Waziri Dr. Kalemani anapaswa kutoa taarifa kwa umma kuhusu shambulizi la Mh.Lissu. CCTV camera ilirekodi tukio?

Mimi nashangaa WAANDISHI WA HABARI hawajamtafuta Dr.Kalemani na kujua his side of the story.

Cc Pascal Mayalla, maggid, Manyerere Jackton
Mkuu Joka Kuu, mambo ya contents za CCTV ya Kalemani ni personal private matters usitake kuibadili kugeuka public matter. It depends ni ujirani wa aina gani, the magnitude ya hizo CCTV na beaming ya hizo camera, kuna camera zinaweza kuonyesha mtaa mzima, kuna camera zinaweza kutelekezwa kwa jirani, na kuna ujirani hata kuisikia mayowe kwa jirani, wewe unajifungia ndani kwako kwa vile hayakuhusu, kama hakuna yoyote aliyesikia hata mlio tuu wa risasi, what are the chances za kujua contents za CCTV za jirani?.

Shambulizi la Lissu ni criminal offence inayohitaji criminal investigation na sio issue inayohitaji investigative journalism.

Nikakueleze kama kuna mtu wa kuhojiwa, mtu wa kwanza ni Lissu na dereva wake, wengine watafuatia.

Kiukweli kwa issue hii sililaumu jeshi letu la polisi kwa kutomuhoji mtu yoyote mpaka sasa, kwa sababu ambazo nimeisha zieleza hapa
Shambulio la Lissu: Wajue Wasiojulikana Watakaojulikana na 'Wasiojulikana' Ambao Kamwe, Hawatajulikana!.

Paskali
 
..Thanks.

..Majibu yanaweza kuwa kati ya hayo uliyoeleza.

..sasa kwanini hakuna mhusika toka chombo chochote kile anayejitokeza na kutoa majibu?

..Na waandishi wa habari mngekuwa wajanja mngeuliza maswali ya kina kuhusu tukio hili.
Ujanja huo pasco hana...

ujanja alionao ni kujikombakomba na kulamba miguu ya mkanda wa ziwa mwenzie huenda akaonekana akalambishwa matamu ya nchi...

huyu naye ni mchumia tumbo katika level ya chini kidogo ya jerry muro.
 
Kwa vile kukitokea tukio, watu wa kwanza kabisa kuulizwa maswali ni the witnesses, hivyo tunamsubiri Lissu na dereva wake waje, ndipo sisi waandishi makini, tuanze kuuliza maswali.

Paskali
Huna umakini huo kaka...sahivi unachuana na jerry muro kulamba miguu.

umejiondolea sifa yako uliyoijenga kwa makumi ya miaka..wewe sio pasco mayala yule wa KITIMOTO...sio wewe yule mwandishi wa habari chokonozi..

Pasco huyu wa sasa AMEUFYATA...huyu wa sasa uso umempwelepweta umejaa soni...umejiinamia kama mwana mkiwa...pasco wa sasa umepoteza dira na huna nyendo wala mwelekeo.

Tulia jitafakari na amua kurudi katika pasco yule wa KITIMOTO au kuongeza bidii kumfikia na kumpita jerry muro wa sasa.

Nisamehe brother kwa kuamua kukuambia ukweli japo mchungu maana naamini nitakuwa nimekusaidia kwa kiasi fulani.
 
..Iakini Dr.Kalemani wanafahamiana na TL toka Udsm kitivo cha Sheria.

..kuna suala la UBINADAMU hapa.
Pia Dr Kalemani ni mrithi wa mzee jimboni na ndiye aliyempa nafasi aliyonayo na anaweza kumtoa pia akabaki kama Nape tuu
 
Ujanja huo pasco hana...

ujanja alionao ni kujikombakomba na kulamba miguu ya mkanda wa ziwa mwenzie huenda akaonekana akalambishwa matamu ya nchi...

huyu naye ni mchumia tumbo katika level ya chini kidogo ya jerry muro.
Huna umakini huo kaka...sahivi unachuana na jerry muro kulamba miguu.

umejiondolea sifa yako uliyoijenga kwa makumi ya miaka..wewe sio pasco mayala yule wa KITIMOTO...sio wewe yule mwandishi wa habari chokonozi..

Pasco huyu wa sasa AMEUFYATA...huyu wa sasa uso umempwelepweta umejaa soni...umejiinamia kama mwana mkiwa...pasco wa sasa umepoteza dira na huna nyendo wala mwelekeo.

