Waziri Faustine Ndugulile atunukiwa Tuzo ya umahiri na Wizara ya Afya

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
47,870
2,000
Aliyekuwa naibu Waziri wa afya katika Serikali ya awamu ya 5 na ambaye kwa sasa ni waziri wa Tehama Dr. Ndugulile ametunukiwa Tuzo ya umahiri na kupromoti afya na wizara ya afya.

Dr. Ndugulile ndiye aliyetoa tahadhari juu ya kupiga nyungu kienyeji hatua iliyopelekea atumbuliwe.

Jana Askofu Gwajima alimpongeza Dr Ndugulile kwa ujasiri aliouonyesha na kusimamia taaluma hadi akapoteza uwaziri.

Mungu ni mwema wakati wote!

ndugulile.jpg
 

Ad majorem

JF-Expert Member
Aug 11, 2018
610
1,000
Wizara ya afya hao hao waliojenga kibanda cha kupinga nyungu Muhimbili. Hii nchi ni Alfu lela Ulela.
Wajumbe wa Kamati ya Prof Lyamuya iliyochunguza sakata la Matunda kutest postive kwa COVID-19, ndio hao hao waliopendekeza Chanjo. Wakati wa JPM.

Kila Jumatano asubuhi Chuo Cha Muhimbili walikua Wana host Symposium za Nyungu ( Inhalational therapy) na Kama haitoshi, wakaanzisha na jumba la kujifukiza. Leo hii watu hao hao ndio wanaowaona wenzao wanaopinga na kukataa Chanjo Kama washamba.

Nchi hii tuna safari ndefu Sana.
 

orturoo

JF-Expert Member
Mar 13, 2017
2,297
2,000
Nadhani elimu yetu inatuyumbisha watanzania hatuwezi kukosa dira kwa kiwango hichi ,kuna chanzo mahali
 

JUMA JUMA

JF-Expert Member
Jan 5, 2013
223
500
NDUGULILE ATUNUKIWA TUZO NA WIZARA YA AFYA

Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dkt Faustine Ndugulile (Mb) leo tarehe 23.08.2021 ametunukiwa tuzo na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwa kutambua mchango wake katika kukuza na kuimarisha ya Afya Jamii nchini. Tuzo imetolewa katika mkutano wa wataalam wa elimu ya Afya kwa Umma unaoendelea kwenye ukumbi wa Julius Nyerere, Dar es Salaam.

Naye Dkt Ndugulile kupitia mitandao ya jamii amewashukuru sana Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwa heshima waliyompa na pia kwa kutambua mchango wake kwenye elimu ya afya kwa umma nchini.
Aidha, wametaka wataalamu wa Afya ya Umma kuongeza kasi na wigo wa elimu ya Afya kwa Umma hususan katika kipindi hiki ambacho Tanzania inakabiliwa na ugonjwa wa Covid-19.

IMG-20210823-WA0051.jpg
 

Retired

JF-Expert Member
Jul 22, 2016
29,470
2,000
which health promotion services... ngoja Magfuli aje mtamueleza mmempa kwa vigezo vipi wakati yeye alimfukuza huko wizarani
 

MtanzaniaOG

Senior Member
Apr 7, 2021
151
500
Ninamtetea, yeye alisimamia ethics za profession yake hadi akafukuzwa. Hakuamini kwenye kashwagala na aliamini kwenye science. Huyu wa Singida aliyeolewa kwa akina Gwajima amekula matapishi yake mwenyewe so she is supposed to resign.
 

MtanzaniaOG

Senior Member
Apr 7, 2021
151
500
Ninamtetea, yeye alisimamia ethics za profession yake hadi akafukuzwa. Hakuamini kwenye kashwagala na aliamini kwenye science. Huyu wa Singida aliyeolewa kwa akina Gwajima amekula matapishi yake mwenyewe so she is supposed to resign.
Baada ya kula matapishi yake mwenyewe anaanza kutoka kwenye hoja ya chanjo anamuattack Gwaji Boy personally....Gwaji Girl ni Disgrace to this Nation.
 

Kishimbe wa Kishimbe

JF-Expert Member
Jul 18, 2013
3,753
2,000
Pamoja na yote hayo mimi nitashangaa sana kama uteuzi wa Dk Dorothy utatenguliwa, ... Dk Dorothy ameimudu wizara ipaswavyo kwenye kipindi cha hii CRISIS!
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom