Kurzweil
JF-Expert Member
- May 25, 2011
- 6,622
- 8,410
Waziri wa Kilimo Mifugo na Uvuvi Mhe. Dr. Charles John Tizeba amewasimamisha kazi Watendaji Wakuu mbali mbali wa wizara yake pamoja na mambo mengine kwa kushindwa kuwajibika na kutumia madaraka yao ipasavyo ili kupisha uchunguzi wa tuhuma zinazowakabili.
Akizungumza na Waandishi wa Habari katika ukumbi wa wizara amesema amefanya mabadiliko kwa Kaimu Mkurugenzi wa Usalama wa Chakula Bw. Ombeni Lemweli kwa madai kuwa ametumia vibaya madaraka yake kwa kuweza kutoa vibali vya kusafirisha mazao nje ya nchi pasipokufanya tathmini ya kutosha juu usalama wa chakula hapa nchini.
Nafasi ya Bw. Lemweli imechukuliwa na MKurugenzi Mkuu wa Bodi ya Mazao Mchanganyiko Bw. Elimpaa Kiranga na nafasi ya Bw. Kiranga kwenye Bodi ya Mazao Mchanganyiko itashikwa na Bw. John Maige.
Pia Mhe. Dr. Tizeba amewasimamisha kazi Watendaji Wakuu wa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula ( NFRA) , katika zoezi hilo limewakumba Mtendaji Mkuu wa NFRA Bw. Charles Warwa, Mkurugenzi wa Huduma na Uendeshaji Bi. Anna Ngoo, Mkurugenzi wa Masoko Bw. Mikalu Mapunda na Meneja wa NFRA Songea Bw. Jeremiah Mtafya.
Idara kuu ya Uvuvi nayo imeguswa na mabadiliko haya ambapo Mhe. Dkt. Tizeba amemteua Bw. Hosea Gonza Mbilinyi kukaimu nafasi ya Mkurugenzi Mkuu wa Uvuvi wa Bahari Kuu kuchukua nafasi ya Bw. Rashidi Hoza ambaye pia utendaji wake si wa ufanisi.
Mhe. Dkt. Tizeba pia hakuishia hapo ametengua nafasi ya Mkurugenzi wa Utafiti na Maendeleo Kanda ya Nyanda za Juu Kusini yenye makao yake Uyole Jijini Mbeya Dkt. Zakaria Malley ambaye atahamishiwa Kituo cha Utafiti cha Selian kuendeleza shughuli zake za kawaida za utafiti, nafasi yake itachukuliwa na Dkt. Tulole Lugendo Buchayeki wa kituo cha Ilonga.
Vituo vya Utafiti vya Naliendele na Ilonga navyo vinaonekana kuwa utendaji wake si mzuri kwa mujibu wa Mhe. Dkt. Tizeba.
Kutokana na mbadiliko hayo Mhe. Dkt. Tizeba amemwagiza Katibu Mkuu kuyafanyia kazi marekebisho hayo haraka iwezekanavyo kuanzia leo.