TENGEFU
Senior Member
- Jan 25, 2017
- 138
- 206
Sisi ni wakulima tunaozalisha kwa mkataba kwa makubaliano na wakala wa mbegu za serikali yaani agricultural seed agency (ASA) yenye makao yake mjini Morogoro na matawi mikoani. Msimu wa kilimo wa mwaka 2021 tulifanikiwa kuzalisha mbegu na kuwauzia ASA kwa mujibu wa mkataba. Katika hali ya kawaida tulitakiwa kuwa tumelipwa hela zetu by December 2021.
Ilipofika November 2021 wakulima wote baada ya kukabidhi mbegu tuliandika barua ya kuomba malipo kama ilivyo kawaida. Leo ni mwishoni mwa January 2022 ASA wamenyamaza kimya na hawataki kutulipa malipo yetu ya mamilioni ya shilingi. Tunapofuatilia kwa maafisa wakuu akiwemo mkurugenzi wa Uzalishaji Dr. Justin Ringo na engineer Sumuni wanatupa majibu ya mitaani mfano. Hela itawekwa tu. Tunapofuatilia malipo kwa simu hawa hawa akina Ringo na Sumuni wamekuwa hawapokei wala kujibu simu zetu na hawaleti mrejesho ni kwa nini hatupewi fedha zetu.
Wengi wetu tumekopa hadi Milioni 20 kupata mkopo wa kuzalisha kwa ajili ya ASA na tumeanza kuuza baadhi ya mali zetu kulipa madeni kwa sababu tulitegemea malipo ya kazi yetu yangetuwezesha kulipa madeni.
Mh Bashe naomba utusaidie ili tuweze kulipwa hela zetu na hii taasisi ambayo ni ya serikali
NB: Msimu wa kilimo unaanza maeneo mengi na ni hakika sisi tunaozalisha kwa ajili ya ASA ni dhahiri hatutaweza kuingia mkataba maana mtaji wetu umeshikiliwa na hawa ASA bila maelezo yoyote.
Tafadhali tusaidieni ili turudi tena kuzalisha
NB: ASA ni taasisi ya serikali iliyoko ndani ya Wizara ya Kilimo na makao yake makuu ni Morogoro