Waziri Bashungwa aagiza ukamilishaji wa ujenzi wa vituo vya afya 233 kabla ya Aprili 2022

Uongo upi mbona mapovu hivyo Mzee,unanichukia mimi au Samia aliyejenga? 😂😂
Pole sana, na nitarudia Ni Mh. Raisi Samia Suluhu Hassan sio Samia tu. Chuki ya nini? Kwani yeye ndie anayenilisha?

Ukijiangalia nankujitazama unajiona ulivojaa chuki...mwendazake ni nini? kama sio chuki? Inaeleweka umejaa chuki kwa sababu tu mlikuwa mmefungiwa mirija ya unyonyaji, sasa mnajikomba kwa Mh. ili muanze tena kutunyonya Watanzania.
Mapovu yamekujaa wewe.

Kamwe katika Ubuntu wangu hauwezi kunidhibiti hamwezi! na Propaganda zako na wana CCM wenzako mlioungana nao kuchochea mabadiliko ya mawazo na ufikiri wa Mwafrika utagota tu! Dingaan hapa bwa ha ha.

Usinibadilishie kibao hapo na hili sio ombi, hiyo saikolojia ya mizozo mizozo na mie nguli kawafanyie wakina wajinga na wapuuzi wenzako huko Exeter Hall bwahaaha
Huwezi kamwe kunipotosha, huwezi kunitisha tisha na hata kunivunja moyo au kunishawishi ili nikusujudie ww kama unavyotaka na longo longo zako. Genge lako litashindwa tu. Utalegea na kurudi machakani tu.

Utashindwa tu.
 
Wewe na mods mna wivu,ona mods wamebadili heading ya thread,karibia naacha kuanzisha nyuzi humu ntabakia ku comment kwa sababu haiingii akilini unaweka heading fulani afu wanabadili.
 
Twende kwenye mada.

Unaweza mbeza na kumchukia na ukamfanya vyovyote unavyojiskia ila ukweli itabakia pale pale kwamba rekodi anazoweka mh.Rais SSH hazijawahi kuwekwa na Rais yeyote aliyemtangulia.

Afya ikiwa ni moja ya kipaumbele chake, Serikali inajenga jumla ya vituo vya afya vipya zaidi ya 233 Kwa mpigo.

Hii ni sekta moja tuu ya Afya, ukienda sekta ya maji hivyo hivyo, barabara hasa za Tarura kote mambo ya bam bam.

Licha ya wenye chuki nae kuwa busy kutunga uongo na uzushi lakini ukweli wa kwenye Takwimu unambeba.

Mungu mbariki Rais wetu, huyu sasa ndio anafaa aongoze hadi achoke kama Angel Markel.

Kazi iendelee 👇

=============

BASHUNGWA AAGIZA UKAMILISHAJI WA UJENZI WA VITUO VYA AFYA 233 KABLA YA APRILI 2022

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Innocent Bashungwa ameziagiza Halmashauri zote nchini zilizopokea fedha kuanzia mwezi Oktoba – Disemba 2021 kwa ajili ya ujenzi wa vituo vya afya 233 kuhakikisha vinakamilika ifikapo tarehe 30 Aprili, 2022.

Akiongea na Waandishi wa Habari leo tarehe 16 Machi, 2022 baada ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa kituo cha afya cha Igawilo Halmashauri ya Jiji la Mbeya Mkoani Mbeya Waziri Bashungwa amesema halmashauri ambazo haitakamilisha ujenzi hawatapewa fedha za kuendeleza ujenzi.

Bashungwa amesema kwa Halmashauri zitakazoshindwa kukamilisha ujenzi kwa wakati uliotolewa na Serikali, Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi Watendaji wa Halmashauri watachukuliwa hatua za kinidhamu, hivyo amewaagiza Wakuu wa Mikoa yote nchini kuhakikisha wanasimamia ukamilishaji huo.

