Waziri Chamuriho uliahidi kutangaza tenda ya ujenzi wa Barabara ya Itoni (Njombe) - Lusitu (Ludewa), mbona kimya?

Munjombe

JF-Expert Member
Dec 10, 2018
1,932
2,627
Mheshimiwa waziri ukiwa pale Luponde Mkoani Njombe, wakati ukitokea Ludewa watu walikusimamisha na kukueleza adha wanayopitia kutokana na barabara kuwa mbovu na wewe uliuona uhalisia na ukaahidi kuwa mwezi wa tano mtatangaza Tender ya kuanza ujenzi wa barabara ya Njombe-Ludewa-Manda kwa kujenga kipande cha kilomita 50 Kuanzia Itoni hadi Lusitu.

Mheshimiwa wakati ule ilikuwa tarehe 26.04.2021. Leo ni tarehe 11.08.2021 Imeshapita miezi takribani mitatu na mwezi watano ulishaisha kitambo na tuko mwezi wa nane bado hujatangaza na wananchi wale uliowaahidi wanatupigia simu kutuuliza maana kwa vile tuko mjini wanahisi tunaonana na wewe kila siku.

Hivyo kwa kupitia jukwaa hili la jamiiforum naomba uturudishie jibu kama ile ilikuwa ni staili ya kuondokea au ulimaanisha.Naomba pia ninukuu maneno yako hapa chini ambayo pia yapo YouTube.

“Naomba wananchi wa hapa muondoe hofu, kwani barabara hii tutaijenga kwa kiwango cha lami na kwamba ifikapo mwezi wa Tano mwaka huu, Serikali itatangaza zabuni ya barabara hii”.

“Barabara hii ni ya kiuchumi, hivyo lazima ijengwe kwa kiwango cha lami, ili kurahisisha huduma za usafirishaji katika maeneo haya ambapo wengi wenu mnalima mazao kama chai, mbao, viazi na mahindi”


Mheshimiwa waziri mvua Njombe zinaanza mwezi wa kumi na moja au wa kumi na mbili na kuishi mwezi mei katika kipindi hicho magari makubwa kuanzia Tani 10 juu huwa yanaivuruga barabara hii ya vumbi kwa kuwa mzigo wako hauendani na uimara ya barabara yenyewe. Naomba ile ahadi yako uikumbuke tena.
 
Back
Top Bottom