Waziri Bashungwa apiga marufuku walimu kupita kila ofisi ya halmashauri kutafuta huduma

JUMA JUMA

JF-Expert Member
Jan 5, 2013
664
829
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mhe. Innocent Bashungwa amepiga marufuku walimu kupita kila Ofisi ya Halmashauri kutafuta huduma na ameagiza wapelekewe huduma hizo shuleni badala ya watoa huduma kufatwa Ofisini.

Ametoa agizo hilo leo tarehe 8 Septemba, 2022 Jijini Dodoma wakati akiongea na waandishi wa habari kutoa taarifa kwa umma ya uboreshaji wa huduma kwa walimu nchini.

“Ni marufuku kuwaacha walimu kupita kila ofisi ya Halmashauri kutafuta huduma, narudia tena mwalimu apelekewe huduma shuleni badala ya watoa huduma kukaa ofisini,” amesema Bashungwa.

Amesisitiza kuwa Mwalimu akiandika barua kwenye Mamlaka za Serikali za Mitaa kuhitaji huduma, anapaswa kujibiwa kwa maandishi ndani ya siku 7 baada ya kupokelewa.

Aidha, Bashungwa amewaagiza Wakuu wa Mikoa na Wilaya zote nchini kuwasimamia Wakurugenzi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa, Maafisaelimu, Maafisa wa Tume ya Utumishi wa Walimu, Wathibiti Ubora wa Shule kuhakikisha wanawafuata walimu mashuleni na kutatua kero na malalamiko yao kwa wakati.

Amewataka viongozi hao kufuatilia na kuwasimamia viongozi wa elimu katika ngazi ya Mikoa, Halmashauri, Kata na shule kutekeleza mikakati ya uboreshaji na usimamizi wa elimu na kuhakikisha wanawasilisha taarifa ya utekelezaji Ofisi ya Rais – TAMISEMI kila robo mwaka.

Vile vile, amewataka kusimamia utekelezaji wa Mipango ya Mafunzo kazini kwa walimu, kwa mujibu wa Mwongozo uliotolewa na Katibu Mkuu Utumishi na ufanyike kwa uwazi na ushirishwaji wa kutosha, ili kuondoa dhana ya kuwa waajiri wanatoa nafasi za mafunzo kwa upendeleo.

Pia, Bashungwa amewaelekeza Wakuu wa Mikoa na Wilaya kuwasimamia Maafisa wa Tume ya Utumishi wa Walimu kuzingatia miongozo ya upandishwaji vyeo walimu, ili kila anayestahili kupandishwa cheo, anapandishwa kwa mujibu Sheria, Kanuni na Miongozo.
 

Attachments

  • IMG-20220908-WA0097(2).jpg
    IMG-20220908-WA0097(2).jpg
    44.2 KB · Views: 3
  • IMG-20220908-WA0099(2).jpg
    IMG-20220908-WA0099(2).jpg
    72.1 KB · Views: 3
  • IMG-20220908-WA0098(2).jpg
    IMG-20220908-WA0098(2).jpg
    68.6 KB · Views: 3
viongozi wa elimu katika ngazi ya Mikoa, Halmashauri, Kata na shule
Walimu wana mabosi wengi!!!

Hapo bado wakurugenzi, madiwani, mawaziri, makatibu wakuu, makatibu tawala, maafisa Utumiaji, rais, waziri mkuu, makamu wa rais, n.k
 
Tuchukulie mfano wa wilaya moja ya Kinondoni.

Afisa Elimu msingi akifika ofisini anatakiwa atembelee shule ngapi kwa siku ili kupeleka huduma yake. Yaani mawaziri wetu sijui wanawazaga nini sijui. Hivi kwa siku kuna maombi/Shida za waalimu wangapi zinapelekwa wilayani au mkoani? Mkurugenzi ataweza kweli kuzunguka kila shule kupeleka majibu na solutions za waalimu? Wakati huo masuala mengine ya ukurugenzi nani anafanya?

Yeye angesema wilaya/Mikoa au wizara ziboreshe huduma zao za Tehama na waalimu kama ilivyo wafanyakazi wengine wawe wana log shida zao kwenye websites za wilaya au idara na zinashughulikiwa

Sometimes viongozi sijui huwa wanafikiria nini
 
Tunao supply mnatufikiliajie maana kupeleka huduma hamuwezi alafu mnawatuma waje kuchukua kwetu.
 
Porojo tu, huku Maswa mwalimu aliyehamia kutoka Arusha mpaka sasa hawajampangia kituo cha kazi.

Miezi miwili kupanga tu kituo cha kazi ni shughuli ya kufanikisha.
 
Yaani nikae ofisini na shida zangu nikisubir afisa elimu apite anisainie barua yangu?,je shule zipo ngapi za kutembelea?,je hayo mafuta ya kuzungukia anawapa?.Siungi mkono hoja ya namna hii mie.
 
Yeye angekuja na agizo la malimbikizo yote ya walimu yaliyohakikiwa na kuonekana ni halali yalipwe hapo walimu wangesema tumepata mtetezi .Watu wamesubiri kila mwezi malimbikizo yao ila kila mwezi hola.
 
He is out of touch with reality, au hata hajui hao waalimu huwa wanafuata nini huko halmashauri.

Yaani ukae shuleni unangojea huduma 🤣🤣.

Cha muhimu ni maombi ya watu yafanyiwe kazi kwa wakati, walimu wanalazimika kutembea ofisi kwa ofisi kuulizia 'progress' ya mafaili yao kwakua hayafanywi kazi kwa wakati.
NIna hakika 99% ni mwandishi ndio anatulishwa upupu, hajaelewa kilichosemwa.

Simjuia Bashungwa uwezo na upeo wake, lakini mtu timamu hawezi ku suggest mwalimu akiwa na lake jambo kichwani basi Halmashauri iote ndoto ijue alipo, ibebe vishikwambi na mafaili ya yule teacher iende ikamtembelee shuleni kwake...

Waandishi wetu ni vilaza wa kutupwa mashimoni....
 
Back
Top Bottom