Waziri Faustine Ndugulile atunukiwa Tuzo ya umahiri na Wizara ya Afya

💯%💪🇹🇿👍
"Only Stupid People Don't Change Their Minds"..😷😷.. Boutros Boutros-Ghali
Former Secretary-General of the United Nations
 
Wajumbe wa Kamati ya Prof Lyamuya iliyochunguza sakata la Matunda kutest postive kwa COVID-19, ndio hao hao waliopendekeza Chanjo. Wakati wa JPM, kila jumatano asubuhi Chuo Cha Muhimbili walikua Wana host Symposium za Nyungu ( Inhalational therapy) na Kama haitoshi, wakaanzisha na jumba la kujifukiza. Leo hii watu hao hao ndio wanaowaona wenzao wanaopinga na kukataa Chanjo Kama washamba.
Nchi hii tuna safari ndefu Sana.
Mkuu hiyo ni inhalation kweli au ni steam therapy? Au mimi ndiye nachanganya madesa?
 
NDUGULILE ATUNUKIWA TUZO NA WIZARA YA AFYA

Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dkt Faustine Ndugulile (Mb) leo tarehe 23.08.2021 ametunukiwa tuzo na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwa kutambua mchango wake katika kukuza na kuimarisha ya Afya Jamii nchini. Tuzo imetolewa katika mkutano wa wataalam wa elimu ya Afya kwa Umma unaoendelea kwenye ukumbi wa Julius Nyerere, Dar es Salaam.

Naye Dkt Ndugulile kupitia mitandao ya jamii amewashukuru sana Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwa heshima waliyompa na pia kwa kutambua mchango wake kwenye elimu ya afya kwa umma nchini.
Aidha, wametaka wataalamu wa Afya ya Umma kuongeza kasi na wigo wa elimu ya Afya kwa Umma hususan katika kipindi hiki ambacho Tanzania inakabiliwa na ugonjwa wa Covid-19.

View attachment 1905092
haha
 
Aliyekuwa naibu Waziri wa afya katika Serikali ya awamu ya 5 na ambaye kwa sasa ni waziri wa Tehama Dr. Ndugulile ametunukiwa Tuzo ya umahiri na kupromoti afya na wizara ya afya.

Dr. Ndugulile ndiye aliyetoa tahadhari juu ya kupiga nyungu kienyeji hatua iliyopelekea atumbuliwe.

Jana Askofu Gwajima alimpongeza Dr Ndugulile kwa ujasiri aliouonyesha na kusimamia taaluma hadi akapoteza uwaziri.

Mungu ni mwema wakati wote!

Kama wizara imemtunuku cheti maana yake wanakubaliana na maneno ya Askofu Gwajima.

Sent from my SM-A207F using JamiiForums mobile app
 
Aliyekuwa naibu Waziri wa afya katika Serikali ya awamu ya 5 na ambaye kwa sasa ni waziri wa Tehama Dr. Ndugulile ametunukiwa Tuzo ya umahiri na kupromoti afya na wizara ya afya.

Dr. Ndugulile ndiye aliyetoa tahadhari juu ya kupiga nyungu kienyeji hatua iliyopelekea atumbuliwe.

Jana Askofu Gwajima alimpongeza Dr Ndugulile kwa ujasiri aliouonyesha na kusimamia taaluma hadi akapoteza uwaziri.

Mungu ni mwema wakati wote!

Joke of the century
 
which health promotion services... ngoja Magfuli aje mtamueleza mmempa kwa vigezo vipi wakati yeye alimfukuza huko wizarani
Lakini huyo Magufuli ndo alimuwezesha kushinda kura za maoni Kigamboni. Bila Jiwe Bashite the witch angechukuwa jimbo
 
Pamoja na yote hayo mimi nitashangaa sana kama uteuzi wa Dk Dorothy utatenguliwa, ... Dk Dorothy ameimudu wizara ipaswavyo kwenye kipindi cha hii CRISIS!

Kwa kutukana wanaopinga chanjo na kusema ni wahuni wanaolipwa kuipinga. Na naibu wake kuwaita wapumbafu na wajinga. Mtangaze wenyewe kuwa chanjo ni hiari. Wakitokea wanao chagua hiari ya kuto kuchanja ni wahuni wanaolipwa kupinga chanjo, wapumbavu na wajinga. Ila wale wanaochanjwa kwa mashinikizo ndio waerevu na wenye akili. Mungu wa Mbinguni ni wa haki yote siku zote, hatanyamaza atafanya kitu maada anaishi.
 
Back
Top Bottom