Ameagiza majengo yote ya kutolea huduma yaliyokamilika katika maeneo mbalimbali nchini kuanza kutoa huduma kwa wananchi na sio kuyaacha na kuwa kama magofu, watakaobainika majengo yamekamilika na hayatumiki serikali haitasita kuwachukulia hatua.

Vilevile, Waziri Bashungwa amesema Jumla ya shilingi bilioni 243.9 zimetolewa katika kipindi cha mwezi Julai 2021 hadi Februari,2022 kwa ajili ya ujenzi wa vituo vya kutolea huduma ya msingi .

Amefafanua kuwa fedha kiasi cha shilingi bilioni 113.7 ruzuku ya ndani kwa mwaka 2021/22 zimetumika kwa ajili ya ujenzi wa Hospitali za Wilaya 104, shilingi Bilioni 66.3 kwa ajili ya kuendeleza na kukamilisha Ujenzi wa Hospitali hizo ambazo zilianza ujenzi katika mwaka wa fedha 2018/2019 na 2019/2020.

Waziri Bashungwa ameendelelea kusema jumla ya shilingi bilioni 21.8 kwa ajili ya ukamilishaji na ukarabari wa vituo vya afya 61, bilioni 22.6 kwa ajili ya ukamilishaji wa zahanati 141 na ununuzi wa vifaa tiba bilioni 3.1 kwa ajili ya ununuzi wa vifaa tiba kwenye vituo vya kutolea huduma za afya.

Aidha, Jumla ya Shilingi billioni 44.5 zimetolewa kwa ajili ya ujenzi wa Majengo ya dharura 80, Wagonjwa mahututi majengo 26, Kituo cha matibabu ya magonjwa ya mliopuko 1 na Nyumba za watumishi 150(3 in 1) ambazo zitachukua familia 450.

Chanzo: TAMISEMI
😍
 
Hebu muwe mnatuwekea hata maeneo vinako jengwa hata kwa majina ya maeneo husika....isije kuwa ya ile ya REA eti vijijini takribani elfu 9 vina umeme kati ya vijiji elf 12 kumbe ni takwimu tuu
 
Hebu muwe mnatuwekea hata maeneo vinako jengwa hata kwa majina ya maeneo husika....isije kuwa ya ile ya REA eti vijijini takribani elfu 9 vina umeme kati ya vijiji elf 12 kumbe ni takwimu tuu
Jana niliomba anitajie majina ya vituo 10 Tu kati ya233 mpaka navyoongea hajavitaja

Hii nchi ngumu sana
 
Hebu muwe mnatuwekea hata maeneo vinako jengwa hata kwa majina ya maeneo husika....isije kuwa ya ile ya REA eti vijijini takribani elfu 9 vina umeme kati ya vijiji elf 12 kumbe ni takwimu tuu
Unakuta na wewe eti uligharamiwa na wazazi wako Hadi chuo Kikuu 😬😬😬

JamiiForums-443627714_375x463.jpg
 
Jana niliomba anitajie majina ya vituo 10 Tu kati ya233 mpaka navyoongea hajavitaja

Hii nchi ngumu sana
Kama ulienda shule kukuza makalio ,hiyo ni hasara yako na waliokuzaa ,non of my business..

Nilishakueleza kwa kuvipata kwamba chukua bajeti ya Tamisemi inayoishia utaviona au la ingia tovuti ya Tamisemi.

Kama huwezi hainihusu Baki na ujinga wako ilimradi umeona unakufaa.Tukutane 2025

JamiiForums-443627714_375x463.jpg
 
🤣🤣
Hawajambo hapo mtaa wa ufipa ?!!
Maandamano ya katiba mpya nchi nzima ni lini ?
Mkuu nisaidie kufikisha kilio changu kwa mods, yaani Hawa mods wamekuwa ni wafuasi wa chadema.

Ukiandika heading ya kumsifia mama wanabadili wanavyopenda wao kiasi kwamba nataka kuacha kutumia hili forums wameshakuwa wapuuzi.

Niliandika Samia aweka rekodi,ajenga jumla ya vituo vya afya 233 wamebadili heading Tena baada ya siku 5 toka nimeandika Uzi.

