Waziri Bashungwa akata ngebe za Membe, Korosho yote yanunuliwa!.

Elitwege

JF-Expert Member
Jun 4, 2017
5,154
10,809
Waziri kijana wa viwanda na biashara baada ya kuteuliwa tu kushika wizara hiyo ,alifanya ziara kwenye mikoa yote inalima korosho ya Lindi na Mtwara, matokeo ya ziara hiyo ni kupata masoko nje ya nchi.

Kitendo cha serikali kupata masoko ya korosho imetafasiliwa kama kukata ngebe za Membe na Nnape ambao ilionekana wanajiimalisha mikoa ya kusini kupitia korosho iliyonunuliwa na serikali kukosa soko duniani, hivyo kuwafanya wakulima wa korosho waichukie serikali yao.
Ikumbukwe mara baada ya waziri Bashungwa kuwaita wafanyabiashara waje kununua korosho ,kuna baadhi ya makuwadi wa mabeberu waliwapigia simu wafanyabiashara hao na kuwaambia wasije kununua korosho hizo kwa sababu zimeoza kama vitunguu!!

My take .
Rais Magufuli alishaonya tangu mwanzo wa utawala wake kwamba huwa hakwamishwi ,na wote waliojaribu kumkwamisha walikwama wao. Kiki ya Membe na Nnape kupitia zao la korosho sasa imekwama.
Screenshot_20190823-210850.jpeg
 
Maisha ya mkulima watu wanayafanyia maigizo.

Ziara ya Lindi na Mtwara na soko la nje vina uhusiano kweli?

Hao wanaowapigia simu watu kuwaambia korosho zimeoza kwanini wasipelekwe mahakamani?

Meli ya kwanza kati ya ngapi?
 
Waziri kijana wa viwanda na biashara baada ya kuteuliwa tu kushika wizara hiyo ,alifanya ziara kwenye mikoa yote inalima korosho ya Lindi na Mtwara, matokeo ya ziara hiyo ni kupata masoko nje ya nchi.

Kitendo cha serikali kupata masoko ya korosho imetafasiliwa kama kukata ngebe za Membe na Nnape ambao ilionekana wanajiimalisha mikoa ya kusini kupitia korosho iliyonunuliwa na serikali kukosa soko duniani, hivyo kuwafanya wakulima wa korosho waichukie serikali yao.
Ikumbukwe mara baada ya waziri Bashungwa kuwaita wafanyabiashara waje kununua korosho ,kuna baadhi ya makuwadi wa mabeberu waliwapigia simu wafanyabiashara hao na kuwaambia wasije kununua korosho hizo kwa sababu zimeoza kama vitunguu!!

My take .
Rais Magufuli alishaonya tangu mwanzo wa utawala wake kwamba huwa hakwamishwi ,na wote waliojaribu kumkwamisha walikwama wao. Kiki ya Membe na Nnape kupitia zao la korosho sasa imekwama.View attachment 1188836
Kiinimacho hicho. Unajua zilikopelekwa korosho wewe? Kama hujui kaa kimya.
 
Ninaweza kumuamini mamba pale anaponiambia hawezi kung'ata kuliko kuamini kuwa korosho zote zimepata soko. Kwanza; kuna zile walizorudishiwa wakulima kwa madai ya kukosa ubora. Pili, muda uliopita tangu jeshi liendeshe hilo "zoezi" hadi leo sioni mnunuzi akinunua korosho zote kwa kuwa hazikuhifadhiwa vema.

I hope am wrong.
 
Watu wazima hawafundishwa kumpenda au kumchukia mtu au hata serikali. Matendo yanayofanywa na mtu/serikali kwa wananchi wake ndio hupelekea kupendwa au kuchukiwa

Hivi watu wa Chato kwa mfano utawashawishi vipi waichukie serikali na rais? Unafikiri kwanini?

Kama serikali inafanya mambo mazuri iache kupiga kampeni ili ipendwe watu si wataona tu kama wanvyoona wqtu wa Chato

Hata kama mtu huwapendi Nape na Membe ukweli mnawaonea tu kwenye hili la kuwatetea wakulima wa korosho kwa sababu wamefanyiwa faulo ya waziwazi kabisa ambayo hata mtoto mdogo aliiona

Anyways mnawazodoa Nape na Membe sio kwa sababu wanafanya jambo baya kuwatetea wananchi wakulima wa korosho ila ni kutokana na ile kauli ya mwanafalsafa Albert Einstein aliposema;

IT IS VERY DANGEROUS TO BE RIGHT WHEN THE GOVERMENT IS WRONG
 
Maisha ya mkulima watu wanayafanyia maigizo.

Ziara ya Lindi na Mtwara na soko la nje vina uhusiano kweli?

Hao wanaowapigia simu watu kuwaambia korosho zimeoza kwanini wasipelekwe mahakamani?

Meli ya kwanza kati ya ngapi?

Si uwaambie hao Wakulima waichague chadema basi unaona wanafanyiwa maigizo?
 
Back
Top Bottom