Waziri Bashungwa alivyoanza kazi Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,806
11,968
Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Innocent Lugha Bashungwa ameripoti rasmi Wizarani na kulakiwa na Watumishi wa Wizara, wakiongozwa na Katibu Mkuu wa Wizara, Dkt. Faraji Kasidi Mnyepe.

Mapokezi hayo yamefanyika tarehe 04 Oktoba, 2022, mbele ya Jengo Kuu eneo la Mtumba. Mara baada ya kusalimiana na watumishi, Mheshimiwa Bashungwa aliingia ofisini kwake ambapo alipata fursa ya kusaini Kitabu cha Wageni kabla ya kuongea na Menejimenti ya Wizara.
310572105_1156481875248699_8429896519475725722_n.jpg


Akiongea na Menejimenti hiyo, Waziri amemshukuru Rais na Amiri Jeshi Mkuu, Mheshimiwa Samia Suluhu Hasa kwa kuendelea kumwamini na kumteua kuwa Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, ili aweze kuwa sehemu ya Wizara ili aweze kumsaidia katika utekelezaji wa majukumu yake ya kuliongoza Taifa letu.

Aidha, Waziri amesema kuwa kuteuliwa kwake kunatokana na imani kubwa aliyonayo Rais na Amiri Jeshi Mkuu kwake. Kwa maana hiyo, akaomba kupewa ushirikiano wa kutosha utakaomwezesha kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi kama alivyoaminiwa na Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan.

Amemshukuru pia, Katibu Mkuu na watumishi wa Wizara kwa ujumla wao kwa mapokezi na makaribisho mazuri, waliyompa mara tu baada ya kuwasili hapo Wizarani, ikiwa ni siku moja tangu ateuliwe na kuapishwa rasmi tarehe 03 Oktoba, 2022 Ikulu jijini Dar es Salaam.
310490640_102101022659439_6414418680702709139_n.jpg

Wakati wa Mkutano huo, Bashungwa ameainisha baadhi ya maeneo mbalimbali ya kipaumbele atakayoyapa uzito wa kipekee wakati anatekeleza majukumu yake. Baadhi ya maeneo hayo ni pamoja na kuendelea kuhakikisha usalama na ulinzi wa mipaka ya nchi unadumishwa, kuendelea kuliimarisha Jeshi kwa zana na vifaa, kuendelea kuboresha maslahi ya Wanajeshi na Watumishi wa Umma, utatuzi wa migogoro ya ardhi, pamoja na utawala bora.

Naye, Katibu Mkuu ambaye pia ni Mtendaji Mkuu wa Wizara, kwa niaba ya Menejimenti na watumishi wote amemkaribisha rasmi Wizarani na kumwaahidi kumpa ushirikiano wa kutosha kwa kipindi chote cha kuiongoza Wizara hii.

Innocent Bashungwa anakuwa Waziri wa kumi na tisa kuiongoza Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, tangu kuanzishwa kwake mwaka 1962.
 
Tutafutie test hata moya tangia 79 kwel,? mwisho hawa jamaa wanaota tumbo kubwa
 
Nimefutahi jinsi Urusi ilivyojimegea majimbo ya ukrane. Sisi tujachukue ziwa lote la Nyasa.
 
Back
Top Bottom