Waziri Dkt. Stergomena ziarani nchini India baada ya kupata mwaliko wa Waziri wa Ulinzi wa India, Rajnath Singh

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,806
11,968
WhatsApp Image 2022-08-28 at 10.46.52 PM (1).jpeg


Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dkt. Stergomena Lawrence Tax (Mb) amefanya ziara ya kikazi Nchini India kufuatia mwaliko wa Waziri wa Ulinzi wa India, Rajnath Singh.

Hii ni ziara yake ya kwanza ya kutembelea India tangu alipoteuliwa kuiongoza Wizara hii Septemba 12, 2021.

Wakati wa ziara hiyo, Mheshimiwa Stergomena na ujumbe wake walipata fursa ya kushiriki mkutano wa ulioandaliwa na mwenyeji wake kuhusu masuala mbalimbali ya ushirikiano katika sekta ya ulinzi. Katika mkutano huo, Serikali ya India imeahidi kuisadia Serikali ya Tanzania katika masuala mbalimbali yahusuyo ulinzi hususan teknolojia za kijeshi. Mkutano huo, ulifanyika katika Ukumbi wa Sushma Swaraj Bhawan na kulihudhuriwa pia, na Balozi anayeiwakilisha Tanzania nchini India, Mheshimiwa Balozi Anisa Mbega.

WhatsApp Image 2022-08-28 at 10.46.59 PM (1).jpeg


Akiongea katika mkutano huo, kwa umuhimu wa kipekee Mheshimiwa Waziri ameipongeza na kuishukuru Serikali ya India kwa kuendeleza Ushirikiano wa kihistoria na kindugu na baina ya Tanzania na India ulioduma tangu enzi za utawala wa Hayati Javan Neru na Hayati Mwl Julius Nyerere ambapo pande zote mbili zimeendelea kunufaika na ushirikiano huu.

Mheshimiwa Tax pia, aliwasilisha salaam za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Mheshimiwa Suluhu Hassan kwa Serikali ya India kuwa, azima ya Serikali ya Awamu ya Sita ya kukuza na kuendelea kudumisha ushirikiano wa kindungu na wa kihistoria kwa ustawi wa watu wa mataifa yote mawili.

Aidha, majeshi ya nchi hizi mbili yamekuwa na ushirikiano katika nyanja mbalimbali ikiwemo mafunzo. Ushirikiano huu umeanza tangu enzi za Vita vya Kagera ambapo India iliweza kutuma timu ya wataalamu waliosaidia kuandaa silabi inayotumiwa na Chuo cha Ukamanda na Unadhimu (CSC) na hivi sasa kuna timu ya wataalamu sita wanaofundisha namna ya uendeshaji wa Tri Service katika Chuo CSC.

Wakati wa ziara hiyo, Mheshimiwa Waziri alipata fursa ya kutembelea maeneo mbalimbali yakiwemo War gamming Development Centre, Mnara wa Kumbukumbu ya Mashujaa (Indian Gate) uliopo New Delhi na kusaini Kitabu cha maombolezo. Katika Jimbo la Hyderabad alitembelea wazalishaji wakubwa wa zana na vifaa vya kijeshi pamoja na maeneo mengine.

Katika ziara hiyo Mheshimiwa Waziri ameambatana na Mkuu wa Tawi la Mipango na Maendeleo Jeshini, Brigedia Jenerali Celestine Msola, Meneja Mkuu Shirika la Mzinga, Brigedia Jenerali Seif Hamis, Mkurugenzi Mkuu Tanzania Automotive Technology Centre (TATC), Brigedia Jenerali Hashimu Komba na Mkuu wa Mafunzo na Utendaji Kivita kutoka Jeshi la Wanamaji, Brigedia Jenerali Hamis.

WhatsApp Image 2022-08-28 at 10.47.12 PM.jpeg

WhatsApp Image 2022-08-28 at 10.47.16 PM.jpeg

WhatsApp Image 2022-08-28 at 10.47.10 PM.jpeg
 
Back
Top Bottom