Pia niliandika Uzi wa RUWASA kusaini mikataba zaidi ya 86 haijawahi kutokea mama anaupiga mwingi wakabadili heading baada ya siku kadhaa,ni vyema wahariri wa jukwaa hili kama wao ni wapinzani wa Rais wawe wazi Ili waendeleee kutumia wao hili jukwaa,hii sio fair ila ukimsifu Mbowe wanafurahi na hawabadili heading.
 
Pole sana, na nitarudia Ni Mh. Raisi Samia Suluhu Hassan sio Samia tu. Chuki ya nini? Kwani yeye ndie anayenilisha?

Ukijiangalia nankujitazama unajiona ulivojaa chuki...mwendazake ni nini? kama sio chuki? Inaeleweka umejaa chuki kwa sababu tu mlikuwa mmefungiwa mirija ya unyonyaji, sasa mnajikomba kwa Mh. ili muanze tena kutunyonya Watanzania.
Mapovu yamekujaa wewe.

Kamwe katika Ubuntu wangu hauwezi kunidhibiti hamwezi! na Propaganda zako na wana CCM wenzako mlioungana nao kuchochea mabadiliko ya mawazo na ufikiri wa Mwafrika utagota tu! Dingaan hapa bwa ha ha.

Usinibadilishie kibao hapo na hili sio ombi, hiyo saikolojia ya mizozo mizozo na mie nguli kawafanyie wakina wajinga na wapuuzi wenzako huko Exeter Hall bwahaaha
Huwezi kamwe kunipotosha, huwezi kunitisha tisha na hata kunivunja moyo au kunishawishi ili nikusujudie ww kama unavyotaka na longo longo zako. Genge lako litashindwa tu. Utalegea na kurudi machakani tu.

Utashindwa tu.
Rubbish and nonsense
 
Wewe hao wote wanajengewa kadiri ya upatikanaji wa pesa.

Ukiona inakukata acha Kazi,huko private sector CO analiowa 300k afu wewe unabeza 700k ya nesi?
Hujanielewa kabisa mana nyie ndio muliojenga uovu na ufisadi na unafiki na rushwa kwenye nchi hii.

Mkoloni alikuwa mwema kuliko nyie mara mia mana aliweza kuajiri watu Kwa mishahara midogo lakini kwenye mazingira yenye kujenga uadilifu.

Huwezi ukamlinganisha Mfanyakazi wa umma na sekta binafsi ni upuuzi na ushenzi kuwalinganisha katika nyanja zote.

Kaulize taasisi za Dini hasa RC wanaweka mazingira Bora Kwa watumishi wao bila kujali kwanza mishahara.

Hivi unaona kuwa ni sawa kumtoa Daktari Mwanza mpaka Mtwara halafu hakuna nyumba ya daktari ya kuishi akapange mitaani. ?
Kwa Nini isiwe Kwa wabunge wenye mishahara mikubwa ,Kwa Nini isiwe Kwa Mwaziri wenye mishahara mikubwa ambao hawana hata kazi za dharura za usiku lakini wanapewa nyumba,walinzi,Dereva, gari na mafuta na mishahara mikubwa utadhani wao Wana tumbo mbili au tatu lakini Bado ndio wezi wa Mali za umma na mikataba ya kijinga kuliko Ile ya Chifu Mangungo.

Enzi za mkoloni na baadae serikali ya Tanganyika wafanyakazi wa mashirika ya umma na mashamba binafsi walipewa nyumba za kuishi ili wajenge uzalendo japo mishahara ilikua midogo.

Walafi na wezi wakauza nyumba za serikali ili wazitumie kupangishia watumishi wa umma Kwa Kodi kubwa ya pango huku wakijua kuwa mishahara yao ni midogo mmatokeo yake ni kuibuka Kwa wimbi la Wala rushwa na matumizi mabaya ya ofisi kulingana na urefu wa kamba. Ndiyo Tanzania ya Chawa.
 
Back
Top Bottom