Waziri Biteko atembelea GGML, asema Geita imekusanya Bilioni 400 toka sekta ya madini

mkiluvya

JF-Expert Member
May 23, 2019
802
725
1591363172585.png

Waziri wa Madini, Dotto Biteko ameipongeza Kampuni ya Uchimbaji wa Madini ya dhahabu – Geita (GGML) kwa kuwa mdau wa mfano katika kuchangia utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika Mkoa wa Geita.

Biteko ametoa kauli hiyo jana katika ziara fupi aliyoifanya mkoani Geita na kukagua miradi inayotekelezwa na Kampuni ya GGML chini ya mpango wake wa kusaidia jamii (Corporate Social Responsibility) katika Mji wa Geita.
Aidha, alisema lengo la Serikali ni kuona maisha ya watu katika maeneo yote yenye rasilimali madini, ikiwemo Geita yanabadilika kiuchumi.

“Nimefurahishwa na namna ambavyo Serikali katika Mkoa wa Geita inavyosimamia ukusanyaji wa mapato kutoka kwenye sekta ya madini. Tayari tumeshafikia lengo la kukusanya zaidi ya Sh bilioni 400 kwa mwaka wa fedha unaoishia Juni 2020 kutoka kwenye sekta hii, na sehemu kubwa ya makusanyo haya imetoka Geita, hususan GGML.

“Inatia moyo sana kuona kwamba sekta hii sasa inachangia zaidi ya asilimia 5 ya uchumi wa nchi yetu. Lengo ni kuhakikisha kwamba sekta ya madini inachangia asilimia 10 ifikapo mwaka 2025,’’ alisema Biteko.

Mojawapo ya miradi ambayo ilikaguliwa na waziri huyo katika ziara yake ni ujenzi wa Kanda maalumu ya uwekezaji ”Special Economic Investment Zone” ambao utasimamiwa na Mamlaka ya ukanda maalumu wa Uwekezaji (EPZA) na Halmashauri ya Mji wa Geita. Pia alitembelea miradi mingine ya kimkakati inayofadhiliwa na GGML, ikiwemo ujenzi wa Soko Kuu la Geita Mjini na soko la Katundu.

Aidha, Makamu wa Rais anayeshughulikia Maendeleo Endelevu katika Kampuni ya GGML, Simon Shayo alisema utekelezaji wa miradi ambayo imetembelewa na waziri Biteko ni sehemu ya mpango wa mwaka 2018/19 unaoenda sambamba na mojawapo ya tunu za kampuni hiyo inayoelekeza kwamba jamii inayozunguka shughuli zake sharti ifaidike kwa uwepo wake.
 
Back
Top Bottom