Waziri Dkt. Pindi Chana apokea taarifa hitilafu ya umeme Uwanja wa Mkapa

Ojuolegbha

JF-Expert Member
Sep 6, 2020
731
475
Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana leo Mei 6, 2023 katika Uwanja wa Benjamin Mkapa, amepokea taarifa ya Kamati aliyoiunda kuchunguza tukio la kukatika umeme katika uwanja huo wakati wa mechi ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika kati ya Dar es Salaam Young Africa (Yanga) dhidi ya Rivers United ya Nigeria.

Baada ya kupokea taarifa hiyo, Waziri Dkt. Chana amemuelekeza Katibu Mkuu wa Wizara Ndg. Saidi Yakubu kufanyia kazi taarifa hiyo ikiwemo kuchukua hatua zinazostahili kulingana na taarifa hiyo.Tukio hilo la kupokea taarifa lilihudhuriwa pia na Naibu Katibu Mkuu, Bw Nicholas Mkapa.

Kamati hiyo imeongozwa na Mwenyekiti Mhandisi Keneth Boymanda kutoka Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), ikiwa na Wajumbe kutoka Wakala wa Majengo nchini TBA, na baadhi ya watumishi wa wizara.

IMG-20230506-WA0036.jpg
 
Uwanja wa Mkapa, umeme kukatika katika imekuwa ni tatizo sugu, lazima lipatiwe suluhisho la kudumu
 
Huku kijiweni story kuhusu Hayati B.mkapa na watoto wake ni nyingi mno.
Nikemuona Naibu Katibu Mkuu Ndugu Nicholaus Mkapa.
Ni copyright ya Mshua wake.
Kiranga.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom