Waziri Charles Kitwanga --Kosa la kiufundi!

MBATATA

JF-Expert Member
Jul 23, 2013
542
209
Mhe Waziri uko kwenye press conference kuzungumzia ujambazi. Ina waambia Wananchi kuwa sasa utawasiliana na Waziri wa Ulinzi muanze kufagia misitu inayo zunguka Jiji la Dar es Salaam na kuvunja kambi za wahalifu!
Unategemea utamkuta mtu huko kwa kauli hiyo?
Hebu tafuteni ushauri kwanza, hata kama una jazba?
 
Ina maana hao majambazi wanaishi ktk misitu?hawana makwao?kazi bado sana!
 
Mhe Waziri uko kwenye press conference kuzungumzia ujambazi. Ina waambia Wananchi kuwa sasa utawasiliana na Waziri wa Ulinzi muanze kufagia misitu inayo zunguka Jiji la Dar es Salaam na kuvunja kambi za wahalifu!
Unategemea utamkuta mtu huko kwa kauli hiyo?
Hebu tafuteni ushauri kwanza, hata kama una jazba?
Kiintelijensia hayuko sawa. Halafu tukio dogo kama lile la Mbagala Waziri unatoaje tamko? mwachie RPC ndio shughuli yake. Hata idara imemshangaa sana.
 
Mh Kitwanga awe makini anapo ongea na vyombo vya habari..... Juzi anaenda ofisi ya maadili nilimsikia akisema " niliandika mshahara wa waziri maana nilikuwa siujui" kimsingi mi niliona kuandika hivo sio sawa maana angeuliza hata kwa katibu mkuu wake angempa figure maana alikuwa naibu kwa muda mrefu tu, au hata mtangulizi wake.... halafu kusema hivo ni kuonyesha kuto jipanga ukiwa mbele ya vyombo vya habari.... awe makini maana yeye ndo tumaini letu kwenye suala la usalama.....
 
Kiongozi umenena. La msingi ni kujipanga unapokabiliwa na vyombo vya habari, lipi la kusema na lipi la kutafakari kabla hujatoa tamko. Bwana Kitwanga ana mtihani mkubwa kwa kuwa sehemu kubwa ya kazi yake itakuwa ni kufafanua mambo yanayohusu usalama wa raia, na mikakati inayotumika ya vyombo anavyo viongoza!
 
Mhe Waziri uko kwenye press conference kuzungumzia ujambazi. Ina waambia Wananchi kuwa sasa utawasiliana na Waziri wa Ulinzi muanze kufagia misitu inayo zunguka Jiji la Dar es Salaam na kuvunja kambi za wahalifu!
Unategemea utamkuta mtu huko kwa kauli hiyo?
Hebu tafuteni ushauri kwanza, hata kama una jazba?

You know nothing about security! Shurr-up!
 
Mh Kitwanga awe makini anapo ongea na vyombo vya habari..... Juzi anaenda ofisi ya maadili nilimsikia akisema " niliandika mshahara wa waziri maana nilikuwa siujui" kimsingi mi niliona kuandika hivo sio sawa maana angeuliza hata kwa katibu mkuu wake angempa figure maana alikuwa naibu kwa muda mrefu tu, au hata mtangulizi wake.... halafu kusema hivo ni kuonyesha kuto jipanga ukiwa mbele ya vyombo vya habari.... awe makini maana yeye ndo tumaini letu kwenye suala la usalama.....
Mkuu.. Ebu nisaidie.. Maana nina uelewa mdogo... Kuna waziri naye juzi wakati anarudisha fomu alisema alichelewa kurudisha hizo fomu kwa sababu alikuwa hajui mshahara wake... Sasa sijuhi ndio huyu au mwingine.

Swali langu: inawezekanaje mtu akawa hajuhi mshahara wake!? Mahususi hawa mawaziri!??
 
Mkuu ni yeye ila alijaza " mshahara wa waziri" kwa maneno...inawezekana alikuwa hajapewa apointment letter na anatakiwa awe amerudisha form in 30 days tangu amechaguliwa kwa kujibu
wa sheria.....
 
Kiintelijensia hayuko sawa. Halafu tukio dogo kama lile la Mbagala Waziri unatoaje tamko? mwachie RPC ndio shughuli yake. Hata idara imemshangaa sana.
Sidhani kama hilo tukio lilikuwa dogo. Majambazi 12 kuvamia benki na bunduki + mabomu ya kutupwa na mkono, kuua na kutoroka na fedha! Hili tukio lingetokea nchi ziliendelea lingepewa kila aina ya kipaumbele. Yuko sawa kabisa.
 
Back
Top Bottom