#COVID19 Waziri Dorothy Gwajima: "Mume wangu ametest mitambo, kakuta Niko fiti"

SIyo vitu vya kawaida kuongelea mambo kama hayo kwenye public

Masuala ya Afya na tiba huwa hayana "AIBU"----- "mficha maradhi kilio humuumbua" wahenga walisema isitoshe mficha mbususu hazai wahenga wakamalizia.🤣
 
Sasa mwingine akisema ni effects za chanjo ndo maana kauli na tabia zake hazieleweki - atakataa???

Maana her behaviour is not of a rational human being ni kama speaking zombie....

Ajifunze 'emotional intelligence'

Huyo akiwa kama Dr kakosea nini???
 
WAZIRI wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, nchini Tanzania Dk. Dorothy Gwajima amewaacha na hamaki wakazi wa jiji la Mwanza mara baada ya kusema, baada ya yeye kuchanja chanjo ya UVIKO-19, mume wake ametesti ‘mitambo’ kwake na kukuta yupo ‘fiti’ kama mwanamke.

Ametoa kauli hivyo jana jijini Mwanza alipokagua jengo la Mama na Mtoto katika Hospitali ya Sekou Toure ya Jijini Mwanza. Amesema chanjo haiathiri kitu chochote katika mwili ndio maana yeye yupo vizuri baada ya kuchanjwa chanjo hiyo na kuhimiza watu kwenda kuchanjwa, “Hakuna aliyechanjwa akageuka kuwa zombi.”

Mtu mwenye dhamana ya Waziri bila shaka anatakiwa kuwa makini kwenye matamko mbalimbali, kutoa kauli kama hii ya mambo ya faragha kati yake na mume wake, hata kama ni kwa kuhamasisha watu wakachanjwe chanjo ya COVID 19 kauli ya namna hii siyo nzuri amemwaibisha mume wake na amejiaabisha mwenyewe kwa hadhi aliyonayo.

Kauli hiyo haiwezi kuleta ushawishi wowote wa kuwafanya watu waitikie kupata chanjo hiyo, nafikiri ni vyema kamati za maadili na viongozi wastaafu kukaa na viongozi wa namna hii na kuwaonya kutokutumia kauli za aina hii maana hazifai.

Hivi kama mume wake angetest akakuta kuna mabadiliko ikatokea tafrani kati yao angeutangazia umma wa wa Tanzania jambo hilo?
Au kulikuwa na ulazima gani wa kutamka maneno ya aina hiyo?
Ni hayo tu, karibuni wadau na ninyi mtoe maoni yenu juu ya kauli hii ya mh waziri.
Hata washauriwe na kufundwa na malaika hawawezi badilika, wote wote hawana namna nyingine ya kushawishi umma ktk mambo yote wakaeleweka achilia mbali la UVICO 19 NA CHANJO yake. Viongozi hawa na taasisi yao ya kisiasa walishapoteza kibali na ushawishi mbele za watu utaishia kuropoka kutapatapa maana hawajui watu wanataka nini ili wawaelewe. Watu wameerevuka wanaelewa ukanjanja unaofanyika nchini ktk mambo yote
 
Kuna baadhi ya nati zimelegea kwa huyu mama, huyu ndo anawapa backup wajinga wanaopinga chanjo
 
Walimtest akiwa kwenye popo kanyea mbingu,mbuzi kagoma kwenda au cha mende?? Atuambie sasa
 
WAZIRI wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Dorothy Gwajima amesema baada ya kuchanja chanjo ya UVIKO-19, mume wake ametesti 'mitambo' kwake na kukuta yupo 'fiti'

Ametoa kauli hiyo leo jijini Mwanza alipokagua jengo la Mama na Mtoto katika Hospitali ya Sekou Toure.

Amesema chanjo haiathiri kitu chochote katika mwili ndiyo maana yeye yupo vizuri baada ya kuchanja chanjo hiyo.

Pia, soma =▷ Waziri Gwajima: IGP Sirro yupo sahihi, wanaonichonganisha nitawavua nguo hadharani. Asema Corona imesababisha vifo vya kutosha

Hatujapenda kutuambia hivyo hadharani!
 
Rudia kuchanjwa uongeze fitness
 
Jamani
 
Back
Top Bottom