Waziri Chibulunje apandwa pressure akijibu swali; apelekwa hospitali. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Waziri Chibulunje apandwa pressure akijibu swali; apelekwa hospitali.

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Hassani, Jul 22, 2009.

 1. Hassani

  Hassani JF-Expert Member

  #1
  Jul 22, 2009
  Joined: Jun 5, 2009
  Messages: 267
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 45
  wakuu nimesikia tetesi kuna waziri kadondoka ghafla wakati akijibu swali bungeni,je ni kweli?kama kuna mwenye full details atumwagie
   
  Last edited by a moderator: Jul 23, 2009
 2. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #2
  Jul 22, 2009
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180

  Mi sijaipata BADO.
  Mwenye nazo atupe
   
 3. Sokwe Mjanja

  Sokwe Mjanja JF-Expert Member

  #3
  Jul 22, 2009
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 579
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Naibu Waziri wa Maendeleo ya Miundombinu, Hezekiah Chibulunje amesema changamoto za kazi zilisababisha akumbwe na shinikizo la damu wakati anajibu swali bungeni leo asubuhi.

  Muda mfupi uliopita Chibulunje amewaeleza waandishi wa habari mjini Dodoma kuwa anaendelea vizuri.

  Kiongozi huyo wa Serikali ameyasema hayo saa nane mchana baada ya kuruhusiwa kutoka katika Hospitali Kuu ya mkoa wa Dodoma takribani saa tano tangu alazwe.

  Alilazwa leo saa tatu asubuhi dakika kadhaa baada ya kushindwa kujibu swali bungeni na kuonekana kupumua kwa taabu. "Ni stress za kazi. Presha ilipanda tu lakini sasa naendelea vyema," amesema Chibulunje.

  Daktari aliyekuwa akimtibu, Dk Zainab Chaula amesema, Chibulunje alikuwa na malaria tangu Jumatatu.

  Kwa mujibu wa daktari huo, Mbunge huyo wa Chilonwa mkoani Dodoma amekuwa akitumia dawa za kutibu malaria vile vile alifikishwa hospitalini hapo akisumbuliwa na shinikizo la damu.

  Mganga Mkuu wa Hospitali ya Mkoa wa Dodoma, Godfrey Mtei pia amethibitisha kwamba Naibu Waziri huyo alikuwa akisumbuliwa na shinikizo la damu.

  Leo chana Rais Jakaya Kikwete alifika hospitalini kumuona Naibu Waziri na kukaa wodini kwa takribani dakika 10.

  Wakati anakumbwa na tatizo hilo la shinikizo la damu, Chibulunje alikuwa akijibu swali la Mbunge wa Kalenga, Stephen Galinoma aliyetaka kufahamu sababu za Iringa kutounganishwa na njia nyingine za anga kama Mbeya au miji mingine ya Kusini.

  Wakati anaanza kujibu swali hilo alikuwa akisitasita, mkono wa kulia ulishika kifua upande ulipo moyo na akawa anahema haraka haraka.

  Aliendelea kusoma majibu hayo, kwa namna alivyokuwa anahema sauti ilisikika kwenye vipaza sauti na kusababisha ukimya huku watu ukumbini wakimtazama kwa makini na kufuatilia alivyokuwa akijibu.

  Wakati anaendelea kujibu swali hilo huku akisita mara kwa mara, Naibu Spika Anne Makinda alimtaka aache kujibu na apumzike.

  "Mheshimiwa Naibu Waziri pumzika na Waziri endelea" alisema Makinda. Hata hivyo Chibulunje aliendelea na ndipo baada ya sekunde chache akashindwa kuendelea kujibu.

  Waziri wa Maendeleo ya Miundombinu, Dk. Shukuru Kawambwa alikwenda kumshikilia na kumsogeza kwenye kiti ,yeye (Kawambwa) akaendelea kujibu swali hilo.

  Dk Kawambwa amesema "kutokana na matatizo ya kiafya aliyokuwa nayo nilimuuliza kama angeweza kujibu maswali akanihakikishia angeweza na anaendelea vizuri lakini kilichotokea mmekiona.

  Baada ya Chibulunje kukaa kwenye kiti, Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Jumanne Maghembe , Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Dk. Maua Daftari na Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Profesa David Mwakyusa walikwenda kumsaidia.

  Naibu Waziri wa Afya, Dk. Aisha Kigoda alishirikiana na mawaziri hao kumsaidia kunyanyuka kwenye kiti, wakamtoa nje ya ukumbi wa Bunge huku wabunge wengine na askari wa ndani ya bunge wakiwafuata kwa nyuma.

  Dk.Mwakyusa na Chibulunje waliingia kwenye gari binafsi na kuondoka kwa kupitia lango analopitia Waziri Mkuu, dakika 10 baadaye Waziri huyo alirudi bungeni.

  Huyu ni mbunge wa pili kulazwa hospitalini hapo katika kipindi cha mkutano huu wa bunge unaoendelea Dodoma. Mwingine ni Mbunge wa Same Mashariki, Anne Kilango aliyelazwa hivi karibuni ili kufanyiwa operesheni ndogo.
   
 4. Sokwe Mjanja

  Sokwe Mjanja JF-Expert Member

  #4
  Jul 22, 2009
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 579
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Sio yangu jamani ni from ippmedia........
   
 5. Hassani

  Hassani JF-Expert Member

  #5
  Jul 22, 2009
  Joined: Jun 5, 2009
  Messages: 267
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 45
  Ahsante kwa manews mkuu
   
 6. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #6
  Jul 22, 2009
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  teh teh teh ..presha inapanda presha inashuka..hofu ya kutoa majibu ya hovyo hovyo hii
   
 7. Tusker Bariiiidi

  Tusker Bariiiidi JF-Expert Member

  #7
  Jul 23, 2009
  Joined: Jul 3, 2007
  Messages: 4,757
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 160
  Kama nawaona Ze orijino komedi wamepata cha kuigiza wiki hii...
   
 8. Mkaa Mweupe

  Mkaa Mweupe JF-Expert Member

  #8
  Jul 23, 2009
  Joined: Jun 29, 2007
  Messages: 654
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Hizi nilizobold zimenitatiza kuelewa timing, nisaidieni waungwana
   
 9. Monsignor

  Monsignor JF-Expert Member

  #9
  Jul 23, 2009
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 523
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Waandishi wa form four failure hao mkuu. Hizo mbili za juu zinaweza kuwa sahihi ila hiyo ya mwisho ndio imeharibu kila kitu. Mimi nilidhani kuwaa vyombo vya habari vina wahariri wa habari ambao wangeweza kuona utumbo huu kumbe nao bure tu.
   
Loading...