi kutoka kwa haraka na siku anatoka pale nyumbani alikuwa amenunua mabati 150 na mifuko ya saruji 100 ya kwake wala sio mali ya serikali.

Mzee Abdallah Said Natepe alimkatalia kuvichukua akidai ni mali ya serekali kweli mzee Ali Hassan Mwinyi akaviacha akaondoka.

Baada ya miezi kadhaa tu mzee Ali Hassan Mwinyi akateuliwa kuwa Rais wa serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar . Mzee Abdallah Natepe wakati anajifikiria jinsi ya kwenda kumpongeza na kumuomba radhi kwa aliyomfanyia kabla ya kufikiria njia mzee Ali Hassan Mwinyi akaletwa bara mwaka 1985 kama Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Hapa sasa Mzee Meja jenerali Abdallah Natepe akajua kazi hana na atatimuliwa haraka iwezekanavyo tena na kutengwa na nyadhifa za serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwakuwa kuna mabaya ya wazi na ya sirini aliyomtendea mzee Ali Hassan Mwinyi.

Mzee Mwinyi baada tu ya kuapishwa kuwa Rais wa JMT wakati anateua baraza la mawaziri akamteua tena Abdallah Said Natepe kuwa waziri pale pale mambo ya ndani.

Siku ya kumuapisha akamwambia mzee Abdallah Natepe sio kwamba nakupenda sana hapana ila napenda kazi yako unavyofanya endelea kufanya kazi.

Siku moja mzee Mwinyi yupo ikulu kapumzika akaona malori yanaingia na akaambiwa mzigo wako huu Mh. Ali Hassan Mwinyi rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania akashtuka mbona sijaagiza kitu mie??

Ndipo akaambiwa umetoka kwa Natepe, mzee Ali Hassan Mwinyi akacheka sana akawaambia wasaidizi wake shusheni mabati 150 na saruji 100 hizo ndio haki yangu zingine mrudishieni tu.

N.B
Habari za ziada kwa hisani ya intaneti

Sunday, September 26, 2010​

MUASISI WA MAPINDUZI ZANZIBAR ABDALLA SAID NATEPE AMEFARIKI DUNIA​


Mmoja wa viongozi 14 wa Mapinduzi matukufu ya Zanzibar,Meja Jenerali Abdallah Said Natepe amefariki dunia jana mchana katika hospitali yajeshi Lugalo mjini Dar es Salaam.

Marehemu Natepe ni miongoni mwa viongozi wa mapinduzi kumbi na mbili waliofariki dunia ambao walifanikisha kufanikiwa kwa mapinduzi ya Januari 12, 1964 yaliyoindoa serikali ya kisultani visiwa vya Zanzibar,

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, kifo hicho kimetokea jana mchana kwenye hospitali hiyo kuu ya Jeshi la Wananchi.
Taarifa hiyo inamnukuu Rais Jakaya Mrisho Kikwete akieleza kushtushwa na kuhuzunishwa na kifo cha mwanamapinduzi huyo na kumtumia salamu za rambirambi katibu mkuu wa CCM akielezea jinsi alivyoguswa na kifo hicho cha Mzee Natepe.

“Kifo kimemchukua mwanamapinduzi, mzalendo na mwanachama wetu mwaminifu katika kipindi ambacho taifa na chama bado kinamhitaji sana. Kifo kimetunyang’anya tunu wakati huu tunaoelekea uchaguzi mkuu; ni huzuni kubwa kwetu; ni majonzi makubwa na hatuna neno kubwa linaloweza kuelezea huzuni hii,” Rais Kikwete anakaririwa kwenye taarifa hiyo.

Rais alipokea taarifa za kifo cha Mzee Natepe jana mchana akiwa Njombe mkoani Iringa ambako yuko kwa ajili ya shughuli za kampeni.

Rais Kikwete pia ametuma salaamu za rambirambi kwa familia, ndugu na jamaa wa Marehemu Natepe.

“Mzee Natepe amekuwa sehemu ya maisha yangu ya kisiasa, kijamii na amenipa malezi na maelekezo mengi nikiwa kama kijana wake na amekuwa moja ya nguzo yangu kubwa katika shughuli zangu za kisiasa na kikazi katika maeneo yote niliyotumikia nchi yangu,” alisema rais na kuelezea kwa masikitiko huzuni aliyonayo na kuwahakikishia kuwa yuko nao katika kipindi hiki kigumu.

