Waziri Emmanuel Nchimbi aombwe radhi kwa lipi katika sakata la uchaguzi wa meya Songea? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Waziri Emmanuel Nchimbi aombwe radhi kwa lipi katika sakata la uchaguzi wa meya Songea?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Ngalikivembu, Sep 25, 2011.

 1. Ngalikivembu

  Ngalikivembu JF-Expert Member

  #1
  Sep 25, 2011
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 1,908
  Likes Received: 355
  Trophy Points: 180
  Baada ya Jumamosi ya 24.9.2011 kuripoti kuhusu Emmanuel Nchimbi kukimbia na sanduku la kura, baada ya mzozo wa kuchakachua kura za umeya, leo amawaita waandishi wa habari na kukanusha kuwa yeye hakufanya kitu kama hicho. Na magazeti ya Tanzania Daima, Mwananchi na Majira yaliyoripoti habari hiyo yameatakiwa kumwomba radhi katika kurasa za mbele za matoleo ya jumatatu kesho 26.9.2011.

  Ukweli ni kwamba kama ilivyoripitiwa na magazeti hayo na pia sisi tulioshuhudia tukio hilo Ijumaa hatuoni sababu ya magazeti hayo kufanya hivyo kwani ni dhahiri Nchimbi alifanya kitu hicho. Labda tuseme Bwana Nchimbi atumie tu cheo chake cha Uwaziri wa habari kutaka kuyalazimisha magazeti hayo kufanya hivyo. Vinginevyo ni habari zilizo na usahihi kabisa wala waandishi hawakutunga. Labda wahariri wa magazeti hayo waamue kuufyata kwa Nchimbi.

  Ndugu zangu vitendo vya kimafya kwenye chaguzi hapa songea Nchimbi ni bingwa wa kufanya hivyo. Uongozi anataka yeye ndio aupange. Na anawaweka watu wasio na kisomo ili awaburuze. Mfano, Ndugu G Ndimbo ndiye aliyesoma na mwenye uelewa sana katika madiwani wote ambaye kipindi cha 2005 hadi 2010 ndiye aliyekuwa meya. Sasa huyu kutokana na usomi wake hawakuwa anaburuzwa. Kuona hivyo Nchimbi akamfanyia zengwe asipite tena. Akampandikiza Darasa la Saba Marehemu Manya. Hata huyu mama Mariamu Dizumba naye ni boya hana elimu. Hivyo anaburuzwa tu na Nchimbi.
  Kwa maoni yangu, magazeti hayo hayana sababu ya kumwomba radhi, habari hiyo ilikuwa sahihi kabisa. Labda tu wamwogope.

  Na hapa nimwombe ndugu Gerson Msigwa kuacha ushabiki wake kwani alitakiwa kuripoti taarifa ile. Sina hakika kama aliripoti kwan Songea hatukuwa na umeme maeneo mengi ya mji huu kwa siku tatu mfululizo.SHivyo sijui kama alitoa hewani habari hiyo.Hapo naomba nifahamishwe.
   
 2. M

  Mthuya JF-Expert Member

  #2
  Sep 25, 2011
  Joined: Jun 9, 2011
  Messages: 1,415
  Likes Received: 65
  Trophy Points: 145
  Ccm wanavituko sana nasikuzao zahesabika
   
 3. Eshacky

  Eshacky JF-Expert Member

  #3
  Sep 25, 2011
  Joined: Apr 26, 2011
  Messages: 966
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 45
  Mawaziri wengi tu wameshapiga mikwara kama hiyo,na hakuna aliyewahi kuomba msamaa.
   
 4. e

  ebrah JF-Expert Member

  #4
  Sep 25, 2011
  Joined: Oct 9, 2010
  Messages: 397
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  huyu kuku mayai anataka tumuumbue zaidi?
  ccm kumejaa scraps!
   
 5. Kijuche

  Kijuche JF-Expert Member

  #5
  Sep 25, 2011
  Joined: Aug 26, 2010
  Messages: 419
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Itakuwa ni jambo la kiungwana endapo kama atakuwa mpole kwa sasa kama ni kweli amehusika katika sakata hilo.
   