Tulia jitafakari na amua kurudi katika pasco yule wa KITIMOTO au kuongeza bidii kumfikia na kumpita jerry muro wa sasa.

Nisamehe brother kwa kuamua kukuambia ukweli japo mchungu maana naamini nitakuwa nimekusaidia kwa kiasi fulani.
Mkuu Mkojo wa bangi, amini usiamini, nafurahi sana unaponifananisha mimi na Jerry Muro, kwa sababu hiyo ndio level yako ya uelewa wa maandishi yangu, na hauko peke yako unayenidhania mimi ni kujipendekeza na full kujikombakomba type of Jerry, Le Mutuz and the like!. Pole!. In reality mimi na hawa jamaa ni mbingu na ardhi, ila kwa vile kwenye jamii yetu vilaza ni wengi zaidi kuliko ma GT, kuna mengi ya maandishi yangu yako coded ndani ya fasihi ya level fulani, ukiwa kilaza unadhani najikomba kutafuta uteuzi.

Mimi ni Pasco yule yule wa Kiti Moto, na bado niko vile vile kama juzi, jana, leo na hata milele, ila naandika kwa ajili ya wachache tuu wenye level ya uelewa wa mada zangu, mliobaki endeleeni kunidhania najipendekeza na kujikombakomba kutafuta uteuzi!.

Most welcome mukojo ya bangi.

Paskali
 
Ulinzi unalipiwa na nani? Kama ni wa serkali utakuwa na masharti yake, hautawajibika kwa majirani. Hivi kwa nini CHADEMA hawakumpa ulinzi Mnadhimu wake Mkuu? Au walimpa hela akazila? Umemtaka Waziri Kalimani "ajitolee": hii inategemea mahusiano. Je, walikuwa wanaamkuana asubuhi? Wanatembeleana Iddi? Watoto wanacheza goroli pamoja? Lissu kamtukana Kalimani matusi ya nguoni mara nyingi tu kuwa ni jambazi wa mikataba mibovu, kapewa kazi tu na Rais mtoto wa Dada lakini hafai, nk. Na Spika Tulia anatukanwa hivyo hivyo. Je ni sawa mtu kama huyu kujitolea? Mwisho kabisa hatujajua wahusika ni nani hasa? Dereva yuko wapi? Au ni inside job ndani ya CHADEMA?Mlinzi kafichwa wapi na na nani na aliponaje? Au ni majambazi wa kawaida au wamenunuliwa na maadui za Lissu kwenye kesi za mahakama? Au wachimba madini waliopunjwa?
we subiri mtu anayemchukua mkeo au adui yako yeyote afie tu karibu na eneo lako uone kama hutotoa maelezo tena ya kina hata kama hu husiki!
 
..Waziri wa Nishati Dr.Kalemani ni jirani na Mh.Tundu Lissu ktk makazi ya viongozi Area D Dodoma ambako shambulizi lilitokea.

..Watu mbalimbali wameeleza kwamba Dr.Kalemani ameweka CCTV cameras nyumbani kwake. Na cameras hizo zimeelekezwa eneo aliposhambuliwa Mh.Lissu.

..Sasa ingependeza kama Dr.Kalemani angejitokeza mbele ya umma na kueleza kilichomo ktk rekodi za camera.

..Lakini pia kuna ulazima wa camera hizo kukaguliwa na chombo huru ili kuondoa mashaka yoyote yanayoweza kutokea kutokana na maelezo ya Dr.Kalemani.

..Majirani wengine nao wanapaswa kujitokeza na kueleza waliona na kusikia nini kabla, siku ya tukio, na baada ya tukio.

..Baadhi ya majirani ni Dr.Tulia Ackson, Dr.Haji Mponda, na Katibu Mkuu wa wizara ambaye jina lake Mh.Lissu alishindwa kulikumbuka.

Cc MISULI, BAK

IKO SIKU UPELELEZI HUU UTAFANYIKA TU NA UKWELI KUJULIKANA HATA KAMA NI BAADA YA KARNE NA SISI WOTE TUKIWA HATUPO,HUO NDIO UKWELI.
 
..ama wameshindwa, au hawana nia ya kuchunguza.

..TL na dereva wako Nairobi. Sasa ni nini kinawakwaza polisi wasiende kuwahoji?

