uchumi2018
JF-Expert Member
- Mar 4, 2018
- 1,424
- 1,966
Kwa maelez
tunaposema kiswahili ni lugha ya taifa huku tunaendelea kutumia kiingereza tunamdanganya nani?
Mambo yote lazima kuwepo mwanzo wake,na mwanzo ni mgumu.
Mfano mzuri ni uthubutu wa mh. Rais kuihamishia ikulu mjini Dodoma.
Nimesoma habari hizi na faida za ikulu kuhamia dodoma toka nipo shule ya msingi,marais wamepita wanne hakuna aliyethubutu nadhani hofu ilikuwa kama hii ya kwako.Mmmoja amethubutu na mambo yanaenda vizuri.Tuchukulie huu mfano,kufanya na mengine.
Tuache hofu na woga wa kuthubutu,vinginevyo tuanze kufundisha kiingereza kuanzia shule za misingi.
Kwa hoja yako hii,basi peleka mswada tuondoe kiswahili kuwa lugha ya taifa.Unaweza kujifanya unajua sana lakini hiyo haitaondoa ukweli wa usichokijua.
Lugha ni kielelezo cha mambo mengi. Kulazimisha kutumia Kiswahili wakati Sheria zenyewe zinafundishwa kwa Kiingereza, mfumo wenyewe wa Sheria tunaoutumia ni wa UK (jumuia ya Madola), fani nyingine zote, na mfumo wote wa sheria ni wa Kiingereza, ni kukurupuka kwa hali ya juu.
Huwezi kuwa na uhuru wa lugha kama huna uhuru wa tekinolojia na uchumi. Ukilazimisha kutumia lugha yako, unajitesa mwenyewe. Dunia imekuwa hivyo tangu enzi za Yesu. Wayahudi walikuwa na lugha yao lakini kutokana na uduni wa tekinolojia, lugha iliyokuwa inatumika kwenye mambo yote ya kitaalam ilikuwa Kigiriki. Imekuwa hivyo kwa mataifa mengi.
Ni nchi gani maskini inayotumia lugha yake ya asili? Hakuna anayekukataza lakini ukifanya hivyo, utajitesa mwenyewe.
Huyo mkurupukaji Mwigulu, anayesema sheria zote zitafsiriwe kwa Kiswahili, atatafsiri na marejeo yote ya hukumu kutoka jumuiya ya madola kwenda kwenye Kiswahili? Atawapeleka wanasheria wote masomoni ili wakapate uoanishi mzuri wa walichojifunza toka Kiingereza kwenda Kiswahili?
Sent using Jamii Forums mobile app