Suley2019
JF-Expert Member
- Oct 7, 2019
- 1,811
- 4,533
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Innocent Bashungwa amewataka wamiliki wa vyombo vya habari Tanzania kuhakikisha wanalipa tozo za muziki unaopigwa katika redio zao ili kuwawezesha wasanii kupata haki zao.
Bashungwa amesema hayo jana Ijumaa Septemba 3, 2021 wakati akizinduzi kituo kipya cha redio cha Gold FM mjini Kahama, akibainisha kuwa wasanii wanaingia gharama kubwa kutayarisha muziki lakini wanapata ujira mdogo.
Amesema, kila mmiliki wa redio hapa nchini anatakiwa kulipa kiasi cha Sh62,500 kwa mwezi bila kusukumwa na anaruhusiwa kupiga wimbo wowote ulioimbwa na wasanii wa Tanzania na kufanya hivyo ni kuwawezesha wasanii hao kupata ujira wao.
Bashungwa amesema, Serikali ni wakala wa ukusanyaji wa tozo hizo hivyo kile kinachokusanywa kila mwezi kupitia kazi za wanamuziki zinazopigwa redioni kinawasilishwa katika chama kinachosimamia haki za wasaniii (Kosota).
Pia Bashungwa amesema, Serikali imefuta tozo za kwenye mitandao ya kijamii ikiwemo Instagram, YouTube na Facebook kwa watu ambao hawafanyi maudhui ya kihabari hivyo wajasirimali wanaruhusiwa kutangaza biashara zao kupitia mitandao hiyo.
Kwa upande wake Meneja wa Mamlaka ya Mawasiliano (TCRA) Kanda ya ziwa Francis Mihayo amesema, tozo hizo zipo kisheria na gharama zake, hivyo lazima wamiliki waweze kuzilipa fedha hizo kwani haziingii serikalini bali zinakwenda kuwalipa wale wanamuziki ambao wameshiriki katika kuimba nyimbo hizo.
Mihayo amesema, Kanda ya Ziwa kuna redio 39, ambapo Mkoa wa Mwanza pekee una Redio 15, Kagera radio 12, Shinyanga Radio tano, huku Gold Fm kikiwa kituo cha sita baada ya kufungukiwa na kwamba vituo hivyo vikilipa tozo hizo kutawanyanyua wasanii.
Naye Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Festo Kiswaga amesema, atahakikisha anasimamia tozo hizo zinatolewa kwa wakati ili kuondoa migogoro isiyokuwa na tija baina ya wamiliki wa redio hizo na serikali na hakikisha wasanii wananufaika na uwepo wa radio zilizopo.