 6. F

  FJM JF-Expert Member

  #6
  Sep 25, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Nilimuona Nchimbi TBC1 akinena kuhusu sakata hili na pia akitoa list ya nini haya magazeti yafanye kesho! Lugha au niseme 'tone' aliyotumia haikuwa nzuri hata kidogo kwa public figure. Alikuwa anaongea kwa hasira. Hata hivyo nijuavyo mimi media za Tanzania zinao utaratibu wa mtu kufuata kama hukuridhirika na habari inayokuhusu n.k,. Mlalamikaji anatakiwa awasialine na mhariri wa gazeti lenyewe, then jukwaa la wahiriri na pia Media council halafu kuna nafasi ya kufanya uchunguzi huru ili kubaini kiini cha tatizo. Sina hakika kama Nchimbi keshafanya lolote kati ya haya niliyotaja na itakuwa ajabu sana kwa waziri mwenye dhamana ya habari kwenda kinyume na taratibu ambazo media stakeholders (yeye Nchimbi akiwepo) wamejiwekea.

  Tatizo jingine ninaloona hapa ni kwa Nchimbi kutaka kujigeuza judge & jury! Anatoa hukumu kwa hivi vyombo vya habari kwa sababu wameandika habari za uwongo au tu hakupendezwa na habari yenyewe? Kama ni za uwongo uchunguzi kafanya nani na lini? na report ya uchunguzi iko wapi na inasemaje? Pamoja na matatizo yake lakini bado nchi hii inaendeshwa kwa sheria na Nchimbi kama public figure ni vizuri aondokane harafu ya kutozingatia sheria na taratibu za ki-uongozi katika kutekeleza majukumu yake. Bado ni waziri kijana kwa hiyo avute pumzi kwenye hili kabla ya kuchukuwa hatua vingenevyo anaweza kuumbuka. Hivi ikitokea mtu alimnasa kwenye simu ya mchina akibeba sanduku itakuwaje? Just think careful Nchimbi.
   
 7. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #7
  Sep 26, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Kule Songea anayofanya ni yaleyale ya Babake alivyofanya alipokuwa mkuu wa wilaya na mbunge, na mtoto wake karithi, kwa haya ndugu zanguni usitegemee kuchuma zabibu shamba ndani ya mzabibu mwitu.
   
 8. Mwanaukweli

  Mwanaukweli JF-Expert Member

  #8
  Sep 26, 2011
  Joined: May 18, 2007
  Messages: 4,451
  Likes Received: 288
  Trophy Points: 180

  Nchimbi ana arrogance ya kiwango cha juu sana.
   
 9. CHIETH

  CHIETH Senior Member

  #9
  Sep 26, 2011
  Joined: Aug 15, 2011
  Messages: 179
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Bw Nchimbi nakuomba kama ulijifunza uongo ilikuwa ni wakati wa chama kimoja na wakati ambapo vyombo vya habari vilikuwa chache. Ukiendelea kututisha sisi vyombo vya habari tutakuita waziri X.
  Uombwe radhi? Acha mambo ya kale ndugu yangu ninakushauri utulie yataisha.
   
 10. h

  hahoyaya Member

  #10
  Sep 26, 2011
  Joined: Apr 24, 2011
  Messages: 89
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Huyu nchimbi yuko usingizini tena wa blanket,hii generation ni nyingine kabisa ni kizazi chenye upeo mkubwa wa uelewa,so asitegemee kuwaburuza hawa hawakupitia chipukizi na kukaririshwa kuwa ccm ni nambari wani.Mind u hawa ni kizazi cha wasomi,hv kwanini waafrika hatujifunzi?Handle with care vinginevyo wataondoka na ww,anyway ni ushauri tu!
   
