Sandinistas
JF-Expert Member
- Jul 5, 2013
- 2,609
- 1,771
Kwa haraka ambayo Waziri Kigwangala alitoa ile kauli ya kuondoa OBC ilikuwa wazi kuwa waziri alikurupuka. OBC ni mboni ya jicho la ccm na serikali yake. Ili kufanya uamuzi wowote unaoweza kuathiri OBC sharti kwanza ngazi za juu kabisa katika siasa na uongozi wa nchi ziridhia. Waziri alitoa kauli yake muda mfupi tu baada ya kuteuliwa hivyo hakuwa na muda wa kuifahamu kampuni yenyewe wala msimamo rasmi wa serikali yake kuhusu kampuni hiyo.