Waziri Dkt. Mwigulu ataka sheria zitafsiriwe kwa lugha ya Kiswahili

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,001
9,866
Waziri wa Katiba na Sheria, Dkt. Mwigulu Nchemba amemtaka Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, kutafuta wataalamu mara moja wenye uwezo wa kutafsiri sheria zote za nchi kwa lugha ya Kiswahili

Imeamriwa kufanywa hivyo ili iwe rahisi kwa wananchi kuelewa sheria hizo hususan wakati wa kesi na hukumu ili kurahisha uelewa

Dkt. Mwigulu ametoa kauli hiyo, Dar es Salaam katika ziara yake katika Taasisi ya Mafunzo ya Sheria kwa Vitendo, ambapo amesema wananchi wanapata shida kuelewa sheria za nchi kutokana na lugha inayotumiwa

Aidha ameitaka Taasisi ya Mafunzo ya Sheria kwa Vitendo kuwaandaa wanaopata mafunzo hayo kwa muelekeo wa Kiswahili hata kama watatumia kiingereza.
 
Nimeyasikia maagizo yako ulipokuwa ktk chuo cha sheria.

Pamoja na yote uliyoyaongea, kilichonifrahisha ni maagizo yako yakutaka itaftwe team ya kutafsiri sheria zetu kutoka kiingereza na kwenda katika rug'ha tam ya kiswahili. Ambayovpia ni lugha ya taifa.

Ninachokuomba au kitu ambacho nilitegemea nikisikie ni kutoa muda maalum wa kutekelezwa jambo hilo, ili lisiwe agizo kama maagizo mengine ya mchakato bado unaendelea.

Maana sioni sababu ya jambo hili kutotekelezwa hata ndani ya miezi mitatu, kwakuwa tuna wasomi wengi ktk lugha hii ya kiswahili, na waalimu wengi wanaofundisha kiswahili ktk mataifa duniani.

Nawasirisha tafadhari.
Enzi na Enzi.
Dar es salaam.
 
Hongera sana Mhe. Mwigulu Nchemba kwa kuweka mkazo la matumizi ya kiswahili ktk mambo yanayo tuhusu watanzania na haswa katika maswaala ya haki.

Watanzania karibu 95% wanafahamu kiswahili sio kiingereza hivyo jambo hilo litawasaidia watanzania wengi kujua sheria na jinsi ya kudai haki zao, na tunaomba hilo liende sambamba na hukumu zinazo tolewa pia ziwe kwa lugha yetu ya kiswahili ili tuweze kujua kilicho andikwa.

Hakika matumizi ya lugha yetu yatarahisisha zaidi upatikanaji wa haki za wananchi kuliko matumizi ya kiingereza.
tunaomba maamuzi haya yatekelezwa haraka kama waziri alivyo sisitiza.
 
Nadhani itawasaidia hata Majaji wetu ambao Tundu Lissu aliwananga kuwa hawajui Kiingereza! Big up Mwigulu.
 
Kujua kiingereza sio weledi wa kujua sheria, kinacho takiwa watanzania waelewe haki zao, kwa nini wasumbuke kwa kulazimishwa na kizungu?!! mataifa mbali mbali yanatumia lugha zao ktk mambo yao, mfano china, urusi, uturuki, ufarnsa, n.k.

Lugha ya kiingereza ibaki kama lugha tu lkn isiwe ndio inaongoza taratibu za utoaji haki za watanzania ambao wengi wao hawajui lugha ya kizungu.
 
Ni wazo zuri ila kusema sheria ziandikwe kwa kiswahili ili watanzania waweze kuelewa hapa nadhani mheshimiwa hajaelezwa vyema.

Kujua lugha fulani sio kujua sheria, sheria ni zaidi ya hapo.

Uingereza wanaongea kiingereza lakini bado sheria ni moja ya fani ngumu kuielewa.

Mfano wapili, Katiba yetu ipo kwa lugha ya kiswahili lakini watanzania hawajui hata haki zao zilizopo kwenye katiba.

