Waziri Doroth Gwajima, Wazazi na Wanafunzi tunasubiri ahadi yako kuhusu hatma ya waliovujisha mitihani ya utabibu

Travelogue_tz

JF-Expert Member
Sep 28, 2010
848
1,212
Habari JF


Serikali kupitia Wizara ya Afya ilitoa taarifa kuwa ipo katika hatua za mwisho kuwachukulia hatua wote watakaobainika walihusika katika kuvujisha mtihani wa kitaaluma wa mwaka wa pili wa matabibu pindi tu ripoti ya uchunguzi itakapokamilika na kuwasilishwa.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Dorothy Gwajima wakati akizindua kituo cha Elimu masafa kilichopo Mkoani Morogoro.

“Serikali imeunda kamati ya uchunguzi iliyoshirikisha vyombo vyote, wakiwemo polisi na vyombo vyote vingine vinavyohusika na kuchunguza tuhuma kama hizi, ripoti ipo hatua za mwisho kukamilika, itasomwa wazi… maana wahalifu hao walichokitafuta watakipata…” Amesema Dkt. Gwajima.

Ameendelea kusema kuwa, Serikali kupitia Wizara ya Afya itachukua hatua hizo kwa kufuata Sheria, Kanuni na miongozo bila kuonea yoyote ili iwe fundisho kwa wengine wanaofanya vitendo hivi ambavyo ni kinyume na taratibu na Sheria za nchi.
 
Kuchukuwa hatua ni jambo moja ila hatima ya wanafunzi itakuaje? Je watapoteza muhula mzima nyumbani? Hill linatakiwa kutatuliwa kwa haraka vijana wasipoteze muda
 
Back
Top Bottom