Waziri Dkt. Mwigulu Nchemba unapata wapi 'guts' za kutupangia 'emotions' zetu Watanzania juu ya Msiba uliotupata?

Diplomat Son

JF-Expert Member
Apr 2, 2015
6,010
2,000
Tena leo nakusema (nakuchana) Mubashara na kwa Uhuru kabisa kwakuwa Wewe upande wa Kabila na Mkoa ni Mtani wangu (Nyiramba na Nyaturu) na hata katika Medani za Soka la Tanzania pia ni Mtani Wewe ukiwa Yanga SC na Mimi nikiwa Simba SC.

Kwanza nikuambie tu Mtani wangu Mwigulu kuwa Kibinadamu hakuna aliyefurahia kilichotokea na kuna wakati hata Sisi ' aliotukwaza ' tulisikitika na kutoka ' tumachozi ' pia japo 'tudogo tudogo' sana.

Ila Mtani Mwigulu kinachotuuma Watanzania wachache tunaojielewa ' Upstairs ' acha wale wengi Wasiojielewa ambao waliguswa nae mno ni kwamba 'Jamaa' yako alitengeneza 'Bomu' kubwa ndani ya Taifa letu ambalo nina uhakika kwa ule mwendo wake tu ipo Siku lingelipuka na hata pia ' Kukudhuru ' na Wewe.

Yaani Mtani wangu Mwigulu Nchemba pamoja na hiyo 'Doctorate' yako na Akili zako kubwa ( nyingi ) za ' Kinyiramba / Kinyaturu ' umeshindwa tu kujua kuwa ' Jamaa ' alikuwa anatupeleka ' Kuzimu ' kabisa?

Kwahiyo Mtani wangu Mwigulu ukijengewa Barabara, Madaraja, treni ya Umeme, Bwawa la Umeme, kununuliwa Ndege, Vivuko na Masikini Kubatizwa Jina la Wanyonge ndiyo ' Legacy ' pekee ambayo utaiacha kwa Watanzania na hata Ukifa ( Ukifariki ) utataka ukumbukwe nayo?

Mtani wangu Mwigulu hivi umeshajiuliza tu Swali dogo kwamba kwanini Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere hakufanya mengi ya huyu ' Jamaa ' yako lakini haliliwi tu na Sisi Watanzania bali mpaka leo hata Watu wengine wa Mataifa mengi Ulimwenguni wanamlilia ( japo Washamba Wanyiramba na Wanyaturu ) wa Singida walipenda atokee Kwao ila bahati nzuri katokea Mkoa wa Mashujaa tupu wa Mara?

Ina maana Mtani ' Jamaa ' alivyoharibu ' Mifumo ' mingi, kuachia Vitendo vya ' Kikatili ' kutokea, Kuibaka kwa Nguvu Demokrasia ya Tanzania, Kuminya kwa Makusudi na Kuvichukia Vyombo vya Habari, kutengeneza Kundi la ' Wanaofaidika ' wachache, kutumia Pesa za Kujenga Kwao ambazo hazikuwa ' audited ' na CAG, kutisha ' Critics ' wake, Kukomoa, kuwa na Visasi vya Kipuuzi na Kuuharibu kabisa Uchumi wa Mtanzania Mmoja Mmoja Kwako Wewe ni sawa?

Tena Mtani Mwigulu nasikia nawe una Ndoto za kuja kuwa Rais wa Tanzania. Nakuombea Kheri ufanikiwe ila na Wewe ukiupata na kuja Kutuongoza ' hovyo ' kama huyo ' Jamaa ' yako (yenu) Mimi Mtani wako mkubwa Generalist ndiyo nitakuwa wa Kwanza kukuombea ' mabaya ' ili ' ufe ' kabisa na tukienda Kukuzika kule ' Unyirambani / Unyaturuni' kila Siku tuwe tunalipiga tu Mawe Kaburi lako.

Uwe na Kazi njema Mtani wangu MLN.
 
Mhandisi Mzalendo

JF-Expert Member
Aug 23, 2010
4,818
2,000
Gentamycin Genta nani sijui naona mwandiko wako haupotei

Umenena vyema kila mtu ashinde mechi zake

Wakucheka acheke wa kulia alie

Hata jambazi akiuawa kuna watu wanasikitika wengine wanafurahi

Hata Yesu alivyosulubiwa mpaka kufa kuna waliosikitika na walihuzunika na Mungu akulaumu wala kumuadhibu yeyote

Tuishi humo
 
Japo Mimi siyo huyo GENTAMYCINE ( na nashangaa kuona wengi 24/7 mnalazimisha ) kuwa Mimi ( ID hii ) ya Generalist ni yake nafurahia pia Kufafanishwa nae kwani inaonyesha huyo Member alikuwa ni Kipenzi chenu Kiuwasilishaji hapa JamiiForums.