Wazo zuri ila halitatibu tatizo. Tatizo lipo nje ya lugha ya kiingereza inayotumika kwenye mambo ya kisheria nchini.

Sheria ya ardhi inayo nakala ya kiswahili lakini bado migogoro inaongezeka vile vile sheria za mirathi na kanuni ya adhabu.
 
Waziri wa Katiba na Sheria, Dkt. Mwigulu Nchemba amemtaka Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, kutafuta wataalamu mara moja wenye uwezo wa kutafsiri sheria zote za nchi kwa lugha ya Kiswahili...
Hana mvuto huyu waziri. Alipe kwanza madeni yake makubwa ya fedha kwa wananchi. Eti naye dokta! Hovyooo.
 
Tatizo baadhi ya watanzania wanajivunia sana kiingereza utadhani lugha ya mama lkn kumbe ni ulimbukeni tu umemjaa kichwani. mpaka leo bado wengi wao wanadhani weledi wa mtu unapomwa kwa kujua kuongea au kuandika kizungu!!! huu ni utumwa uliopo kichwani, tuheshimu lugha yetu ya kiswahili hii ndio lugha yetu na inapaswa itumiwe kila mahala ktk taifa letu

1. BUNGENI taarifa zote za bunge ziwe kwa lugha ya kiswahili.

2. MAHAKAMANI taarifa zote yaani Hukumu, n.k ziwe kwa lugha ya kiswahili maaana nyaraka hizo zinawahusu watanzania sio wazungu wala wamerekani, hivyo hakuna sababu ya kuwafucha watanzania wengi kwa lugha wasiyo ufahamu.

3. Maofisi yote ya serikali yatumie lugha ya kiswahili ktk nyaraka zao.

Haya matumizi ya kiswahili ni kwa masilahi ya watanzania/wananchi tusijaribu kulinda maslahi ya wachache kwa kuwaminya walio wengi.

sijaona tija ya kunga'gania kiingereza wakati wanao kielewa ni wachache, tuzungumze kiingereza tukitaka lkn kumbukumbu zetu zibaki au ziandikwe kwa lugha ya KISWAHILI huu ndio uzalendo na kuenzi utamaduni wa kitanzania kwa vizazi vya sasa na vijavyo.
 
Ni wazo zuri ila kusema sheria ziandikwe kwa kiswahili ili watanzania waweze kuelewa hapa nadhani mheshimiwa hajaelezwa vyema.

Kujua lugha fulani sio kujua sheria, sheria ni zaidi ya hapo.

Uingereza wanaongea kiingereza lakini bado sheria ni moja ya fani ngumu kuielewa.

Mfano wapili, Katiba yetu ipo kwa lugha ya kiswahili lakini watanzania hawajui hata haki zao zilizopo kwenye katiba.

Wazo zuri ila halitatibu tatizo. Tatizo lipo nje ya lugha ya kiingereza inayotumika kwenye mambo ya kisheria nchini.

Sheria ya ardhi inayo nakala ya kiswahili lakini bado migogoro inaongezeka vile vile sheria za mirathi na kanuni ya adhabu.
kinacho takiwa hapa ni kurahisisha watu kuelewa haki zao kwa kutumia lugha yao ya kiswahili,

mfano. Hukumu inayo tolewa mahakamani imeandikwa kwa kiingereza halafu unapewa, mimi sijui kiingereza lazima nitafute mtu kwanza anitafsirie ili nielewe kilicho andikwa....lkn kama ingeandikwa kwa kiswahili ningejisomea mwenyewe na kuelewa neno kwa neno.

hivyo suala hapa kwanza ni uelewa sio ujuzi, ujuzi wa sheria utabaki kwa wanasheria wenyewe...tunacho taka ni wananchi kwanza waelewe kilicho andikwa hiyo ndio haki yao ya msingi.
 
Makaratasi yoote ya kupigia kura yalichapishwa kwa kiswahili lakini mliiba kura!!!

Watawala wanatumia kiswahili kubambikizia kesi feki wananchi wasio na hatia.

Nina mashaka Kama matumizi ya kiswahili pekee yanaweza kuleta HAKI
 
Back
Top Bottom