..Zaidi ni CCTV camera ya Dr.Kalemani. Kama ilikuwa ikifanya kazi basi kuna uwezekano mkubwa wauaji wanaweza kutambulika.

..Kwa hiyo tusijifunge kwenye imani kwamba bila dereva uchunguzi hauwezi kufanyika.
Jamani naomba kuwauliza polisi wetu; dereva au Lissu au wote wangekufa uchunguzi usingefanyika na kuwapata wauaji? Mnatuchosha kila siku dereva, dereva. Please be more serious.

Kama ni hivyo jeshi letu linatumia mbinu za kizamani sana kuukabili uhalifu
 
Mambo mengine ni kutumia common sense tu.

Kifupi ni kwamba police hawafanyi uchunguzi wowote wana sogeza muda tu, sema kitendo cha Lisu kupona ndio kinawatia hasira.
 
Nyie mnazunguuuka waliompiga risasi TL ni serikali ndio maana pesa ya matibabu bunge halitaki kutoa
 
Kuna CCTV Camera ambazo tumeambiwa zineondolewa kimya kimya, hatuchelewi kuambiwa huyo aliyezitoa hajulikani, sawa hilo sio tatizo, lakini kwa uelewa wangu hizi CCTV camera huwa zinarekodi na kutuma video kwenye control box (NVR) kwa hiyo hata mtu akiichomoa camera kwa nje ukiingia kwenye hiyo NVR utapata hizo video zote. Huu ushahidi upo lakini ni kama vile watu wanakwepa kuutumia.
 
Ndiyo maana familia ya Tundu Lissu na chama cha Chadema wanasisitiza kuwa ni muhimu wakaja wapelelezi toka nje.

Sasa kama CCM wanadai ni Chadema wamefanya lile tukio na Chadema wanasema ni vyombo vya serikali vilivyotekeleza suala lile.

Kukata mzizi wa fitina ni kuleta wapelelezi toka nje.

Sasa kwa nini serikali ya awamu ya 5 inashikwa na kigugumizi kuwaleta wachunguzi toka nje??

Siyo kuwa wanavipuuza vyombo vya ndani.....

Ila vyombo vya ndani vinafanya kazi ya maelekezo toka juu.....

Kuna "killing squad" ndani ya vyombo vya usalama vya Taifa ambavyo havitakiwi kuhojiwa!
Ni Aibu kwa serekali yoyote ile duniani kukubali hayo, ila pakiwa na tatizo kubwa la kisiasa na mfarakano wa kikabila.

KWA mfano Kenya alipouawa Dr Ouko, ilibidi wafanye hivyo , kwa sababu ya matatizo ya kikabila, Wajaluo walimpoteza Tom Mboya hivyo hivyo, na pia wakati huo Raisi Moi atokeae kabila la Wakalenjin, wahasimu wake walikua wakikuyu amabao walikuwa wanachochea ili machafuko yatokee.

Mh! Makubwa haya! Ahsante sana JokaKuu kunitag kwenye huu uzi. Naona ndiyo sababu Serikali hii dhalimu ikawa mbogo sana kwenye kuruhusu FBI au Scotland Yard kuingia nchini kufanya uchunguzi.

Mwenyezi Mungu kweli hamtupi mja wake.
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Mjadala wa Tundu Lissu ulipigwa marufuku,kuna shida gani kutii sheria bila shurutiii..???
Imani yangu inasema..."Kwa hakika kila nafsi ITAONJA umauti"Hapo kuna hekima kubwa saana,baada ya kuonja tutarudishiwa uhai na kuwa katika barza ya uhai wa milele,huko sasa ndipo kwenye kimbembe.
 
..kwasababu cctv camera ilikuwa installed ktk nyumba ya Dr.Kalemani.

..Kwa maana hiyo ni mali yake na yeye ndiye mwenye mamlaka ya kujua kilichomo ktk kumbukumbu za camera hizo.

..Hebu jiulize ingekuwa wewe ndiyo Dr.Kalemani, je baada ya tukio kama lile kutokea nje ya nyumba yako hutakuwa na interest ya kwenda kuangalia kama camera zako zilirekodi?

..Sasa ni vizuri kufahamu Dr.Kalemani aliona nini, na alimtaarifu nani. Na alitoa taarifa hizo lini.
Kwani unafikiri uwaziri kamili Wa nishati ni malipo ya kitu gani?
 
Mambo mengine ni kutumia common sense tu.