Hata leo hii Mchezaji wa Kiungo wa Simba SC Jonas Mkude akifananishwa na aliyekuwa Kiungo wa FC Barcelona Xavi Hernandez huwa anafurahia na kiukweli hata Mkude 99% ya Uchezaji wake Uwanjani anamuiga Xavi.

Kuna Uzi nilianzisha wa kutoa ( kuweka ) Ufafanuzi kuhusu hii ID yangu ya Generalist na hizo ( hizi ) ID's zote mnazozilazimisha kuwa ni zangu nakuomba utafute uusome.

Naitwa Generalist ( alias ) ' Gifted Intellectually, Knowledgeable and Well Informed ' tu na siyo hao wengine na naomba hili lieleweke vyema Kwenu tafadhali kwani si tu mnanikera bali pia huwa mnaniboa.
 
Mkuu jinsi ulivyofafanua hapa na ulivyopatia jina la Genta ndio kabsa wewe ndiye yule.

Naomba link nikasome uzi wa ufafanuzi.
 
Odhiambo cairo

JF-Expert Member
Jul 11, 2015
15,393
2,000
Huyu unayemtukuza na kumsema kama mtani . Ni moja kati ya watu waliomchafulia sana mwendazake. Kumbuka WASIOJULIKANA walishamiri kipindi akiwa kiongozi wa idara hiyo . Kujikomba kulimrudisha relini

Odhis *
 
Diplomat Son

JF-Expert Member
Apr 2, 2015
6,010
2,000
Huyu unayemtukuza na kumsema kama mtani . Ni moja kati ya watu waliomchafulia sana mwendazake. Kumbuka WASIOJULIKANA walishamiri kipindi akiwa kiongozi wa idara hiyo . Kujikomba kulimrudisha relini

Odhis *

Akiwa mbele ya Vipaza Sauti na Camera anatutishia wale tunaompongeza Israeli kwa Kazi yake nzuri, wakati inasemekana hata Yeye pia alimpongeza sana tu huyu huyu Israeli ila anazuga tu Kiaina.
 
Odhiambo cairo

JF-Expert Member
Jul 11, 2015
15,393
2,000
Akiwa mbele ya Vipaza Sauti na Camera anatutishia wale tunaompongeza Israeli kwa Kazi yake nzuri, wakati inasemekana hata Yeye pia alimpongeza sana tu huyu huyu Israeli ila anazuga tu Kiaina.
Nakumbuka Alphonse Mawazo alivyocharangwa na mashoka. Kisa eti mkoa anaotoka bwana mkubwa hautakiwi kuwa na upinzani !!. Wakawapiga watu mabomu hospital BMC, wakazuia hata watu kumuaga, na hata mahakama iliposema aagwe walienda kuvunja kaburi lake. Kipindi hicho huyo ndiyo alikuwa waziri wa mambo ya ndani. AIBU

Halafu leo wanazuia furaha ya watu ,tena iliyotokana na kibali cha Mungu?!

Odhis *
 
dumejeuri

JF-Expert Member
Dec 28, 2014
1,785
2,000
Phd holder
IMG-20210330-WA0002.jpg
 
ZE DONE

Senior Member
Mar 3, 2012
153
250
Japo Mimi siyo huyo GENTAMYCINE ( na nashangaa kuona wengi 24/7 mnalazimisha ) kuwa Mimi ( ID hii ) ya Generalist ni yake nafurahia pia Kufafanishwa nae kwani inaonyesha huyo Member alikuwa ni Kipenzi chenu Kiuwasilishaji hapa JamiiForums.

Hata leo hii Mchezaji wa Kiungo wa Simba SC Jonas Mkude akifananishwa na aliyekuwa Kiungo wa FC Barcelona Xavi Hernandez huwa anafurahia na kiukweli hata Mkude 99% ya Uchezaji wake Uwanjani anamuiga Xavi.

Kuna Uzi nilianzisha wa kutoa ( kuweka ) Ufafanuzi kuhusu hii ID yangu ya Generalist na hizo ( hizi ) ID's zote mnazozilazimisha kuwa ni zangu nakuomba utafute uusome.

Naitwa Generalist ( alias ) ' Gifted Intellectually, Knowledgeable and Well Informed ' tu na siyo hao wengine na naomba hili lieleweke vyema Kwenu tafadhali kwani si tu mnanikera bali pia huwa mnaniboa.
Hakika wewe ni Genta😂😂😂
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom