Waziri Dkt. Mwigulu Nchemba aagiza taarifa za wananchi kurasimishwa

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,877
6,326
Waziri wa Katiba na Sheria Mwigulu Nchemba ameitaka Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA,) kuendelea kutoa elimu kwa wananchi kuhusiana na majukumu yanayotekelezwa na Wakala hiyo ikiwa ni pamoja na kuongeza kasi ya kufikia Mikoa mingi zaidi katika zoezi la usajili wa vizazi.

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam wakati alipotembelea Wakala hiyo Waziri Mwigulu amesema kuwa kazi zinazofanywa na Wakala hiyo ni kubwa na zinategemeana na taasisi nyingine ikiwemo Mamlaka ya vitambulisho vya utaifa na Uhamiaji hivyo ni vyema taarifa zote za usajili wa kila mwananchi zikasoma sawa katika ofisi zote zinazosajili na kuisaidia Serikali kupunguza gharama za kusajili wananchi pindi taarifa zao zinapohitajika.

"RITA ni kiungo muhimu sana na taarifa zote zinaanzia hapa hivyo mifumo ya taarifa lazima iongezewe nguvu kwa kuzirasimisha rasmi katika mfumo wa Serikali....mtu mwenye kitambulisho cha utaifa akienda katika Ofisi nyingine asianze kusajiliwa upya taarifa zake azikute kule, shirikianeni na taasisi nyingine kwa kushirikiana na watu wa tehama kujenga suala hili." Amesema.

Kuhusiana na utolewaji wa vyeti vya kuzaliwa Mwigulu ameipongeza Wakala hiyo kwa kuendelea kuifikia Mikoa mingi zaidi na amewaonya watendaji na raia wanaoshiriki kughushi vyeti hivyo kuacha mara moja.

"Kumpenyeza mtu asiye raia kupata cheti cha kuzaliwa ni kuihujumu Serikali, na Mtendaji yeyote na raia asiye mtendaji akishiriki hujuma hiyo atapata kile kinachofanana na uhujumu uchumi kwa mujibu wa Sheria." Amesema.

Aidha katika suala la mirathi amesema kuwa, Wakala hiyo ina jambo kubwa la kufanya katika suala hilo hasa kwa kuhakikisha mapungufu ya sehemu za sheria yanatatuliwa haraka na kurekebishwa na taratibu za kimila na imani zitengenezewe mazingira ya kisheria ili kuwafuata machozi wajane na yatima.

Vilevile amewataka kutunza kumbukumbu kwa Uzalendo wa hali ya juu na kwa kuzingatia sheria na kuahidi kutoa ushirikiano wa kutosha pamoja na kufanyia kazi maelekezo yaliyotolewa na viongozi wao.

Kwa upande wake Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Geophrey Mizengo Pinda ameitaka Wakala hiyo kuendelea kutoa elimu zaidi kuhusiana na suala zima la mirathi ili kuweza kupunguza migogoro katika jamii.
 
Naibu waziri G. Mizengo pinda?Aysee mwenye nacho huongezewa
Bahati nzuri kila mtu anacho chake amepewa; tofauti tu ni kwamba yule anatamani chako, wewe watamani cha yule. Sasa tujifunze kuona mkononi tuna nini na tutumieje. Huo ndio mtihani ambao majibu yake hutofautisha kati ya wale tuwaonao ni "wenyenavyo" & "wasonavyo."
 
Hatari mkuu😂
 
Wengine mkononi tuna madeni tu, na tunaongezewa, ngoja nione nitayatumiaje 😂
 
Kuhusiana na utolewaji wa vyeti vya kuzaliwa Mwigulu ameipongeza Wakala hiyo kwa kuendelea kuifikia Mikoa mingi zaidi na amewaonya watendaji na raia wanaoshiriki kughushi vyeti hivyo kuacha mara moja.

Yeye kabla hajaanza kulalamikia hili, amejipanga vipi kudhibiti hali hiyo?
Je anatambua nguvu ya teknolojia ya sasa?
 
Ni sahihi waziri yuko sahihi digitalization ni kuhakikisha taarifa za taasisi tofauti xa serikali zinasomana mfano kitengo cha passport unai gia digitally unajaza mifomu ao halafu inakuwa approved digitally halafu tena u atakiwa u print mi hard copy uwapelekee manually waanze tena kuipitia manually kama ilivyokuwa kabla ya digitalization hiyo ni double work na urasimu
Kazi kitengo cha passport imeongezeka badala ya kupungua hata wanaposema ohh tume digitalise uongo process ni shahidi ni kuwa kazi zimeongezeka badala ya kupungua kupunguza usumbufu kwa mwombaji na ofisa passport ukiuliza why double work wanasema sysyem hazisomani!!! kila moja ni stand Alone!!! ukijaza mfano kitambulisho cha taifa kupmba passport online inabidi upeleke hard copy uhamiaji waone uitoe photocopy !!! ha ha ha sasa wame digitalize nini? Kama system zao hazisomani ata na kitambulisho cha taifa?

Kampuni za simu zimejitahidi mno ukienda kusajili line ukiwa na namba tu ya NIDA unasajili shida unaweka dole gumba tu biashara imeisha zinasomana na NIDA Kitengo cha Passport hakuna.Hiyo digitalization ya Kutengo cha Passpirt hata siielewi wali digitalise nini wakati bado mikazi inaenda manually
 
Back
Top Bottom