Kifupi ni kwamba police hawafanyi uchunguzi wowote wana sogeza muda tu, sema kitendo cha Lisu kupona ndio kinawatia hasira.

Jibu la uhakika hili. Mtu yeyote anayejua nchi inaendaje hivi leo hawezi kupoteza muda kutafuta majibu toka serikalini kwa matukio ya aina hii.
 
Mh! Makubwa haya! Ahsante sana JokaKuu kunitag kwenye huu uzi. Naona ndiyo sababu Serikali hii dhalimu ikawa mbogo sana kwenye kuruhusu FBI au Scotland Yard kuingia nchini kufanya uchunguzi.

Mwenyezi Mungu kweli hamtupi mja wake.
Najaribu kuwaza, paapu cdm ya twaa madaraka, vurugu za tokea maafa makubwa yatokea , watu waanza kuzusha kuwa serikali ya cdm ndiyo imesababisha maafa. cdm kwa kuwa wanapenda wachunguzi wa viwango wanawaalika FBI na Scotland Yard kufanya uchunguzi. Likitokea lisiloeleweka wanawaita wachunguzi kutoka nje. Na wakija hao wachunguzi wanachukua coordinates zetu na kuweka 'nano-quantum devices' kurahisisha utengenezaji wa blackmail strategies zao kwa viongozi wetu. Kwa sababu cdm inafurahia kutumia vitu vya kigeni bado ya kuthamini vya kwetu wenyewe, inaendelea kuwaalika kila mara... Inafika siku ya siku hao mabosi wa wachunguzi wanataka kutununua... cdm sijui atafanyaje? Je. cdm atajitoa ufahamu kama wahuni wa Benghaz wanavyowafanya Waafrika wa Libya na mataifa jirani?! Ama cdm watasema 'bora' kuuzwa huko.... Nawaza!!!
====
Ukiona mtu anadharau ' apparatuses ' za nchini mwake na kusifia za nje ya nchi yake ujue huyo hafai kuwa raia wa nchi hiyo bali anahitaji counselling ya hali ya juu ili afae kuwa raia wa nchi hiyo.
BAK sijakamilisha uchunguzi wangu kujua kama wewe pia una hitaji counselling ya hali ya juu.
 
Huna umakini huo kaka...sahivi unachuana na jerry muro kulamba miguu.

umejiondolea sifa yako uliyoijenga kwa makumi ya miaka..wewe sio pasco mayala yule wa KITIMOTO...sio wewe yule mwandishi wa habari chokonozi..

Pasco huyu wa sasa AMEUFYATA...huyu wa sasa uso umempwelepweta umejaa soni...umejiinamia kama mwana mkiwa...pasco wa sasa umepoteza dira na huna nyendo wala mwelekeo.

Tulia jitafakari na amua kurudi katika pasco yule wa KITIMOTO au kuongeza bidii kumfikia na kumpita jerry muro wa sasa.

Nisamehe brother kwa kuamua kukuambia ukweli japo mchungu maana naamini nitakuwa nimekusaidia kwa kiasi fulani.
Tangu Paskali ametoka ktk ziara ya mikoani yuko vizuri sana naona ziara imemkutanisha na ambayo alikuwa hategemei. Hongera Paskali umerudi vizuri
 
Shambulizi la Lissu ni criminal offence inayohitaji criminal investigation na sio issue inayohitaji investigative journalism.
Baadhi ya Mengine nakubaliana na wewe. Lakini mojawapo ya hili hapo juu ninachakusema.
Hapa nakubishia kidogo nikirejea kazi za Mohamed Ali wa Jicho Pevu. Hivi kazi za Mohamed mfano" Pawanja la Mihadarati " na "Ghururi la Saitoti " hazikufaa kuwa investigative journalism?
 
Mohamed Amin na jicho pevu ni habari nyingine, sisi hapa bongo hatuna waandishi wa level ile, na hata tukiwa nao, individual journalists wenye uwezo wa kufanya IJ kama za Mohammed Amin, but atafanya with what capacity, na akiishafanya atarusha media ipi with what independence?.

Paskali
 
Mshawishi alwatan Mboye amrudishe yule dereva aseme ukweli, amemfungia hotelini anachangisha fedha kutunza Lisu na dereva kumbe anapiga dili
Mboye ndiye nani? Unafahamu kazi ya polisi kwenye makosa ya jinai, au unapelekwa pelekwa tu kwa sababu wanajua wajinga mko wengi?
 
Back
Top Bottom