“Tunamshukuru mwenyezi Mungu kwa kutupa nafasi ya kuishi na Mzee Natepe na kufanya naye kazi. Tunamuomba Mungu amlaze mzee wetu mahali pema peponi na kumpa pumziko la milele, amina”
Katika kitabu chake "Maisha ya Mzee Rukhsa" ameiongelea habari hiyo na amemtaja Waziri huyo kuwa ni Marehemu Jackson Makweta
 
Na bado hakuwa na kinyongo kwa wale "mashemeji" zake yaani wanafunzi wa shule ya sekondari Forodhani waliokuwa wakipiga kelele za "shemeji, shemeji" kila msafara wake ulipokuwa ukipita maeneo yale kwa vile alijichukulia kibinti kidogo kilichokuwa bado kinasoma shule hiyo miaka hiyo. Huyo binti alikuwa mtoto wa KK aliyekuwa meya wa jiji la Dsm kipindi hicho.
Hebu wacheni kumzushia mzee wa watu!
 
Ukiona mtu anajenga hoja kwa kuegemea umri wake ama kujisifia taaluma yake ujue ni mtupu katika hoja.
Ninyi vibinti vya themanini mshajiona wazee. Kwa wazoefu tuliobahatika kwa neema za Mungu kuziishi awamu zote za Urais nchini hatuna mawaaa tunapowapima viongozi wetu.

Narudia tena pasi kumvunjia heshima Mzee wangu Mzee Ruksa, alikuwa Rais dhaifu na bila shaka yeyote aliyedharaulika kuliko rais yeyote katika historia ya nchi yetu.

Hakuwa mjenga hoja pale alipobanwa hata na vijana wa chuo kikuu hapa Mlimani (Kina Mbatia et al) na wala haku execute any notable actions against maadui zake wala wa nchi yetu.

Udhaifu wake ulionekana si kwa waliokuwa chini yake tu, bali hata wastaafu na hata vijana wa nje ya Chama na wa vyuo vikuu.

Kuwa dhaifu si dhambi, ni sawa na kuwa mfupi ama mrefu. Kamata nakala yako ya MZEE RUKSA ujipe elimu walau juu ya mapungufu ya Mzee wangu Mwinyi na si kupuyanga kujibu hoja kwa hisia na si kwa kutumia ubongo!
Vibinti vya themanini seriously? Kwa taarifa yako tu mwaka 1978 ndiyo nilijiunga na Chuo Kikuu (enzi hiyo ni Dar tu), kwa hivyo tafadhali tuheshimiane kwa hilo na tukubaliane kutafautiana kimawazo na kimtazamo kuhusu Mwinyi kwani siyo dhambi.

Hao akina Mbatia waliokuwa wajuaji sana wameishia wapi? Ni kawaida enzi zile wanafunzi wa Chuo Kikuu kujiona wao ndiyo kila kitu na wengine wote ni wajinga.
 
Alikufa akiwa maskini kabisa na yeye alizulumiwa na wajanja wa njombe huko na uchagani
Hivyo akaiachia familia yake majanga!!! Mungu ameikataza dhulma... na hakika kila mmoja analipwa kwa matendo yake. Ila wengi wanalewa madaraka na kusahau..
 
Vibinti vya themanini seriously? Kwa taarifa yako tu mwaka 1978 ndiyo nilijiunga na Chuo Kikuu (enzi hiyo ni Dar tu), kwa hivyo tafadhali tuheshimiane kwa hilo na tukubaliane kutafautiana kimawazo na kimtazamo kuhusu Mwinyi kwani siyo dhambi.

Hao akina Mbatia waliokuwa wajuaji sana wameishia wapi? Ni kawaida enzi zile wanafunzi wa Chuo Kikuu kujiona wao ndiyo kila kitu na wengine wote ni wajinga.
Hufananii na miaka unayosema!...anyway basi wewe ni kikongwe na mie kijana barobaro wa 2000s
 
Kama alimdhulumu kwa nini alimpa Uwaziri mtu mdhulumati asiye na integrity ?
Aliangalia siasa za Tz Bara, na ku balance uongozi wa kitaifa na si kuangalia kutokuwa muungwana kwakèeeeeee na zaidi ya hapo adhabu stahili kwa mtu asiye muungwana ni kumfanyia uungwana ndio atajifunza vizuri zaidi
 
Mzee ana roho nyeupe ndio maana ameishi miaka mingi, he is 96 today.
Kweli roho nyeupe, lakini jee ameeleza ile hoteli ya white sands na zile nyumba za pale msasani maana mwalimu alichukua mkopo THB kujenga na bado ikamshinda mpaka alipowaachia serikali
 
Back
Top Bottom