Waziri Dkt. Stergomena afungua semina ya Wanawake, asisitiza washirikishwe katika amani na usalama

BigTall

JF-Expert Member
Mar 9, 2022
422
1,049
Waziri wa Ulinzi akihutubia.jpeg
Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dkt. Stergomena Lawrence Tax (Mb) amefungua Semina kuhusu Agenda ya Wanawake, Amani na Usalama (Women Peace and Security Agenda) iliyofanyika tarehe 07 Juni, 2022 katika Hoteli ya Serena Jijini Dar es Salaam.

Akihutubia washiriki wa Semina hiyo akiwa Mgeni Rasmi, Dkt. Stergomena amesema kuwa kwa kutambua ushirikishwaji wanawake kuwa ni jambo muhimu katika maendeleo na ustawi wa kijamii.

“Kwa maana hiyo, ni vyema tukatambua kuwa jukumu la wanawake wakati wa migogoro na katika kuleta amani yanatofautiana na pia ni suala gumu, hivyo basi linahitaji ushirikishwaji wa wanawake katika masuala ya amani na usalama ni muhimu.

“Agenda ya Wanawake, amani na usalama inatambua pia, kuwa wanawake na watoto ndiyo wahanga wakubwa wakati wa vita na inahitaji kutiliwa mkazo katika kuwashirikisha wanawake kama wadau wakubwa katika mifumo ya amani na usalama,” alisema.

Akielezea umuhimu wa Semina hiyo, Dkt. Stergomena amebainisha kuwa Semina hiyo inatoa fursa kwa washiriki kujadiliana na kubadilisha mawazo kuhusu mambo yahusuyo umuhimu wa wanawake kama wadau muhimu katika masuala ya kuleta amani na usalama.

Kwa kutambua hilo, Umoja wa Mataifa umepitisha Azimio Na. 1325 (2000) linalotambua umuhimu wa wanawake kushiriki katika kukomesha vita pamoja na kusistiza ushikishwaji sawa wa kijinsia katika kudumisha amani.
Waziri na Meza Kuu mbele nyuma Mabalozi.jpeg

Aidha, Azimio hilo linakumbusha ushirikishwaji wa wanawake katika taasisi za kitaifa za sekta za usalama, michakato pamoja na mapambano dhidi ya kila aina ya unyanyasaji wa kijinsia.

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kama mwanachama wa Jumuiya mbalimbali za Kikanda, mabara na kimataifa, imekuwa mstari wa mbele katika kutetea Agenda ya Wanawake, Amani na Usalama.

Aidha, Tanzania imeendelea kuunga mkono Mifumo ya kimataifa, kikanda katika kuwatambua wanawake kama wadau muhimu na kuwawezesha ili waweze kushiriki katika michakato yote inayohusu masuala ya amani na usalama.

Pia Waziri, alitoa wito kwa wadau wote wa masuala ya wanawake kuendelea kuitangaza na kuiunga mkono Agenda hii ya masuala ya wanawake, amani na usalama.

Semina hiyo ya siku moja, iliandaliwa na Ubalozi wa Norway Nchini Tanzania na kuhudhuriwa na wadau wa masuala ya kijinsia, amani na usalama, taasisi za elimu ya juu, wadau wa masuala ya wanawake, wawakilishi wa jumuiya za kikanda na kimataifa.

Miongoni mwao ni pamoja na Mwakilishi wa Waziri Maendeleo ya Jamii, Jinsia, wanawake na Makundi Maalum, Dkt. Joyce Nyoni, Balozi wa Norway hapa Nchini, Bi. Elisabeth Jacobsen, Balozi wa Denmark hapa nchini, Bi. Mette Norgaard Dissing Spandet, na Balozi wa Finland hapa nchini, Bi. Rita Swan na Bi. Jebbeh Forster Mshauri wa Kanda wa Utawala, Wanawake, Amani na Usalama kutoka Umoja wa Mataifa.
Wajumbe wakimsikiliza Waziri.jpeg
 
Back
Top Bottom