 11. mmbangifingi

  mmbangifingi JF-Expert Member

  #11
  Sep 26, 2011
  Joined: Mar 9, 2011
  Messages: 2,855
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Kama magazeti hayo wanazo more evidences za tukio zima wamlipue tu jumla aumbuke na kuacha ubabe. Hata mie niliwahi kusikia jamaa anajiona ka Mungu mtu Manispaa ya Songea pale. sitashangaa hata Gerson Msigwa ikiwa hakuripoti inshu hii
   
 12. kapotolo

  kapotolo JF-Expert Member

  #12
  Sep 26, 2011
  Joined: Sep 19, 2010
  Messages: 3,727
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
 13. Ngalikivembu

  Ngalikivembu JF-Expert Member

  #13
  Sep 26, 2011
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 1,908
  Likes Received: 355
  Trophy Points: 180
  Kwa namna wanavyomwogopa Nchimbi hapa Songea waandishi wengi hawaandiki majina yao. Wanapenda kujiita 'Na Mwandishi Wetu'.Amekuwa kama Mungu Mtu vile. Lakini pia kuna mushkeli katika waandishi waliopo hapa Songea. Wengine ni wabeba bahasha za kaki za Nchimbi hivyo utabaini kuwa magazeti yaliyoandika ni matatu tu.Wengine wanavyata mkia.Gerson hutangaza kazi za maslahi tu na zinazopamba CCM na serikali yake.Nasema hawana haja ya kuomba radhi.Taarifa zilem za yeye kukimbia na sanduku la kura zilienea jioni ile haraka sana hata kabla ya kuziona magazetini.Ningeshangaa sana kama nisingeona taarifa zile.
   
 14. Kitila Mkumbo

  Kitila Mkumbo Verified User

  #14
  Sep 26, 2011
  Joined: Feb 25, 2006
  Messages: 3,347
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  Simple, waweke picha inayomuonyesha akiondoka na masanduku.
   
 15. Mzee wa Rula

  Mzee wa Rula JF-Expert Member

  #15
  Sep 26, 2011
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 8,177
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  Nchimbi nae !!!!!!!! Anataka watu waje waje wamuumbue live kisha asiwe na pa kutokea!!!! Ngoja tuone sinema hii isiyo na malipo maana kitakaacho amua tu ni suala la muda.
   
 16. Ndallo

  Ndallo JF-Expert Member

  #16
  Sep 26, 2011
  Joined: Oct 1, 2010
  Messages: 7,134
  Likes Received: 1,089
  Trophy Points: 280
  Leo ni jumatatu ngoja nikayatafute hayo magazeti nione kama yamemuomba radhi! Nitarejea.
   
 17. The Dude

  The Dude JF-Expert Member

  #17
  Sep 26, 2011
  Joined: Sep 14, 2011
  Messages: 981
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Vipi wamemuomba radhi ukurasa wa mbele kama anavodai?Yeyote alosoma majira,tanzania daima na mwananchi atujuze tafadhali
   
 18. T

  Tanganyika jeki JF-Expert Member

  #18
  Sep 26, 2011
  Joined: Jun 12, 2011
  Messages: 243
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Jamani eheee! Labda hakukimbia nalo, alitmbea nalo. Taratiiiibu!! na kwenda lihifadhi
   
 19. mashikolomageni

  mashikolomageni JF-Expert Member

  #19
  Sep 26, 2011
  Joined: Jan 5, 2010
  Messages: 1,565
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  100% ur right!!!!!!!!
   
 20. Z

  Zawadi Ngoda JF-Expert Member

  #20
  Sep 26, 2011
  Joined: Aug 13, 2009
  Messages: 2,290
  Likes Received: 175
  Trophy Points: 160
  Tuwekeeni video ili tujue kama alikimbia nalo au alitembea nalo. Wote mliokuwa na simu hamkudiriki kuchukua hata sekunde 30 tu! Ngoja nitembelee YouTube, pengine ziko huko. Nisipozikuta nitajua huo ni umbea tupu.

  No! Nimekumbukua, nitatembelea WikiLeaks vile vile huenda Julie Assange naye kamchora Nchimbi.
   
Loading...